Kubenea Wale Ndio Watesi Wako Kweli?

FDR Jr

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
249
8
Katika taarifa za za habari jana usiku na leo magazetini kumejitokeza kitu cha kufadhaisha sana hususani ktk suala zima la mwanahabari Kubenea na mzee Tega.

Sipendi kuhitimisha ila nimepatwa na mashaka na wasifu wa wale jamaa waliofikishwa mbele ya Pilato. Wale jamaa ndio waliomsurubu Kubenea kweli? Au polisi wameamua kumridhisha kwa kuitikia wito wake wa 5-7 days wakamatwe la sivyo atawaanika wote waliomtishia maisha.

Binafsi namtaka Kubenea atoke clean na kutueleza kama wale ndio watesi wake au la.

Ni hayo tu ndg zangu
 
Katika taarifa za za habari jana usiku na leo magazetini kumejitokeza kitu cha kufadhaisha sana hususani ktk suala zima la mwanahabari Kubenea na mzee Tega.

Sipendi kuhitimisha ila nimepatwa na mashaka na wasifu wa wale jamaa waliofikishwa mbele ya Pilato. Wale jamaa ndio waliomsurubu Kubenea kweli? Au polisi wameamua kumridhisha kwa kuitikia wito wake wa 5-7 days wakamatwe la sivyo atawaanika wote waliomtishia maisha.

Binafsi namtaka Kubenea atoke clean na kutueleza kama wale ndio watesi wake au la.

Ni hayo tu ndg zangu


Jana nimemsikiliza ubene akihojiwa Times FM, alinisikitisha sana.
Kwa kifupi kesi hii itakuwa kama ile ya Ditopile, haitafika kokote na kwa maelrezo niliyoyasikia jana kwa KUBENEA, tusditegemee lolote. kuna kila dalili kuwa kisha onja asali na la kusema tena hana.
 
Watafiti fuatilieni hili jambo ili tujue huyu bwana Kubenea kama anaendelea kututendea haki kwa mujibu wa maadili
 
Anatakiwa atoke mbele na kusema ukweli kwani bila kuusema ukweli watammaliza kabisa ,na silaha nzuri ya kujilinda ni kusema ukweli mbele ya jamii na sio kujificha ......
 
Haha that is when JamboForums maintain motto yake, hapendwi mtu....kama anasema uongo hataka kama alimwagiwa sumu, atasemwa tu!
 
Suala si ni kina nani wamekamatwa, lengo ni kuwapata wale waliowatuma na nini ilikuwa motive yao!
 
Masatu kutiki Mukaruka wesu . Watesi ni watesaji. Walimtesa Kubenea.

Naamini sasa Kubenea kama Deo mwadishi wa habari zamani Taznania Daima sasa anajikomba huko kwa akina RA atakuwa kalamba . Nimekosa maongezi yake hebu sema alicho kisema tafadhali .
 
Nimekuwa nikifuatilia hawa wahanga wote wawili, interview ya Tegambwage pale chanel Ten mzee alitumia muda mwingi kutuonyesha kuwa yeye ni mtu wa kazi na mpiganaji interms of kurusha ngumi,mahojiano yale yalijaa bashasha ya mzee wetu na kupoteza dira yote ya mjadala ulokusudiwa na hadhira.
Hakuwa wazi ktk maelezo yake zaidi ya kuwashukuru marafiki na taasisi mbalimbali zilizompa pole. Binafsi nilichoshwa na kile nilichokuwa nakiangalia pale toka kwa mwalimu wa wana habari.
Jana ktk group ya wale watuhumiwa walioletwa mahakamani kwakweli haikuleta picha sahihi ya maharamia na pia media nazo zimemripoti Kubenea naye kuleta maelezo yaleyale ya Mshauri wake.

Ninamuomba ajitokeze hadharani na kututhibishia kuwa wale jamaa wa jana pale mahakamani ndio waliomdhuru.Kitendo cha kuwaleta wale mahakamani ni wazi Kubenea amewatambua kuwa ndio wahusika,sasa chochoko yangu ni kugeuka kwa maneno baadaye.

Wana Jf endeleeni na kuusaka ukweli juu ya hili na pia Kubenea mwenyewe ajiangalie kama anatutendea haki wapenda amani au ni mchezo wa kuigiza na kuchafuana.
 
Inawezekana kwamba Kubenea (lakini simfahamu... hii ni speculation tu!) ni 'mtafutaji' na kila 'mtafutaji' hutafuta, akiacha kutafuta ujue kwamba 'kishapata' alichokuwa akikitafuta.

Kujitokeza ama kutojitokeza hadharani kwa Kubenea ndiko kutatudhihirishia kwamba 'kishapata' ama la!

./mwanahaki
 
KUBENEA DO SOME JUSTICE MAN, STAND UP AND SAY SOMETHING, AMA UTADHARAULIWA UTAONEKANA KUWA WEWE NI WALEWALE, WE STILL RESPECT YOU MAN, THEN DO THE RECIPROCATE.
 
mnakumbuka kuna news jamaa walituma huku kwamba jamaa alifanya B....N,wakashindwana ndio ikatokea hivyo,,so sikutaka kuamini kwa hili ila najaribu kuvuta subira """LISEMWALO LIPO NA KAMA ALIPO BASI """""****Ja..tusubiri ,,ila kwa taarifa tu wale sio wenyewe na kama ni mtu anaekwenda kanisan ama msikitini atasema ukweli pamoja na mwenzie,,,,ukweli utaonekana tu
 
2.jpg
 
Kwa vile kesi iko mahakamani na bahati nzuri Kubenea hakupofuka macho yake ukweli utajulikana tu,natumpe nafasi ya kutudhibitishia hilo.
 
Kwa vile kesi iko mahakamani na bahati nzuri Kubenea hakupofuka macho yake ukweli utajulikana tu,natumpe nafasi ya kutudhibitishia hilo.

Kwa dhati kabisa nakubaliana nawe lakini bado tunahitaji kumuona hapa JF akitupatia hizo fact.
 
Sasa akija 'hewani' si atavuruga/'atainterfere' ushahidi? Wenyewe si ndio mashahid namba moja?
Ukiona kimya hawajasema chochote basi wamekubaliana na hali inavyoendelea.
au na wao wanafanya utafiti wao
na watasema/watatoa vithibiti siku watakayoitwa mahakamani.
Sisi tuendelee kuvuta subira ili tuje tuone 'other side of the coin!
 
La muhimu ni kuwa kama Kubeana anaufahamu ukweli wa tukio hilo na unahusisha wale jamaa(mafisadi)basi kuendelea kukaa kimya ndio hatari kwake.Atoke hadharani na kusema kwa sauti kuu tumsikie na umma utakuwa naye kama ilivyo kwa Dr. Slaa na wenzake wote walioamua kushtakia maovu kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom