Kubomolewa ukuta wa Hotel ya Crest Arusha Rais amekashifiwa?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kubomolewa ukuta wa Hotel ya Crest Arusha Rais amekashifiwa??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Marigwe, Dec 22, 2009.

 1. M

  Marigwe JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2009
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Baada ya TANROADS Arusha kubomoa uzio wa wa hoteli ya Crest iliyofunguliwa siku kama tatu au nne zilizopita kumekuwepo na madai kadhaa kuwa Rais kakashifiwa. Wanasiasa wengine wamedai uongozi wa mkoa uwajibike. Yafuatayo ni maoni yangu:

  1. Rais alienda kufungua hoteli na siyo kitu kingine na hoteli ilifunguliwa na inafanya kazi. Nasema Rais hajakashifiwa.
  2. TANROADS walienda kubomoa uzio ambao ulijengwa kwenye Road reserve baada ya kuwa wametoa notice kisheria.Notice haikuwa ya kuvunja hoteli bali uzio. Walichofanya TANROADS ni sahihi. Hawakubomoa hoteli iliyofunguliwa na Rais. Rais hajakashifiwa. Kashfa ni yake mwenye hoteli kwa kukaidi maagizo ya TANROADS.
  3. Hoteli bado iko intact. Anachotakiwa kufanya ni kujenga uzio eneo linalokubalika kisheria. Mimi ni mkazi wa Baraa na ninayo nyumba upande huo huo ambako hoteli hiyo ilipo. Nilipokamilisha kujenga nyumba yangu which is 50 metres from the centre of the road, uzio wa ukuta nilikuwa nimejenga ndani ya road reserve kiasi cha mita moja. Nilipewa notice na manispaa wakati huo ya kuuondoa ukuta. Ukuta-mind you- siyo nyumba. Sikubisha. Nilichukua mafundi nikawapa kazi ya ‘kubomoa’ ukuta kwa kutoa tofali moja baada ya nyingine hadi ukuta ukawa haupo tena. Matofali hayo hayo nikajengea ukuta mwingine mita 10 ndani zaidi. Hakuna kilichoharibika. Nilitimiza wajibu wangu kwa kuwa raia mtiifu wa sheria.
  4. Sasa swali nauliza. Kashfa kwa Rais hapo iko wapi? Baadhi ya wanasiasa wanataka uongozi wa mkoa uwajibike kwa kumpotosha Rais kweli wako sahihi?
  5. Ninakumbuka mwaka 1971 Rais Nyerere alikwenda kufungua jengo la IPS likiwa linamilikiwa na AgaKhan, siku ya pili jengo hilo likataifishwa na serikali iliyokuwa chini ya Nyerere na akapewa Msajili wa Majumba. Nyerere hakukosea. Yeye alialikwa kufungua jengo. Lakini sheria ya Acquistion Buildings Act ya 1971 ikachukua mkondo wake. Mlio watu wazima huenda mnalijua hilo. Sasa JK kaenda kufungua hoteli na hoteli bado inafanya kazi kashfa hapo iko kwa JK au kwa mwen ye hoteli? Jamani let us be objective. Aliekashifiwa hapo ni Bwana Tarimo wala siyo Kikwete.
  Mwenye hoteli ajilaumu mwenyewe asitake kumuingiza Rais kwenye upuuzi wake. Yeye sasa ndiye anaetaka kumkashifu Rais. Akajenge uzio kama sheria inavyotaka. Watu wengine jamani!!!
   
 2. M

  Mende dume Member

  #2
  Dec 22, 2009
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mkuu kwani kukashifiwa nini? Kashfa hiyo kwa Rais ni udhaifu wa vyombo vya usalama. Rais anapaswa kujua anafungua hotel ya nani, ipo wapi, wadau ni nani, tax implication etc, pamoja na uhalali wa hotel yenyewe in terms of vibali vya ujenzi, na system kama inavyotakikana.

  Elewa kuwa tatizo linaanza pale ambapo Rais anaingia kufungua mahoteli, mara mgodi, hii ina funga midomo ya watendaji wengine na ndo ugumu unapotekea. Rais anatudhalilisha sisi naye anadhalilika pia, kwani pindi TRA wakitaka kujua kodi imekaa vipi, mdaiwa ana access ya ikulu.
  ufunguzi wa hotel, wapo wahisika mkoani au wizara ya utalii, au hata TBS wazee wa viwango. Rais anapaswa kushughulikia investiment za kutisha na za kitaifa au kimataifa sio tu miradi ya mafisadi binafsi. Kesho ukiambiwa hotel hiyo ni ya Mramba, unaanza kujiramba, oo sikujua.

  think big, tatizo na sie wabongo vichwa mboga.
   
 3. M

  Mende dume Member

  #3
  Dec 22, 2009
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa nyongeza, kashfa kwa Rais, katika hili inakuja kama vile wateuliwa wake wanapokuwa na vyeti feki! kitendo cha kuteuliwa kilipaswa kuanza na uhakiki wa taarifa binafisi ambazo ni pamoja na elimu kwa uhakika. Utamwitaje mtu Dr, eti ana PhD aliyo ichukua kwa miezi 18, akiwa na Bachelor lower Second! nawe unamwita Dr so and so! unamwita mtu prof, ukim-google, prof yake inaonekana toka webu za magazeti ya ndani. which means ni Ikulu tu ndo wanajua kuwa huyu ni prof. Thats rubbish!

  Mie najitoa kwenye ile 70% ya kufuata upepo, simo!
   
 4. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #4
  Dec 22, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mkuu hapo nilipo-bold ndiyo umenail it. Watanzania tuna mentali ya kuvunja sheria kwa makusudi kwa tegemeo kuwa fulani yupo sehemu fulani atanikingia kifua. Nafikiri kitendo cha huyu mwenye hotel kuhakikisha rais anaifungua wakati akijua kuwa yupo kwenye disputy na TANROADS ilikuwa ni mbinu ya kuwanyamazisha hao TANROADS. Ila mimi binafsi ninampongeza sana JK kwa kukubali kuifungua hotel hii na kisha soon TANROADS wanavunja uzio, itatoa funzo kwa wengine kuzingatia sheria na kufuta mawazo ya somebody will be defending me against authorities' actions.

  Umefika wakati sasa tuache kulindana tuache sheria ichukue mkondo. KUDOS JK, KUDOS TANROADS. Together we can change the sick minds of people who don't want to follow the law.
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  dah TANROADS kiboko.
  wamepiga buti la ugoko am soooooooo happy
   
 6. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #6
  Dec 23, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kama alijenga ndani ya barabara alitegemea nini? Sheria imechukuwa mkondo wake!
   
 7. G

  GeraldP Member

  #7
  Dec 23, 2009
  Joined: Mar 27, 2008
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Nadhani mwenye hotel ajenge upya sehemu inayoruhusiwa malumbano yaishe!
   
Loading...