Kubenea... Sali sala yako ya mwisho!

Kwa hali ya vuguvugu iliyopo sasa si jambo la kushangaza kuona napigwa bit na watu asiowafahamu.

Unajua mafisadi walijua wataendelea kusumbua akili za watz milele sasa naona yamewatokea puani wanaanza kuwaya waya.

Ivi hawajui kwa vitisho kama ivyo ndo inawafanya waonekane hopeless zaidi na kuanikwa hazarani?

I call upon the gvt kuprovide uyu ndugu yetu na kaulizi,ivi polisi kazi yao si ni kulinda usalama wa Raia,sasa kama mtu anapigwa bit huoni kuwa anastaili kulindwa.

Pm kama ulimuacknowledge kubenea bungeni wakati umeteuliwa kumridhi Lowasa twaomba umuassist kwa ilo.
 
Ni hatari,Mwema mtu huyu akiuwawa ni juu ya jeshi la polisi kutuambia nani kahusika,maana taarifa zinatolewa wazi na wanasikia na sijui wanachukua hatua gani kwa hili. Maana alitoa taarifa nyingi tu za kufanyiwa vituko,mpaka akamwagiwa tindikali polisi wapo tu. Plosi naona wanasubiri auwawe ndiyo waanze kuwatafuta wahusika. Kubenea wataja hapa unaowahisi wanahusika moja kwa moja na kukuwinda
 
mimi hii nchi naishangaa sana, mna habari hadi sasa kuwa kamanda wa Tibaigana anajiandaa kustaafu mwezi wa sita?
huyu mzee anajua madhambi anayofanya yeye na wenzake kina mwema hao hapo polisi, huwezi kuwakamata wale walinzi eti ndio waliomwaga tindikali kwa hao kina kubenea huo ni uongo mkubwa!

kuna tapeli mkubwa anatafutwa na polisi muda mrefu sasa lakini alikuwepo katika harambee ya mkoa wa kagera kuchangia shule za sekondari alipoonekana simu zikapigwa na polisi wasiojua wakajiandaa kumkata ukumbini cha ajabu Lowassa akazuia hilo alipotakiwa kukamatwa huyo bwana huu sio wizi pia?

mwema ni ahsante Lowassa hawezi kumlinda Kubenea kamwe!
Hosea vile vile!
mwanyika vile vile!

mambo mazito hatuna wa kututoa hapa tulipo tupige mayowe kote dunia ijue labda lakini sio polisi ya Tanzania.
 
Heshima Mbele

Naamini sasa ni wakatio muafaka wa ile sheria ya kuandikisha namba zote za simu ianze kutumika ili kuepusha mambo kama haya.

Nampa Pole ndugu yangu Kubenea.Mungu atakuongoza katikanjia ya haki kwa ueleza ukweli kuhusu unalolijua na kutuambia ukweli yale usiyoyajua bali unayoyahisi yanaweaz kuwa kweli.
 
Ningekuwa mimi ni POLISI,ningeangalia hili jambo kwa jicho la pili.Yani Ninge-suspect maadui zaidi kuliko tunaowahisi.Kwa mtazamo wangu,mimi nahisi kuwa kubenea ana maadui wengi.Sasa kuna mmoja sasa anajifanya ni rafiki yake au ni adui wa chini chini.Baada ya kubenea kupatwa na dhahama ile ya mwanzo sasa yeye huyo adui wa siri anataka kutumia hiyo nafasi ili jamii iseme kuwa labda aliyepiga hiyo simu ya vitisho ni huyu adui tunae mfikiria.

Tutake tusitake,huyo mpiga simu lazima anapitia hapa JF kusoma news.Huyo wa mwanzo aliyemwagia tindikali nae nahisi anapitia hapa JF kusoma news na ktk hali ya Ujambazi wa kawaida LAZIMA anaogopa ama anahisi kuwa jamii tayari inamjua,so hawezi tena kuendelea kupiga simu za vitiso.

Ila kama ni jambazi aliyekubuhu basi huyo mmwaga tindikali ndo mpiga simu,kitu ambacho sitarajii sana kwa ujasiri wa waTZ.Namshauri kubenea kukaa chini na kuanza kuorodhesha ANAO WAHISI NI MAADUI ama wana TOFAUTI zozote.Namba moja awe ni yule anaemhisi kwa asilimia ndogo zaidi na wa mwisho Awe adui wake wa wazi ambae kila mtu anamjua na ambae obvious hawezi kumpigia simu ya vitisho.

Tatizo la Polisi wetu wa bongo ni blah blah nyingi.Yani utafikiri walinzi wa sungusungu vile.Wao kukurupuka tu.Ukitaka kuamini wewe fuatilia wanavyomhoji mtu kukiwa na tukio serious.
Yani wako shallow kweli.

© Ningesema siwapendi ilaisemi tena

Hiyo ndiyo hasara ya kutotoa kipaumbele ktk masuala ya usalama, hao polisi ni form four au six failures. Wanaofanya vizuri darasani hawaajiriwi polisi. Hili ni tatizo la kimfumo. Nchi zingine km vile US, UK wale New scotland yard ni wale walikuwa vichwa darasani. Lazima Serikali ibadili mfumo huu, ili kuwashawishi watu wenye upeo mkubwa kujiunga polisi.
 
Niliwahi kuanguka somo zito na mnenene mmoja mambo ya ndani ni Commissioner wa Polisi alikuwa ni mtupu hadi anaongea kisukuma mie nikanawa na kuondoka.Uelewa wao ni mdogo sana sijui vipi hawa watu .
 
This thing requires a more serious tone; unajua MKJJ aliwahi kuja na habari za namna hii kumhusu Amina Chifupa (RIP), habairi zile zilianza kwa mtindo huu, kazuiwa kuongea, kafungiwa, katishwa,..halafu mwisho wa yote yakatokea yaliyotokea. Sasa mimi naogopa, kama hili limetokea kwa huyu bwana inabidi tuwe wakali zaidi. Hatutaki tena tujikute kwenye bystander effect!
 
yaani nyie ndiyo leo mnagundua kuwa hatuna jeshi la polisi mbona hii inaeleweka tangu zamani maana hata wengi wa hao mapolisi vyeo hupewa kama asante.kwani mmesahau yale ya MAHITA alipopewa cheo baada ya kumthibiti mrema?ni wakati sasa umefika kuwapa sungu sungu wetu mbinu ili watulindie nchi maana twajua sisi ni wakiwa hatuna baba wala mama ila tutaendelea kupiga kelele mpaka mungu atakapotusikia
 
Niliwahi kuanguka somo zito na mnenene mmoja mambo ya ndani ni Commissioner wa Polisi alikuwa ni mtupu hadi anaongea kisukuma mie nikanawa na kuondoka.Uelewa wao ni mdogo sana sijui vipi hawa watu .

Yaani mhalifu akaachiwa kwa jina na nguvu za Lowasa ? Sasa wataendelea kumtafuta ? Unaweza kutaja jina la Jamaa na jamii imjue maana kama anatafutwa na kukamatwa Lowasa akaingilia basi jina lake si siri tena .Hebu mwaga jina tafadhali .
 
I call upon the gvt kuprovide uyu ndugu yetu na kaulizi,ivi polisi kazi yao si ni kulinda usalama wa Raia,sasa kama mtu anapigwa bit huoni kuwa anastaili kulindwa.

Polisi wa bongo wanaamini kazi yao ya kwanza ni kuwalinda watawala kwa mema na mabaya wanayofanya katika nafasi zao. Kulinda usalama wa walalahoi ni jukumu la daraja la pili.
 
Polisi wanaweza ku trace kirahisi sana mtu aliyempigia simu Kubenea kama wakiamua. Makampuni yote ya simu yana rekodi kila simu inayopigwa na kupokelewa.

Hata kama mtu akiweka "private" kwenye simu yake, bado ukienda kwa kampuni ya mtandao anaotumia Kubenea wanaweza ku - print namba za simu zote alizopigiwa na wakajua ni namba ipi ilimpigia muda huo. Hata kama aliyepiga simu alitupa "chip" ya yenye namba hiyo mara tu baada ya kupiga simu, bado anaweza kukamatwa. Kinachoweza kumfanya asikamatwe ni kutupa vyote, handset na chip. Endapo ataweka "chip" nyingine kwenye "handset" ile ile bado anaweza kuwa traced na kukamatwa.
 
Nakubaliana nawe Masaki na sasa Elimu hii kwa Polisi na mwema mwenyewe amewahi kufanya hapa Nairobi kwenye Interpol yote haya anayajua so is matter of willing and deciding to act .
 
Bila shaka safari kuelekea kwenye udikteta tumeshaianza. Bila shaka haya ni matokeo ya baadhi ya vyombo vya habari kukataa kununuliwa na mahakama kukataa kuwa kiota cha kuwasafishia MAFISADI. Hivyo kuwaacha MAFISADI na chaguo moja tu, kuendelea kuanikwa au kuwanyamazisha wale wanaowakemea. La muhimu hapa ni kwa MAFISADI kufahamu kuwa hakuna mahali kwenye historia panapoonyesha ushindi dhidi ya MAFISADI. Watajitahidi kwa muda lakini time ikifika watasalimu amri.
 
Jamani ingawa tuna kila ya sababu ya kupandwa na mzuka kuhusu hili lakini nadhani mambo kama haya ni lazima yatokee. Ukweli ni kuwa pale tu unapoamua kusimamia misingi fulani ni lazima uwe pia tayari kukumbana na misukosuko kama hii anayokumbana nayo Kubenea. Fisadi yeyote yule awe sumaye ama lowassa na zaidi mjanjamjanja kama rostam hawezi akakaa tu pembeni akiangalia ufisadi wake unaanikwa wazi na hata kuwafikisha mahala pagumu kama walivyofikishwa vinara hawa. Ni lazima achukuwe hatua za ama kuondokana ama kupunguza spidi za udhia huo.

Lakini wakati tunawatolea macho mafisadi maarufu hawa ni lazima tuwe makini kutotoa nafasi kwa mafisadi wa chinichini ambao ama ufisadi wao unakuwa hatarini kutokana na kuanguka kwa mafisadi maarufu ama kuunguka kwa kwa mafisadi maaruf hawa kutaweza kutoa mwanya kwao kufanya ufisadi kimahiri zaidi. Yaani hapa ninatoa angalizo kuwa inawezekana kundi jingine la mafisadi wakawa wanafanya haya ili kutoa picha kuwa ni kazi ya mafisadi maarufu ili wao waweze kutekeleza mipango yao Na hapa wanakuja mafisadi makini wa enzi za Ben ambao kuanguka kwao kimikakati kulitokana na kuanikwa kwa ofisadi wao kulikofanikishwa na mafisadi hovyohovyo wa enzi hizi za mtandao.

Yote yawezekana lakini ujumbe wangu kwa Kubenea ni kuwa wakati unafaidi umaarufu kutokana na msimamo wako thabiti kuhusu mafisadi ni lazima uwe tayari kuumia na madhila yanayoandamana na umaarufu huo....

Otherwise wanamapinduzi wa kale walisema...

ALUTA KONTINUA..........
 
Nampa pole Bw. Kubenea, Muhimu ni kwa vyombo vya usalama kutafuta namna ya kumlinda na kuweka mtego wa kuwakamata hawa jamaa. Ni wazi kwamba wanatumwa kufanya hivyo na Mafisadi.

Kwa TZ yetu kutrace namba ya simu ni ngumu sana, maana Laini za simu zinauzwa kama karanga. mtu ananunua laini anakutishia akimaliza anaitupa.

Nakubaliana na wewe kuwa kutrace namba za simu kama mtu akitupa si rahisi kabisa, ila kama haitupi anatumia na kujifanya private, ni rahisi sana kufuatilia from cellur operator! Police wanaweza pata namba zote zilizo pigwa kwa namba fulani at any time 't'.

Pole sana bwana kubenea, ila hao hawajui kuwa wanakujengea umaarufu, usife moyo ndugu yetu!
 
Polisi wanaweza ku trace kirahisi sana mtu aliyempigia simu Kubenea kama wakiamua. Makampuni yote ya simu yana rekodi kila simu inayopigwa na kupokelewa.

Hata kama mtu akiweka "private" kwenye simu yake, bado ukienda kwa kampuni ya mtandao anaotumia Kubenea wanaweza ku - print namba za simu zote alizopigiwa na wakajua ni namba ipi ilimpigia muda huo. Hata kama aliyepiga simu alitupa "chip" ya yenye namba hiyo mara tu baada ya kupiga simu, bado anaweza kukamatwa. Kinachoweza kumfanya asikamatwe ni kutupa vyote, handset na chip. Endapo ataweka "chip" nyingine kwenye "handset" ile ile bado anaweza kuwa traced na kukamatwa.

Thanks Masaki,

Je akina Mwema na Manumbu wanalijua hili?
 
Ninachoogopa ni haya mambo ya kuhisi tunaishi kwenye Police State.. inanikumbusha maisha chini ya Hastings Kamuzu Banda... Hivi huku ndiko tunakoelekea?
 
Ninachoogopa ni haya mambo ya kuhisi tunaishi kwenye Police State.. inanikumbusha maisha chini ya Hastings Kamuzu Banda... Hivi huku ndiko tunakoelekea?

Haya mambo pia alijaribu kuyagusia Mkuchika pale alivyoongea na vyombo vya habari na kutishia kuwa serikali itarudi kule kwa Mkapa kwa kujaribu kudhibiti uhuru wa vyombo vya habari.

Kama wananchi hawajisikii huru katika nchi yao wenyewe basi serikali kuu inabidi iwajibishwe kwa hilo. Haiwezekani siku moja tu baada ya Kubenea kuleta story ya Deep Green ndio aanze kupata vitisho hivi.

Hii Deep Green mbona inalindwa hivi? Mbona Kikwete amekuwa kimya kabisa katika suala hili? lazima kuna kitu hapa na ndio maana namuuliza PM Pinda ahakikishe ulinzi wa maisha ya Kubenea maana kuna mambo yako karibu kutoka hapa na watanzania watajua tu ni nini serikali yao inafanya kwa niaba yao.
 
Hii haikubaliki kabisa kwa nchi ya amani kama Tanzania, tunamkumbuka Katabalo ambaye alifichua ufisadi ngorongoro na yaliyomtokea ilikuwa kama ajali hakuna aliyejali. Hivi sasa ndugu na rafiki yetu Kubenea ambaye amejitoa mhanga kufichua njama za kifisadi zinazoitafuna nchi yetu anaambulia vitisho halafu DOLa ipo kimya. Je tuelewe kwamba Serikali isubiri kumpa pole tena atakapokuwa ICU? au itawapa pole familia yake pale ambapo watishiaji watakapotimiza azma yao??? Hii haikubaliki, Hii inaonesha kuwa mapambano ya kifisadi ambayo serikali inaonesha inachukua hatua ni mchezo wa kisanii usiokuwa na dira yeyote zaidi ya kufunika kombe wanaharamu tupite.

Vitisho hivi siyo vya kupuuza hata kidogo na kwa kuwa serikali imeamua kutompatia ulinzi basi natoa rai kwa wanabodi wenye kuyafahamu haya mambo kumpa sapoti ndugu yetu huyu maana mafisadi hawalali. Tusiishie kulaani tu bali hata hatua tuzichukue ili kupunguza kama si kukomesha matukio haya. Niliwaambia hapo awali kuwa kile kifo cha dereva wa waziri siyo bure na sasa mnajionea jinsi ambavyo polisi walihusika kumtoa uhai wake, je hii ya Kubenea ina maana hata usalama wanahusika???????? Hatutaki kuamini hivyo ila tunalazimishwa kuamini hivyo kwa kuwa vyombo vya usalama havichukui uzito unaostahili dhidi ya vitisho hivi.

Nampa Pole Kubenea na serikali ifahamu kuwa lolote litakalomtokea basi isikwepe lawama ya kuhusika.
 
nimecheka sana na baadhi ya wachangiaji wa hoja kwenye hii mada hadi wengine wakitaka **viongozi wa serikali** wamlinde **mwandishi wa habari** wakati hao viongozi wenyewe wanalindwa na **jeshi la polisi** sasa najua hapa JF wengine ni wenye uelewa mkubwa, inakuwaje kiongozi anayelindwa alinde mwandishi wa habari ? got damn it, jamani fikirieni saa nyingine na sio kutamka tu ili mradi mmeongea, mnaweza kuwa na idea nzuri na kushindwa kuipresent, sasa hao viongozi wakishindwa kumlinda, mtawalaumu hao viongozi ? ni sawa sawa mgonjwa wa ngoma unaenda kupata ushauri nasaha kwa dentist !

fikirieni tena kidogo kwa hapo !

hey, by the way huyu kubenea ni mzima hadi sasa hivi au ? maana naona kimyaaaaaaaaaaa !!
 
Back
Top Bottom