Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 125,657
- 239,129
Mh , Mara tu ulipotangazwa mshindi wa kiti cha ubunge wa jimbo la Ubungo , uliahidi mambo mawili ya kuyashughulikia kwa haraka sana , watanzania wenzako wanakuamini na kwamba hujawahi kuwa muoga , uwezo wa kuyatimiza unao .
1. Uliahidi kuhakikisha UDA na mali zake zote zinarejeshwa kwa wenyewe wananchi wa Dar es salaam maana mkataba wa kuuzwa kwake una utata mkubwa, Taarifa za wadukuzi zinadokeza kwamba hata hizi sarakasi za umeya lengo lilikuwa kujaribu kuwalinda wahusika .
2. Uliahidi kuhakikisha kwamba Mahakama ya jiji inafutiliwa mbali maana imewekwa kwa lengo la kukomoa masikini , mahakama hii kwa miaka yote imekuwa kero kubwa kwa Mama lishe , Machinga na Wajasiria mali wengine wadogowadogo
Kwa mfano , pamoja na askari wa jiji kudaiwa kupora mali za wafanyabiashara ili kuweka ushahidi mahakamani lakini wenyewe wanapozifuatilia baada ya muda mfupi hawazikuti !
kibaya zaidi hata Wali na maharage wa mamalishe unachukuliwa kama ushahidi lakini baada ya masaa machache yanakutwa masufuria matupu , je wali umepelekwa wapi ?
Nimeona nikukumbushe hili mkuu maana ndiyo mambo uliyoahidi kuyashughulikia kwa Haraka sana.