Kubenea: Tutarejesha UDA Kwa Wananchi

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
SAED Kubenea, Mbunge wa Jimbo la Ubungo amesema, Halmashauri ya Jijiji la Dar es Salaam itahakikisha umiliki wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) unarudishwa kwa umma, anaandika Pendo Omary.

Tayari ripoti iliyotolewa jana mjini Dodoma na Profesa Mussa Assad, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) inaeleza hisa za UDA zilithaminishwa kwa bei ya Sh. 744.79 kwa kila hisa Oktoba 2009 na Novemba 2010 thamani ya kila hisa ikiwa Sh. 656.15.

Katika uuzwaji wa UDA, Bodi ya Wakurugenzi ya UDA ilitoa punguzo la asilimia 60 kwa kila hisa kwa mwekezaji bila kuwapo sababu za kufanya hivyo.

Kulingana na mkataba wa kuwasilisha hisa wa 11 Februari 2011, mnunuzi (kampuni ya Simon Group Limited) alitakiwa kulipa Sh. Bilioni 1.14 kwa bei ya ununuzi wa hisa zote.

Hata hivyo, mnunuzi alilipa Sh. 285 Milioni pekee katika akaunti namba OJ1021393700 ya benki ya CRDB inayomilikiwa na UDA.

Idd Simba, Mwenyekiti wa Bodi alipokea kiasi cha Sh. 320 milioni kupitia akaunti yake binafsi kutoka kwa mwekezaji ambapo kwa mujibu wa Simba, ni ada ya ushauri alioutoa kwa mwekezaji jambo ambalo linaonesha kuwepo kwa mgongano wa masilahi.

Akizungumza na MwanaHALISI Online leo asubuhi Kubenea amesema, “alichokisema CAG kuhusu UDA kimedhihirisha ambacho tumekuwa tukikisema muda mrefu. Mchakato mzima wa uuzwaji wa UDA ulikuwa wa rushwa, wizi, udanganyifu na matumizi mabaya ya madaraka.

“Sisi wabunge wa Dar es Salaam kupitia muungano wetu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) tumedhamiria kuirejesha umiliki wa UDA kwa umma kwa asilimia 100.”

Amesema, kwa sasa vikao vya halmashauri ya jiji hilo vinafanyika mfululizo na vitapitia mkataba wa UDA kwenda kwa mwekezaji Kampuni ya Simon Group Limited, mkataba kati ya kampuni Simon Group Limited na Hazina na mkataba kati ya UDA na wakala wa Mradi wa Mabasi yaendayo kasi (DART).

“Tunataka kuona mali zote za UDA zipo wapi? Tumeambiwa hati za UDA zimewekwa benki. Tunataka kujua ni zipi na za gharama gani. Tunamtaka Rais John Magufuli atuunge mkono katika hili,” amesema Kubenea.
 
Kubenea Maskini hajui sera ya Chama chake ni ya kiliberali ambayo inasisitiza Serikali kutojishughulisha na shughuli za uendeshaji wa shughuli zenye muelekeo wa kibiashara.
Unafikia hadhi ya Mbunge hujui kutofautisha kati ya Ilani na Sera!
Lolote la kukupa Kick unalivamia bila ya kuzingatia msingi Mkuu wa sera au ilani.
 
ile kesi yao ilifutwa kwa nolle, kwasababu ya tuhuma kwamba hosea hakutaka wafungwe, nolle inaruhusu kufungua upya kesi hivyo inaweza kuanza upyaaa kabisa. mkurugenzi wa pccb huyu mpya tunaomba asiwe kama hosea. aanzishe upya hiyo kesi na hao mafisadi wafungwe, na UDA irudi. haiwezekani uda ikawa asilimia nyingi vile kwa Robert kisena wa simon group. hisa zote kapewa mtu kama zawadi tu hivyo? na magari haya mapya ndio anaenda kufaidi mtu binafsi?
 
Kubenea Maskini hajui sera ya Chama chake ni ya kiliberali ambayo inasisitiza Serikali kutojishughulisha na shughuli za uendeshaji wa shughuli zenye muelekeo wa kibiashara.
Unafikia hadhi ya Mbunge hujui kutofautisha kati ya Ilani na Sera!
Lolote la kukupa Kick unalivamia bila ya kuzingatia msingi Mkuu wa sera au ilani.
Nivizuri kabla yakupanua mdomo ushirikishe ubongo kwanza
 
Unaonekana unajua vizuri, tumia jukwaa hili ueleze maana ya "SERA" ili angalau ujipe uhalali kwa muda wa kuwaponda wenzio.
 
Nivizuri kabla yakupanua mdomo ushirikishe ubongo kwanza

Usipanik twende taratibu. Utaratibu wa serikali kuendesha huduma ya usafirishaji ni moja ya features za ujamaa. Chama chenu ni cha kiliberali kinachofata sera za soko huria inakuaje mnapigania sera za CCM so mmegundua sera zenu haziuziki au hamjui kabisa masuala ya sera nyie ni kukimbia tu bila ya kujua mnakimbilia wapi?
 
Baada ya kuona mapendekezo ya CAG ameamua kudesa na kujidai hiyo ndio sera na ilani yake...matapeli wa kisiasa wana tabu sana
 
Kubenea Maskini hajui sera ya Chama chake ni ya kiliberali ambayo inasisitiza Serikali kutojishughulisha na shughuli za uendeshaji wa shughuli zenye muelekeo wa kibiashara.
Unafikia hadhi ya Mbunge hujui kutofautisha kati ya Ilani na Sera!
Lolote la kukupa Kick unalivamia bila ya kuzingatia msingi Mkuu wa sera au ilani.

Maliberali CUF hata wenje anajua.
 
SAED Kubenea, Mbunge wa Jimbo la Ubungo amesema, Halmashauri ya Jijiji la Dar es Salaam itahakikisha umiliki wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) unarudishwa kwa umma, anaandika Pendo Omary.

Tayari ripoti iliyotolewa jana mjini Dodoma na Profesa Mussa Assad, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) inaeleza hisa za UDA zilithaminishwa kwa bei ya Sh. 744.79 kwa kila hisa Oktoba 2009 na Novemba 2010 thamani ya kila hisa ikiwa Sh. 656.15.

Katika uuzwaji wa UDA, Bodi ya Wakurugenzi ya UDA ilitoa punguzo la asilimia 60 kwa kila hisa kwa mwekezaji bila kuwapo sababu za kufanya hivyo.

Kulingana na mkataba wa kuwasilisha hisa wa 11 Februari 2011, mnunuzi (kampuni ya Simon Group Limited) alitakiwa kulipa Sh. Bilioni 1.14 kwa bei ya ununuzi wa hisa zote.

Hata hivyo, mnunuzi alilipa Sh. 285 Milioni pekee katika akaunti namba OJ1021393700 ya benki ya CRDB inayomilikiwa na UDA.

Idd Simba, Mwenyekiti wa Bodi alipokea kiasi cha Sh. 320 milioni kupitia akaunti yake binafsi kutoka kwa mwekezaji ambapo kwa mujibu wa Simba, ni ada ya ushauri alioutoa kwa mwekezaji jambo ambalo linaonesha kuwepo kwa mgongano wa masilahi.

Akizungumza na MwanaHALISI Online leo asubuhi Kubenea amesema, “alichokisema CAG kuhusu UDA kimedhihirisha ambacho tumekuwa tukikisema muda mrefu. Mchakato mzima wa uuzwaji wa UDA ulikuwa wa rushwa, wizi, udanganyifu na matumizi mabaya ya madaraka.

“Sisi wabunge wa Dar es Salaam kupitia muungano wetu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) tumedhamiria kuirejesha umiliki wa UDA kwa umma kwa asilimia 100.”

Amesema, kwa sasa vikao vya halmashauri ya jiji hilo vinafanyika mfululizo na vitapitia mkataba wa UDA kwenda kwa mwekezaji Kampuni ya Simon Group Limited, mkataba kati ya kampuni Simon Group Limited na Hazina na mkataba kati ya UDA na wakala wa Mradi wa Mabasi yaendayo kasi (DART).

“Tunataka kuona mali zote za UDA zipo wapi? Tumeambiwa hati za UDA zimewekwa benki. Tunataka kujua ni zipi na za gharama gani. Tunamtaka Rais John Magufuli atuunge mkono katika hili,” amesema Kubenea.
Mungu aendelee kuwaongoza ukawa ,ili maendeleo yapatikane haraka
 
Viva mbunge!!!!!
 
Baada ya kuona mapendekezo ya CAG ameamua kudesa na kujidai hiyo ndio sera na ilani yake...matapeli wa kisiasa wana tabu sana
Aliye anza kuongelea juu ya hili ni meya wa jiji. Akafuata makonda, CAG na sasa Kubenea. Ila sijui Mh Kubenea kama alizungumzia jambo hili katika kampeni yake 2015 au kabla.
 
Usipanik twende taratibu. Utaratibu wa serikali kuendesha huduma ya usafirishaji ni moja ya features za ujamaa. Chama chenu ni cha kiliberali kinachofata sera za soko huria inakuaje mnapigania sera za CCM so mmegundua sera zenu haziuziki au hamjui kabisa masuala ya sera nyie ni kukimbia tu bila ya kujua mnakimbilia wapi?
Sipendi tabia za CHADEMA Ila na wewe hapa umekurupuka ,kwenye mambo ya msingi unaleta ujinga
 
Usipanik twende taratibu. Utaratibu wa serikali kuendesha huduma ya usafirishaji ni moja ya features za ujamaa. Chama chenu ni cha kiliberali kinachofata sera za soko huria inakuaje mnapigania sera za CCM so mmegundua sera zenu haziuziki au hamjui kabisa masuala ya sera nyie ni kukimbia tu bila ya kujua mnakimbilia wapi?
Sijapanic ni wewe kuleta mambo yako ya ulumumba kwenye vitu vya msingi
 
Wewe ndie unaeshangilia UDA irudishwe kwny Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam bila ya kujiuliza litaendeshwaje?

Study zote kubwa Duniani na Practise zinataka serikali ijitoe kwny uendeshaji wenye muelekeo wa biashara na kazi ya serikal hubaki ku regulate kama vile kupitia SUMATRA. Kama hatukubaliani na uendeshaji wa kina Robert Kisena tunapaswa kuitisha upya tenda badala ya kutuletea uzalendo wa kinafki eti Halmashauri iendeshe mradi wa Speed bus. Wanashindwa kukusanya uchafu barabarani wataweza kuendesha mradi mkubwa namna ile au nanyi mnatafuta kitalu cha kuiba?
 
Back
Top Bottom