Kubomoa nyumba 20,000 kwa mkupuo, huyu kweli sio mwanasiasa

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Jamaa wakati wa kampeni alisema kua yeye sio mwanasiasa na hajui siasa, na kweli nikiangalia haya matukio aliyofanya ndani ya miezi 2 tu hili linadhihirisha kweli sio mwanasiasa.

1. Kubomoa nyumba nyingi za wananchi kwa mkupuo mmoja.

2.Kukataza safari za nje, na kutuma wawakilishi kwenye safari yake yeye.

3.Kutimua wakurugenzi na maafisa mbalimbali kazi.

4. Kuanza kufukuza wageni kwa haraka haraka.

Sisemi anafanya vizuri au vibaya ila haongozi kwa kutumia siasa
je siasa ni nzuri au mbaya kwa uongozi mkubwa kwa nchi?
 
Last edited by a moderator:
Uongozi unataka mambo mengi sana ila kwa nchi yetu ilipokafikia ilibidi tumuweke huyu makusudi maana waliokuwa wanaongoza kwa siasa na ustaarabu tuliishia kuwatukana na kuwaita dhaifu sasa tumemuweka ambae sio dhaifu. Kanyaga twende baba tupo nyuma yako watu 20,000 sio mbaya kwa maendeleo ya watu 50 millions
 
wewe PIMBI hv unajua nyumba 20,000 zna zaid ya watu 300,000?

jiulize kwa nin makamba kapingana na maneno yake wakat wa kusitisha bomoabomoa!

wanamshaur vbaya JPM kwa kutafta kuonekana wana uwezo kumbe ni kujichimbia kaburi!

watu laki 3 ni zaid ya idadi ya watu ya waliomuweka madarakani rais wa zanzibar! so shut up
 
Sasa kipi bora tuwatoe mabondeni ili wasife na mafriko au tuwaokoe kwa kuwatoa mabondeni? Tutumiage akili mda mwingine sawa
 
wewe PIMBI hv unajua nyumba 20,000 zna zaid ya watu 300,000?

jiulize kwa nin makamba kapingana na maneno yake wakat wa kusitisha bomoabomoa!

wanamshaur vbaya JPM kwa kutafta kuonekana wana uwezo kumbe ni kujichimbia kaburi!

watu laki 3 ni zaid ya idadi ya watu ya waliomuweka madarakani rais wa zanzibar! so shut up
Lakini wakati huo kumbuka majanga yakiwapata hasa mafuriko wanachi wanaililia sana serikali na maneno mengi utayasiki kwenye media kuilaumu serikali ,kutoka kwa hao hao,

Nadhan hatanserikali imeona inaingia gharama kila mwaka mfuko wa maafa kwa watu wa mabondeni serikali inagharimia wahanga , sasa hali hii hadi lini?? kuna umuhimu wa kutafuta suluhu ya kudumu na labda suluhu ninimhapa?
Kuzuia mvua?.kuzuia mafuriko ???au ni ipi zaid za kuwatoa wanao ishi maeneo hatarishi? Maana hakuna namna ya kuzuia mafuriko mabonden maana ndio njia sahihi ya mafuriko, sasa suluhu ninini hapa?

Hakuna suluhu zaid ya kuwatoa watu huko maana tumeshuhudia mafuriko hayo yakileta maafa pia na uharibifu sasa hali hii hadi lini? Tuache kuingiza siasa katika mambo yanayo hitaji utaalamu ,

Mimi mwenyewe kuna nyumba ya mzee wangu imepigwa x na hatuna namna imebidi tuhamishe wapangaji na tutoe baathi ya vifaa ambavyo vyaweza tumika tena kama bati,blocks ili vikajenge hata kibanda sehemu sahihu,,

Na nikweli pale mahala kipind cha mvua walikuwa wanapata tabu wale watu , maji yana jaa ndan kiasi kwamba wanaogopa hata kuongeza furniture kuhofia uhamishaji wakati wa masika.

Tukubali tu kuwa suluhu ya kudumu ili kutatua tatizo hili ni kutoa watu huko lakini pia itumike busara waoneshwe kwa kwenda ,ingawa kati yao kuna walio kwisha pewa maeneo ya kuhamia kipind cha nyuma wakayauza tena , na hao nao pia bado wanadai tena waoneshwe kwa kwenda ! Katika hili kuna wanao stahili kuhurumiwa na ndio hao tunaiomba serikali iwaoneshe mahali mbadala lakini kuna wengine hawastahili kuhurumiwa hata kidogo kwa ukaidi.
 
hivi mimi nawauliza mliwahi kutembelea skwata za bonde la msimbazi na kuona hali ilivyo
Wewe umewahi kufika Kibera Nairobi? Kwa nini makazi yale hatarishi sana kwa jiji zuri kuliko Dar hayabomolewi kwa mpigo? Watu wa Msimbazi bondeni wanapaswa kuondolewa lakini sio kwa operesheni kubwa kama mko vitani vile.
 
Siongezi mkuu
 
Ndio mana kenya walizima mawasiliano kwa simu feki miaka mitatu iliyo pita na tanzania tutazima mwezi wa sita mwaka huu, tanzania imechoka kuwa nchi ya kuiga inabidi ifike mahali tanzania iwe nchi ya kuigwa, hivyo tusisubiri aanze kenya kubomoa ndio tanzania pia tuige, sidhan kama kenya ni role model ya tanzania.
 
Mm siungi mkono hiyo bomoa bomoa ata kama anataka kupanga jiji si kwa mwendo huu
Wewe ulitaka kwa mwendo gani? watanzania ndivyo walivyo. wanataka maisha mazuri lakini kazi hawataki, wanataka miji mizuri kama ulaya lakini kubomoa vijumba vya ovyo hawataki,wanataka amani lakini kufuata sheria hawataki, wanataka elimu bure lakini kutoa kodi hawataki yaani ni shida.MHESHIMIWA MAGUFULI WEWE FUATA SHERIA TU BASI UTAFANIKIWA.
 
Ndio mana kenya walizima mawasiliano kwa simu feki miaka mitatu iliyo pita na tanzania tutazima mwezi wa sita mwaka huu, tanzania imechoka kuwa nchi ya kuiga inabidi ifike mahali tanzania iwe nchi ya kuigwa, hivyo tusisubiri aanze kenya kubomoa ndio tanzania pia tuige, sidhan kama kenya ni role model ya tanzania.
LOOOK look here, sio kuwa watu wanapinga kubomoa zile nyumba hapana, ila kwa vile tayari kulishakuwa na makosa makubwa hata kwa upande wa serikali na ujue yale ni makazi ya watu wake kwa waume na watoto na ni raia wa nchi hii lazima utaratibu wa kiutu ufanyike sio kama vita.
Tunashukuru hilo serikali imeliona na kulikubali ndio maana imebadili style ya kukabiliana nalo.
 
Wewe umewahi kufika Kibera Nairobi? Kwa nini makazi yale hatarishi sana kwa jiji zuri kuliko Dar hayabomolewi kwa mpigo? Watu wa Msimbazi bondeni wanapaswa kuondolewa lakini sio kwa operesheni kubwa kama mko vitani vile.
Shauri waondolewaje
 
LOOOK look here, sio kuwa watu wanapinga kubomoa zile nyumba hapana, ila kwa vile tayari kulishakuwa na makosa makubwa hata kwa upande wa serikali na ujue yale ni makazi ya watu wake kwa waume na watoto na ni raia wa nchi hii lazima utaratibu wa kiutu ufanyike sio kama vita.
Tunashukuru hilo serikali imeliona na kulikubali ndio maana imebadili style ya kukabiliana nalo.
Naungana na hoja yako 100%
 
Swala sio siasa au la bali kusahihisha makosa ya miaka 10 bila Rais!! Nchi ilikwenda hobelahobela kwa sababu ya kejeli, mipasho na ngonjera nyingi huku wizi, ufisadi na rushwa vikiimaliza nchi. JPM mwendo mdundo!
 
Back
Top Bottom