Kubomoa Naura Spring Hotel ni komoakomoa sio bomoabomoa

teh teh teh achaneni na story za vijiweni...

Mnasema ni la Mkapa, sasa jiulize Magufuli angekubali Mkapa abomolewe..

Wengine wanasema na Museven, teh teh story za kwenye kahawa hizo mkuu...
Chalii wangu hizo sio story za kwenye kahawa ,huo ndio ukweli Unafikiria Mkapa jana alifuata nini Ikulu ???
 
ka
Heshima yenu wakuu,

Mimi nimeanzisha hii thread kulaani kitendo cha Watanzania kushindwa kujiongeza na kurudishana nyuma. Mimi sioni kama kuna haja ya kukomoana kwa kutumia nafasi tulizonazo kisiasa au kiuchumi.

Nianze kwa kusema kwamba Tanzania ni Nchi ya Vyama vingi, na Mtanzania yupo huru kuunga Mkono chama chochote anachopenda.

Usitegemee kwamba utagombea nchi ya vyama vingi wote wakuunge mkono. Huu ni wakati wa kutibu majeraha ya Uchaguzi na Kujenga Nchi yetu iwe na Umoja amani na Maandeleo sio Muda wa Kukomoana.

Nitoe tahadhari katika hili, siku zote unaweza ukamkimbiza mjusi akakimbia, lakini akiona amezidiwa anageuka nyoka na kuanza kukukimbiza wewe.

Mimi kuna Maswali yananitatiza;

1.Hili Jengo hadi linajengwa Serikali haikuwepo?

2.Je, alipewa Vibali vya kujenga na wakaguzi walilikagua?

4.Aliyeruhusu kujengwa kwa jengo hili kachukuliwa hatua gani?.

5.Kwanini Serikali isiingie garama ya hili jengo?

6.Imekuaje Kuanzia Msingi jengo mnaliona hadi lifike hatua hii ndo ulibomoe? Huu ni uzalendo?

7.Hakuna njia mbadala ya kufanya ili hili jengo lisibomolewe?

Hili jengo Mahakama ndiyo ilimruhusu ajenge baada ya kushinda kesi dhidi ya Manispaa ya Arusha kumzuia Kujenga.

Eti inavunjwa kisa ipo bondeni. Mbona maji hayaingii ndani? Mto Sanawari Miaka yote upo na hili jengo halijawahi kusitisha shughuli kisa maji yameigia wala hapajawahi kutuwama maji.

Hii itakuwa Hotel yake ya pili kuwekewa X baada ya moja ya Mwanzo kuwekewa alama ya X.Impala Hotel, Leopard Tours Offices kuvunjwa.

Kama ndivyo, Basi tufanye hii Nchi iwe ya chama Kimoja. Nchi hii ni yetu sote. Nchi kwanza Vyama baadae. Roho za kukomoana zishindwe kwa jina la Yesu.

Arusha Wamechagua Mabadiliko, Wapigwe mabomu, wapigwe risasi, wabomolewe, wanyimwe huduma za kijamii, vyovyote vile mtakavyo fanya haisadii.

View attachment 315535 View attachment 315536
kama iko bondeni piga chini sio kuleta siasa. la msingi kama haina vigezo kisheria piga chini. kwamba nani aliona hajaona mradi sheria ilikiunkwa bomoa. hii ndio kutumbua majipu na mtumbua majipu mungu ametujalia tumempata tumuombee atumbue hadi jipu la mwisho.
 
Chalii wangu hizo sio story za kwenye kahawa ,huo ndio ukweli ?? Unafikiria Mkapa jana alifuata nini Ikulu ???
teh teh teh kwahiyo Mkapa alienda ku reconcile na JPM...

Ila ile Investment na Ngurdoto ni 50 by 50 na Ben.. Impala ni 100% yake
 
teh teh teh kwahiyo Mkapa alienda ku reconcile na JPM...

Ila ile Investment na Ngurdoto ni 50 by 50 na Ben.. Impala ni 100% yake
Impala sina tatizo nako najua hapo mrema ana own 100% ila huku kwengine jamaa ni mwamvuli tu though ana % yake
 
Hatuhitaji kufanya costs benefits analysis tunapo tekeleza sheria kwa wavunja sheria..tukifanya hivyo basi sheria zitaendelea kuvunjwa...!
Teh teh teh!Kitu muhimu kinachoangaliwa katika kutafsiri sheria ni lengo la kutungwa kwa sheria husika, ukitafsiri sheria kama juha unaweza kujikuta hufikii malengo ya sheria husika.
Je unajua lengo la kuondoa shughuli za kibinadamu ndani ya mita sitini kutoka mtoni?
Je sheria hii ipo applicable katika mazingira yote?
 
Mleta mada anadai kuwa Manispaa ilishawahi kuzuia nyuma lakini wakashindwa kesi mahakamani.

Kisheria sidhani kama wana mamlaka hayo ikichukulia kwamba Mmiliki amejenga pale kisheria. Hiyo kesi itabidi irudi tena mahakamani!!
Huyo unayeongea nae kakulia Bukoba kaja Dar kusoma Chuo na alivyomaliza kapata kibarua hapo Lumumba..

Kule Arusha anaenda wakipataka vimikutano vya CCM au wanasheria, haijui Arusha hapa anapiga siasa tu..
 
Haha lulu wa ngarenaro najua yupo Uk ila hawa wengine tokea kitambo wako Aus ,,haha ndio sheria yenyewe hiyo wape pole sana
Vipi ulifanya makabrasha hapo kwa Lulu... teh teh teh

Sasa Mzee wakimpiga chini hizi Hotel zake mbili itabidi watoto warudi kuomboleza..
 
Mleta mada anadai kuwa Manispaa ilishawahi kuzuia nyuma lakini wakashindwa kesi mahakamani.

Kisheria sidhani kama wana mamlaka hayo ikichukulia kwamba Mmiliki amejenga pale kisheria. Hiyo kesi itabidi irudi tena mahakamani!!
Manispaa kushindwa case haimaanishi kuwa jamaa ndio yuko sahihi...huyo jamaa anajulikana alitumia pesa kushina na kuendelea kujenga! Umepita pale Naura?
 
Heshima yenu wakuu,

Mimi nimeanzisha hii thread kulaani kitendo cha Watanzania kushindwa kujiongeza na kurudishana nyuma. Mimi sioni kama kuna haja ya kukomoana kwa kutumia nafasi tulizonazo kisiasa au kiuchumi.

Nianze kwa kusema kwamba Tanzania ni Nchi ya Vyama vingi, na Mtanzania yupo huru kuunga Mkono chama chochote anachopenda.

Usitegemee kwamba utagombea nchi ya vyama vingi wote wakuunge mkono. Huu ni wakati wa kutibu majeraha ya Uchaguzi na Kujenga Nchi yetu iwe na Umoja amani na Maandeleo sio Muda wa Kukomoana.

Nitoe tahadhari katika hili, siku zote unaweza ukamkimbiza mjusi akakimbia, lakini akiona amezidiwa anageuka nyoka na kuanza kukukimbiza wewe.

Mimi kuna Maswali yananitatiza;

1.Hili Jengo hadi linajengwa Serikali haikuwepo?

2.Je, alipewa Vibali vya kujenga na wakaguzi walilikagua?

4.Aliyeruhusu kujengwa kwa jengo hili kachukuliwa hatua gani?.

5.Kwanini Serikali isiingie garama ya hili jengo?

6.Imekuaje Kuanzia Msingi jengo mnaliona hadi lifike hatua hii ndo ulibomoe? Huu ni uzalendo?

7.Hakuna njia mbadala ya kufanya ili hili jengo lisibomolewe?

Hili jengo Mahakama ndiyo ilimruhusu ajenge baada ya kushinda kesi dhidi ya Manispaa ya Arusha kumzuia Kujenga.

Eti inavunjwa kisa ipo bondeni. Mbona maji hayaingii ndani? Mto Sanawari Miaka yote upo na hili jengo halijawahi kusitisha shughuli kisa maji yameigia wala hapajawahi kutuwama maji.

Hii itakuwa Hotel yake ya pili kuwekewa X baada ya moja ya Mwanzo kuwekewa alama ya X.Impala Hotel, Leopard Tours Offices kuvunjwa.

Kama ndivyo, Basi tufanye hii Nchi iwe ya chama Kimoja. Nchi hii ni yetu sote. Nchi kwanza Vyama baadae. Roho za kukomoana zishindwe kwa jina la Yesu.

Arusha Wamechagua Mabadiliko, Wapigwe mabomu, wapigwe risasi, wabomolewe, wanyimwe huduma za kijamii, vyovyote vile mtakavyo fanya haisadii.

View attachment 315535 View attachment 315536
Acha blaa blaa hapa, umepewa siku90 bomoa.
 
Naijua historia ya mzee mrema vizuri sana manake mimi nilikua projects advisor wake kwa miaka...mambo mengi sana hapo ni maneno tuu ya mitaani..Naura sio ya mrema wala sijui kigogo aliestaafu hizo ni hadithi tuu. Naura ni ya bwana mdogo Kabila congo na nikwambie kwamba kickstart capital ya kwanza nili authorize B59 as a start...mengine yoote ni kweli kama mfano kiwanja kilinunuliwa toka kwa ccm..na kesi kweli ilikwenda mahakamani ni kweli kabisa lakini kumbukeni kwamba kipindi cha utawala ule palikua hakuna kesi...mrema alikua anaandika memo tuu inakwenda moja kwa moja mpaka kwa pinda wakati mwingine mpaka kwa mkuu wa kaya mimi nilikua shahidi. Mrema yeye anakula only 20% kama administrator tuu..hotel ilio yake ni impala tuu...ngurdoto niko mpaka na mpaka blackbook of owners secrets kila mtu ana share gani...hapo yuko mkapa...yuko director of eco bank..msimwone sumaye kakimbia ccm mkajua adui nae yumo na percentage pale...kuna mengi saana hapa kwenye hili
 
Jamaa ana HATI na kibali cha ujenzi? Je wakati wanatoa HATI hawakujua kama hapo ni bondeni?/ Je hizo gharama za ujenzi nani atazilipa?
mwenye jengo hili si mgeni na sheria za ujenzi mijini kwani ni tajiri na ana majengo mengi hapa mjini. hati alizonazo alizipata baada ya kupenyeza rupia kwa maafisa mipango miji hadi mahakamani. mbona hili liko wazi. jina lenyewe ni chanzo cha maji kilicho jirani kabisa. unataka kuniambia mwenye jengo hakujua pale si sahihi kuotesha jengo lile? alijua, ila enzi hizo za 'penye udhia penyeza rupia' alitumia msemo huu kukidhi haja yake ingawa alijua ni kinyume na sheria. na hapo arusha wako wengi

makosa lazima yasahihishwe na kila mtu lazima atambue tofauti ya serikali iliyopo madarakani hivi sasa na ile iliyopita. ujanjaujanja au matumizi ya nguvu ya fedha hayana nafasi awamu hii.

rula imewekwa, lazima lazima mstari unyooke. hapa kazi tu.
 
Wacheni city plan ziwe reviewed tunataka miji ya kisasa tuwe kama Pretoria,mpango wa kuwa Giant lazima kuwe na misimamo na mipango kabambe
 
Kwa jinsi Tanzania ilivyo kwa sasa, mtu anaweza kupata kibali cha ujenzi kwa kuhonga wala hiyo sio shida.Na kama alipata kibali kwa mgongo wa nyuma,hastahili compensation yeyote,kwa kuwa kufanya hivyo itakuwa ni ku-reward uovu.Hili litakuwa fundisho baya kwa wengine.

Swala la kwani hawakuona ujenzi ukiendelea halina msingi wowote,the bottomline is kosa limefanyika.Lini nachukua hatua huwezi kunipangia and is none of your business.

Watanzania inabidi tuwe serious,hatuwezi kuendelea kuvunja sheria halafu tutegemee kuhurumiwa.Jawabu ni kutovunja sheria.Tumekuwa yahe yahe mno.

Basi wote waliohusika wachukuliwe HATUA, hii sio kwa NAURA tu hadi jangwani, msimbazi nk... Viongozi wote waliopokea Rushwa na kuuza /kuidhinisha maeneo ya mabondeni/wazi wachukuliwe hatua
 
Hatukatai anatumia sheria ila sheria ikipitiliza inakuwa sio sheria tena ni udicteta kwa sbb amesaidia pia Kutoa ajira. Kwa vijana wasiokuwa na ajira. Zikibomolewa hao wafanyakazi wataenda wapi.
Mkuu mawazo ya aina hii ndo yameifikisha hii nchi hapa!! Mabadiliko yana gharama na machungu yake lazima watu wachache waumie kwa manufaa ya kizazi kijacho la sivyo watoto wetu watakuja kutuona wazazi wao hatukuwa na akili kichwani..!!
 
hivi mtiririko wa maji hupungua kutokana na chanzo kupunguza kutoa maji au maji yanapopita? Unataka kutuambia kwamba hiyo Hoteli imejengwa kwenye mapito ya maji. Lakini pia kuna kitu nakijua kuhusu viongozi wetu, ni wajinga sana wanapotaka kuonesha kwamba wao wana nguvu!
Cc. Makonda
 
mwenye jengo hili si mgeni na sheria za ujenzi mijini kwani ni tajiri na ana majengo mengi hapa mjini. hati alizonazo alizipata baada ya kupenyeza rupia kwa maafisa mipango miji hadi mahakamani. mbona hili liko wazi. jina lenyewe ni chanzo cha maji kilicho jirani kabisa. unataka kuniambia mwenye jengo hakujua pale si sahihi kuotesha jengo lile? alijua, ila enzi hizo za 'penye udhia penyeza rupia' alitumia msemo huu kukidhi haja yake ingawa alijua ni kinyume na sheria. na hapo arusha wako wengi

makosa lazima yasahihishwe na kila mtu lazima atambue tofauti ya serikali iliyopo madarakani hivi sasa na ile iliyopita. ujanjaujanja au matumizi ya nguvu ya fedha hayana nafasi awamu hii.

rula imewekwa, lazima lazima mstari unyooke. hapa kazi tu.

Kama alitumia Rushwa kulipata na kujenga basi anavuna alichokipanda. Kwahiyo hizo serikali zilizopita viongozi wake wanachukuliwa hatua GANI?
 
mto Naura una bonde gani? Mbona kuna taasisi kibao kuanzia TRA, Mount Meru Hospital, CEDHA, Polisi quarters, Polisi kituo cha kati etc. Kuvunja Naura Spring ni kuhujmu Uchumi which is a crime. Sio kupotect mazingira hata kidogo. Ni wivu na visasi baada ya kukosa rushwa pale mahakama ilipotoa hukumu dhidi ya manispaa.
Serikali ya Magufuli isidhani itakaa madarakani for ever. Hayo mambo anayofanya sio aliyotumwa na wanachi afanye.
 
Back
Top Bottom