Kubenea Tuambie Sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kubenea Tuambie Sasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Yona F. Maro, Mar 8, 2008.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Mar 8, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli napenda kumpa pole rafiki na ndugu yetu kubenea kwa mikasa ambayo amekuwa akikabiliana nayo.Ila nina mashaka na story ya jana aliyosema kuwa alipigiwa simu na watu asiyo wafahamu kuwa watamuuwa kwa kuwataja vigogo wa kuu wa Richmond.Kwangu mimi nilishangaa maaana hata kamati teule hajaweza kuthibitishia bunge na watanzania kuwa Richmond ni nani? Sasa kumbe yeye kubenea anawafahamu!!!!.

  Mimi Lowassa sio ndugu yangu wala simuungi mkono kwa ufisadi na hasara waliyoiletea taifa ila nimekuwa nikisoma sana habari za kubenea anaonekana kama ana fisa na Lowassa au kuna kikundi cha watu watamtumia ili andike habari za kumchafua mwanasiasa huyu kwa sababu tu za kisiasa. Amekuwa bingwa wa kubuni habari juu ya lowassa hata kama hazina ukweli ilimradi tu ziweke mazingira ya kumchafua.Mfano kwa akili tu ya kawaida kama mtu anataka kukuuwa watakupigia simu kweli!!!! na wakueleze kosa lako! hii sitakuwa rahisi kujua na kuwakamata!!!!!,Kwangu mimi nimeona kama ni story nyingine tu ya Kubuni kama ilivyo kawaida ili mradi lowassa achafuke na aonekane mbaya.

  Mwanzoni nilikuwa nikifatilia habari alizokuwa akiandika kuhusu Richmond na nilimlaumu sana Lowassa moyoni lakini jinsi siku zinavyozidi kwenda naona wala issue sio richmond kuna jambo jingine ambalo hatujalijua.

  Na wasihi maskini watanzania wenzangu kuwa tusipende kupoteza muda na issues ambazo haziwezi kuleta maendeleo tusizipe kipauwu mbele,mikataba vibovu yote ifichuliwe ila kufichua mikataba isiwe ndio ndira ya taifa hebu tuweke national chartered mfano,kwa kueleza madini ya mkoa wa mara yanawezaje kuwaletea watu wa singinda na mtwara maendeleo? au issue kama za elimu afya ,kilimo zifanyweje ili kumkwamua mtanzania.Vinginevyo itakuwa nchi ya porojo tu.

  Pia tabia za wivu na majungu hazitaweza kutusaidia sana,nasema hivyo kwa kuwa tangu mwaka jana tumekuwa tukipata email zenye majina ya watoto wa vigogo BOT, ila sikuona jina la mtoto wa kikwete.kumbe alikuwa ameajiriwa na private firm, leo nashangaa wanamuhusisha na ufisadi wa BOT wakati hela za EPA zinaibiwa alikuwa hajaajiriwa ila alikuwa anafanya kama internship tu,Hivi kwa akili za kawaida wanafunzi wanaofanya internship wanaweza kutoa uwamuzi mzito unaohusu jambo lolote ofisini? sasa huyu Ridhawani aliwezaje kushirikishwa katika mkataba wa deep green? na wakati huo kikwete hakuwa rais.

  Je kama watoto wa vigogo wana sifa zote za kuajiriwa ina maana hawana haki ya kufanya kazi hapa Tanzania? Tujiulize haya maswala ya mtoto wa nani ana fanya kazi wapi atasaidiaje maendeleo ya nchi.wachunguzwe kama watanzania wengine kama utendaji wao ni mbovu basi wafukuzwe lakini sioni kama ina maitiki kuifanya major issue,kuna vitu vya maana zaidi na vinavyogusa maslahi ya wengi kuliko hili. Naungana na wote wanaopinga ufisadi kwa asilimia 100 ila na wakumbusha kuwa tuvipeleke sambamba na other development issues,mabadiliko yatatokea,hata kama ni CUF,CHADEMA au TLP ipo madarakani
   
 2. H

  HeartBreaker Member

  #2
  Mar 8, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi sijui kama Ridhwani alihusika au la, ila kuhusu hiyo bold ni kukuonyesha tu kwamba inawezekana akahusishwa vilevile coz watu huangalia nani anaweza kutusaidia wapi kivipi kwenye swala flani. So kama waliona wanaweza kumtumia somewhere kwa sababu flani, kuwa intern hakumzuii kuitwa kusaidia kazi iende mbele.
  Na kuhusu Kubenea ,hao watesaji wake wanaweza kufanya lolote, wanaweza kumpigia na kumwambia kosa lake au la, so we cant be in a position kusema haiwezekani, kila kitu kinawezekana under the sun. Sasa unataka kusema Kubenea anamchafua lowassa, mbona ye mwenyewe alishajichafua zamani. Na alivyopigwa na kumwagiwa tindikali pia alikuwa anasingizia? au ali tafuta wale watu mwenyewe?
   
 3. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  si bure na ww una lako jambo na kubenea...
   
 4. Ericus Kimasha

  Ericus Kimasha Verified User

  #4
  Mar 8, 2008
  Joined: Oct 27, 2006
  Messages: 488
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 60

  Ndugu Maro,
  Naheshimu sana mitazamo na michango yako iliyopita majamvini. Ila kwa mchango wako wa sasa naomba kutofauiana nawe na pia kutahadharisha kama unapenda kulinda hadhi yako. Najua freelance wengi sana sasa wanataka kupata walau sehemu ndogo ya mgao wa akina Balile. Kwa wale walikwisha fanikiwa na wanoweza kufanikiwa hiyo ndiyo itakuwa safari yao. Issues ya kuwatetea mafisadi kina EL na RA ghalama yake ni kubwa mbele ya jamii.

  Ushauri wangu wa bure hilo dau la "agenda 21" hata ukilikuta limedondoshwa barabarani usiokote. Na jitihada zozote za kuweka ID na true name ili wakujue na kukutafuta kama mwenzao ni maombi ya uanachama kwenye genge la Majasiri wa Kifisadi. Wewe ni kijana mwema, lizika na visenti halali.
   
 5. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  We nawe una lako jambo hapa, lakini unaweza kuwa unasaidia uchunguzi kufanikiwa.

  Kwa habari yako hii unataka kutueleza kuwa Lowassa ndo anayemfanyia mambo yote kubenea sio?? maana Kubenea anaandika mambo ya Ufisadi kwa wahusika wote sio Lowassa tu, sasa iweje wewe unamhusisha Lowassa pekee, kama yeye ndo anafanya hizo jitihada tueleze.

  Pili huwezi kuniambia kuwa watoto wa Vigogo ndo wenye uwezo wa kuajiri BOT tu, sio kweli hapa, kwanini wawe wao tu, kuajiriwa sio sababu, sababu ni kwanini BOT kuwe kumejaa watoto wa Vigogo??

  Kama ulisoma Thread ya jana kuajiriwa kwa Ridhiwan IMMA kunamashaka, IMMA wanachukua First class ikishindikana kabisa upper second, lakini mchangiaji mmoja alitwambia jana kuwa Ridhiwan alipata Pass, kama alifaulu sana anayo Lower second, sasa huoni kuwa inawezekana aliingia kwa ajili ya kusaidia mambo fulani fulani hapa, kwa sababu hakuwa na vigezo vya kuajiliwa pale??

  Mamluki wengi sana ndani ya JF, kwani hata Mafisadi nao wanachangia kwa kusema tunajenga nchi kumbe wanauma na kupuliza.

  Kazi ipo, ila tutafanikiwa tu
   
 6. S

  Siao Member

  #6
  Mar 8, 2008
  Joined: Jan 4, 2008
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ebo...! Ukija vibaya ujue pia huponi...!

  Hivi vichwa vya jf navipenda mno jamani!!

  Kazi kwelikweli!!!
   
 7. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Mkuu Shy,

  Vipi tena na wewe umejiunga na Lowassa sasa? Hivi muandishi mkubwa kama wewe eti mpaka leo hujui kwa nini Kubenea alimwagiwa tindikali? Eti hujui kuwa aliandika kuhusu Lowassa kuondolewa madarakani, na pia hiyo ndiyo siku alikuwa ametoka kuhojiwa na kamati ya Mwakyembe, na akasema yote anayoyajua kuhusu Richimonduli, ambayo ndio hasa uti wa mgongo wa ripoti nzima ya Rcihimonduli na ndiyo siku alipomwagiwa tindikali, wewe unasema hujui haya? Salva Rweyemamu, mkurugenzi wa Ikulu akishasema kuwa Richmond ni ya Rostam, wewe unasema hakuna anyejua ni ya nani?


  Mkuu ni nani hapa aliyekuuliza kama una uhusiano na Lowassa, maana ni wewe mwenyewe unayetuambia kwa maneno yako kuwa una something na Lowassa, kwa sababu kama unaaamini unayosema ni ukweli mtupu na sio propaganda then hukuwa na sababu ya kuweka mkwara kuwa Lowassa, sio ndugu yako na blah! Blah!

  Huwezi kuwa na tatizo na hasara iliyoletwa na Lowassa, ambayo wewe mwenyewe unasema haijathibitishwa na bunge kama Lowassa anahusika, mbona unajichanganya mkuuu? Kubenea amekuwaje bingwa wa kubuni habari ambazo wewe mwenyewe huzijui, sasa umejuaje kuwa anazibuni na ni za uongo against Lowassa na wewe Lowassa sio ndugu yako?

  Mkuu Shy, kweli wewe mtu kichwa unaweza kuleta hii habari ya nonesense hapa JF?

   
 8. K

  Kalamu JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2008
  Joined: Nov 26, 2006
  Messages: 874
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Shy:
  Just a friendly advice. You call yourself a 'freelance writer and online researcher?' You really need some heavy training, if you need to be a qualified dude in that area.

  Stori yako hapo juu haina mwelekeo, inajichanganya kila sehemu. Kama unataka watu wakuamini hata unaposema habari zisizokuwa na ukweli ni bora mawazo yako yawe na mpangilio wa ushawishi kidogo.
   
 9. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2008
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  I have always been suspicious of this guy...remember his fairytale that he was once kidnapped...and was question about JF?
   
 10. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2008
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Amani iwe kwenu Wana JF,
  Pamoja na ushauri mzuri wa Ntareheirungu na wana JF wengine, nashawishika kuhisi ID za Shy au Yona Fares Maro "Freelance writer" kama alivyojiweka wazi zimevamiwa mwisho wa wiki hii.

  kule ethinktank ameleta kali ya mwaka. Anakaribisha watumiaji wa mtandao wa celtel kujiunga kwenye yahoogroups account. Mod wa kule ametoa dukuduku lake lakini nami sipati jibu kama Corporate Company kama Celtel inaweza kutumia free goods kama hiyo yahoo kwa wateja wake.

  Nami nakushauri kama kweli ni Fares upumzike ili upunguze maluweluwe ya radiations from our Hg computers. Tumia siku ya kesho kuomba Bwana akurudishie fikra pevu kama awali. Wana JF siku zote husamehe na kusahau makosa ya wanaotubu toba ya kweli. EL na AR pia natumaini twaweza kuwasamehe iwapo wataeleza ukweli, watubu na kurejesha fedha zetu. NdG. Fares, NI MAONI YANGU TU NA MTAZAMO!
   
 11. Mtu Mzima

  Mtu Mzima JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ndugu Shy,
  Ina maana hata wajumbe wa kamati ya bunge waliochunguza Richmond waliposema wanapokea sms za vitisho walikuwa wanatoa story za kubuni?.Kama wajumbe wa kamati ya bunge wametishiwa maisha,Kubenea ni nani asitishwe?.Mara ya kwanza alipokea vitisho kama hivyo na baadae akamwagiwa tindikali nayo pia alidanganya?
  Njoo na utetezi mwingine ndugu yangu,suala la kutishiwa maisha ni muhim kupewa uzito unaostahili hati itakapothibitishwa vinginevyo
   
 12. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #12
  Mar 8, 2008
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Baada ya hapo kaingia mitini. Utetezi mwingine bwana!!!

  Amekuwa Tomaso mpaka aone mtu kachinjwa ndiyo ataamini Kubenea alipigiwa simu ya Kifo.
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Mar 8, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,384
  Trophy Points: 280
  Polisi si wanaweza kuangalia tu na kusema "hakupokea simu yoyote wakati huo" na hivyo habari yenyewe ni ya kubuni
   
 14. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #14
  Mar 9, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  huu ni unafiki ndugu yangu

  Matumizi mabaya ya taaluma ya uandishi na uchunguzi, au tujue ulikuwa darasa moja la Propaganda na mzee Kingunge???

  Inaonesha Shetani anafanya kazi yenye nguvu sana ktk kuushawishi moyo wako kuamini kuwa dhambi inaweza kumpa mtenda dhambi utakatifu. Haya tueleze jambo gani hilo unalolifahamu kaka yetu??

  Mbinu za kipropaganda hizi. Masikini sisi wa Tanzania tunaujua ukweli na tunauona ukweli, je tusipoteze muda kuutafuta ukweli na kuusimamia?? Ninadhani wewe mwenzetu siyo masikini wa tanzania au umeridhika na kila jambo hata likuue vipi huioni hatari kwa vizazi vijavyo...

  Halafu msomi mtimilifu hutumia reference hata akitumia quotes za kujenga hoja, Nakumbuka hii quote ya wivu na majungu waliowahi kuitumia ni Mzee Mkapa na Msekwa pale walipobanwa kusema ukweli wa misimamo yao fulani isiyo na tija kwa Taifa.

  Mwisho hapa ninaweza kusema kuwa heri mimi sijasema, ila ninamashaka sana nawe ndugu Maro, na kwa kuwa umekuwa vilevile ukianzisha hoja na kukimbia kuzijibu basi pasipo shaka tunayatafuta majibu ndani ya lines za hoja zako.
   
 15. M

  Mugishagwe JF-Expert Member

  #15
  Mar 9, 2008
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 295
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Amekwisha sema Lowasa ni ndugu yake sasa unauliza nini zaidi ya hili ambao kasema ? Kumsafisha si lazima kutumia nguvu kwa wajanja .Yeye anatumia soft language ili baadaye aungwe mkono .
   
 16. K

  KakindoMaster JF-Expert Member

  #16
  Mar 9, 2008
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 1,349
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Kweli nimekubali Mafisadi wananguvu sana. Hivi na kijana wetu ameisha tekwa nyara? Twambie Mkuu Shy maana siamini ninachokisoma.
   
 17. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #17
  Mar 9, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kuna habari mpya nilizozisikia kijiweni pale Kkoo kuhusu huyu bwana Kubenea, nilisikia kuwa haku fanyiziwa kwa sababu za kisiasa bali ni ufuska, ilizungummzwa kuwa huyu bwana anapenda sana vidosho na alikuwa akicheza na mke au bibi wa mtu na jamaa alisha mpa warning lakini hakusikia ndio matokeo yake yakawa hivyo, Kubenea nakupa pole kwa yaliyokufika no matter iwe ni kisiasa au kama nilivyosikia mitaani.

  Hebu wewe mwenyewe tuambie ukweli, kwani nina uhakika unjaua na wale jamaa tulioambiwa wameshikwa kuhusiana na kuumizwa kwako, imekuwaje?
   
 18. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #18
  Mar 9, 2008
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  kama wauwaji wanataka kutoa onyo kwa wengine basi hii ya kupiga simu ni moja ya mbinu watakazotumia ile wengine waogope wakijua kwamba na wao kifo kitawakuta.
   
 19. M

  Mugishagwe JF-Expert Member

  #19
  Mar 9, 2008
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 295
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  darisalama
  Kama issue ya kupigwa ingalikuwa connected na Ufuska kwa polisi wa Tanzania hadi sasa wangalisha sema .Wanajiuma maana wanajua ukweli wa issue uko vipi achen utani .
   
 20. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #20
  Mar 11, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145

  Sikupenda kuchangia suala hili, lakini nimeguswa na maneno niliyoweka msisitizo wa rangi. Aliyepiga simu aliuliza, "we ndiye unayeandika story za Lowassa?" alipojibu ndiyo, akaambiwa, "sali zala zako za mwisho" sasa hebu fikiria wewe hujui kama aliyepiga simu alimtaja Lowassa, lakini sasa unatuambia hayo maneno, kwanini USISAIDIE POLISI?, maana siku ile story iliyoandikwa ilimhusu mtoto wa Kikwete kwa maana kwamba si Lowassa pekee anayeandikwa, lakini wewe unasema Lowassa!!!! Hebu tusaidie kaka mwenzetu asiendelee kutishwa ama kumwagiwa tindikali.

  Unashangaza sana, kuonyesha kwamba haya ni mambo ya utaniutani wakati mtu alifanyiwa jambo la kweli, hakuna anayeweza kujifanya akamwagiwa tindikali na hawezi kujifanya akakatwa mapanga mtu kama Ndimara. Rais wa nchi (Kikwete) hawezi kuruhusiwa na Usalama kwenda kumtizama mtu anayefanya SANAA!!!Hebu tumia akili kidogo tu!!!
   
Loading...