Kubenea: Sikusema Makonda ni Mjinga,mpumbavu,kibaka na cheo chenyewe cha kupewa

JANA KATIKA MFULULIZO WA KESI YA MBUNGE WA UBUNGO KUBENEA VS MAKONDA; KATIKA UTETEZI WAKE KUBENEA ! SIJASEMA MAKONDA ‘’MJINGA ,MPUMBAVU,KIBAKA NA CHEO CHENYEWE CHA KUPEWA’’ HAKIMU.
ILA NILISEMA MAKONDA NI MTEULE WA RAISI NA MIMI NIMECHAGULIWA NA WANANCHI

IWAPO KUBENEA ATAKUTWA NA HATIA KUNA
1.KUPOTEZA UBUNGE KAMA ILIVYOKUWA KWA MAREHEMU FARES KABUYE MBUNGE WA BIHARAMULO VS CHOYA

2.KULIPA GHARAMA ZA KESI NA FIDIA JUU.

3. UCHAGUZI KUTANGWAZA UPYA JIMBO LA UBUNGO/
Mkuu, tujulishe kuwa hii ni kesi ya Uchaguzi, ya Jinai au ya Madai.
 
KUBENEA NDIE RAISI HALALI WA JIMBO LA UBUNGO! HAKA KAJAMAA UTEUZI WAKE UNAWEZA KUTENGULIWA NA RAISI HATA SAA8 UCKU.
 

lg.php

hii-620x308.jpg

Saed Kubenea, Mkurugenzi Mtendaji wa Hali Halisi Publishers Ltd na pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoka mahakamani

DENIS Mujumba, Mratibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi, ambaye pia alikuwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kinondoni amefura baada ya kuulizwa maswali wakati akitoa ushahidi wake kwenye kesi ya jinai inayomuhusu Saed Kubenea, Mkurugenzi Mtendaji wa Hali Halisi Publishers Ltd na pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo.

Mujumba (39) amefikwa na masaibu hayo baada ya kubanwa kwa maswali na Peter Kibatala ambaye ni wakili wa Kubenea wakati akitoa utetezi wake huku hakimu wa kesi hiyo kwenye Mahakama ya Mkazi Kisutu Thomas Simba akimtaka kupaniki.

Kesi hiyo ambayo Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ndiye mlalamikaji, ilifunguliwa tarehe 15 Desemba mwaka jana baada ya viongozi hao wawili kugombana kwenye Kiwanda cha nguo cha TOOKU kilichopo Ubungo, jijini Dar es Salaam tarehe 14 Desemba mwaka jana.

Wakili Kibatala alimuuliza Mujumba kama ni yeye ndiye aliyekutana na baadhi askari polisi kwenye eneo la tukio na je alikuwa anawafahamu na pia walikuwa chini ya nani? Mujumba alijibu kuwa, aliwakuta askari hao eneo la tukio na kumuongeza kwamba, hakujua walikuwa chini ya nani.

Kibatala: Wewe ndio mwenye wajibu wa kuchunguza kesi hiyo je wewe ndio Mkuu wa Mkuu wa Idara hiyo?

Pia aliuliza kwamba siku hiyo kulikuwepo na waandishi lakini alipataje picha za video na sauti kutoka kwa waandishi wa habari?

Mujumba: Ni kweli kulikuwepo na waandishi na kwamba niliwasiliana na waandishi hao ili wanipe ushahidi wa picha, sauti au video. Waandishi walinijibu kuwa hawana ushahidi huo.

Kibatala: je ulikwenda na askari wangapi?

Mujumba: nilikwenda na askari wanane au tisa.

Kibatala: wataje majina

Mujumba: Ni Sajenti Peter, PC Hamis, Joachim na Doel.

Kibatala: Shahidi hajui askari wake kwani anajua jina moja tu la mwanzo na hajataja wote.

Maswali haya yalisababisha Mjumba kukunja sura na kutoa sauti ya juu huku akitaka kubishana, Hakimu Simba alimwambia “acha kupaniki” na kumtaka aache kubishana na wakili.

Hakimu Simba pia alimwambia Mujumba kwamba hana uwezo wa kubishana na wakili huyo na kuwa, anachotakiwa ni kujieleza kwa kujiamini.

Wakili Kibatala kwa kutumia sheria Namba 155(a) aliiomba mahakama kuonesha picha za ushahidi zilizokuwa zianonesha hali halisi ya tukio.

Wakili huyo aliinesha mahakama picha ambazo zilionesha kuwepo kwa askari walioshika bunduki na kumzingira Kubena, kwenye picha hiyo Mujumba hakuwemo.

Hapo awali Mujumba aliieleza mahakama kwamba yeye ndiye aliyemsihi Kubenea aende naye kwenye Kituo cha Polisi Magomeni, hivyo Wakili Kibatala aliongeza kuwa, kwa kutokuwepo kwenye picha ile Mujumba alitoa maelezo ya uongo. Hakimu Mkazi hata hivyo, baada ya shahidi huyo kutoa ushahidi wake, Hakimu Simba alihairisha kesi hiyo hadi tarehe 15 na 16 Aprili mwaka huu.
 
Wataalamu wa body language na psychology watuambie hapa ni nini kiliendelea................
===============================
========================
CdFpZu3WwAA2XtZ.jpg

Mbona hizo picha ni za kuunga?
 
JANA KATIKA MFULULIZO WA KESI YA MBUNGE WA UBUNGO KUBENEA VS MAKONDA; KATIKA UTETEZI WAKE KUBENEA ! SIJASEMA MAKONDA ‘’MJINGA ,MPUMBAVU,KIBAKA NA CHEO CHENYEWE CHA KUPEWA’’ HAKIMU.
ILA NILISEMA MAKONDA NI MTEULE WA RAISI NA MIMI NIMECHAGULIWA NA WANANCHI

IWAPO KUBENEA ATAKUTWA NA HATIA KUNA
1.KUPOTEZA UBUNGE KAMA ILIVYOKUWA KWA MAREHEMU FARES KABUYE MBUNGE WA BIHARAMULO VS CHOYA

2.KULIPA GHARAMA ZA KESI NA FIDIA JUU.

3. UCHAGUZI KUTANGWAZA UPYA JIMBO LA UBUNGO/

Ndugu

Hebu siku nyingine jifunze kuandika kwa herufi ndogo.

Makala ya herufi kubwa inaboa sana kusoma, hata mail huwa tunaandika kwa herufi ndogo.

Sisi wengine tukiona mtu anatumia herufi kubwa tunajua huyo alikimbia umande, hata thread yako hatusomi

Asante
 
Back
Top Bottom