Kubenea niliyemfahamu mimi. Je, atasahau alikotoka?

Wabongo bhana. Wanapenda sana kuishi maisha mawili. Ya kwake na anavyotaka watu wengine waishi kutokana na mtazamo wake.
 
Daaah Said Kubenea katika ubora wake na gazeti la Mwanahalisi, ama kweli maisha yanaenda kasi sana..@Kesho ni nzuri kuliko jana
 
Mkuu
Kumekucha tena tuendelee
Kama inavyofahamika wazi kuwa EL alikuwa na kiu kubwa ya kuwa rais wa Jamhuri na kwa vyovyote waliunda umoja yeye na JK way back 1995 ili mmojawao awe akiwa raisi basi mwingine awe makamu ama Waziri mkuu.. Aliyetibua hii mission alikuwa hayati Mwalimu Nyerere.. Lakini tukirudi nyuma zaidi miaka ile ya 80 mwishoni kipindi cha mzee Mwinyi wakati huo Mzee Malecela akiwa na nguvu kubwa pia naye alishaonesha nia ya dhati ya kuutaka urais... Kama kwa EL tu aliyetibua mipango yote alikuwa Mwalimu Nyerere mchonga meno.

Malecela alikuwa kajijenga mno ndani ya ccm kuanzia chini mpaka juu.. Wajumbe wote wa mikoani na wilayani walikuwa team yake.. Tunatambua dhima ya wakuu wa wilaya na mikoa.. Hawa ndio wasimamizi wa kamati za ulinzi na usalama.. Na ripoti zote za kila siku walikuwa wanaziwasilisha kwa Waziri mkuu... Malecela pia alishawahi kuwa Waziri mkuu
Mbinu za Malecela ndio zilikuja kuwa mbinu za EL.. Ni kama alikopi na kupest na kumbuka Malecela alishawahi kuwa boss wake..... Nia ya dhati ya Kukaa magogoni haikuwahi kuwatoka vijana wawili machachari almaarufu kama BOYS II MEN.. Jakaya na Lowassa.. Waliendelea kujiwekeza na hatimaye 2005 JK akawa rais na kumteua Lowassa rafiki wa siku nyingi kuwa Waziri mkuu.

Mambo yalikuwa ok mwanzoni lakini uchapakazi wake ulianza kuwatia shaka wengi. Alikuwa na kila elements za hayati Edward Moringe Sokoine wajina wake.. Hili liliwatisha wengi... Taratibu waziri mkuu akawa maarufu kuliko boss wake
Mpango wa wananchi uliovumbuliwa na Waziri mkuu EL wa kuchangia elimu kwa hiari ulikuwa na matokeo chanya ya kutisha.

Ndipo hapa JK akatonywa kuwa ukimuachia huyu 2010 hutoboi atakutoa.. Hii pesa ya UJENZI wa madarasa na kuchangia elimu account zake zilikuwa chini ya PM.. Kwahiyo alikuwa na madaraka nazo kwa asilimia mia.. Ikaonekana wazi anaweza kutumia mwanya huo kujikita zaidi na kukusanya pesa kwa ajili ya uchaguzi 2010

Ni hapa sasa watu kama SK walihitajika kwa nguvu mno.. Hasa kwenye propaganda na kujiwekeza kwenye kukubalika na kuwabana wengine... EL angekuwa na uchaguzi wa watu wengine wenye UTHUBUTU.

Kulikuwa na Mchungaji Mtikila RIP wa Liberty desk lakini huyu alikuwa keshaharibu na akawa hatabiriki wala kuaminika na tayari akawa na chama cha SIASA.

Kulikuwa na Mrema lakini naye alikuwa na nia kama ya EL na tayari alikuwa keshamalizwa na kitengo alipokimbilia NCCR-MAGEUZI.

Kulikuwa na waandishi na wanasiasa wengi lakini akachagua the most potential one.. Na hapa SL akalamba dume.

Kama tunakumbuka Mwanahalisi liliripoti ishu ya Richmond kwa namna ya kumkinga EL
Habari ni ndefu lakini SK aliendelea kuwa bega kwa bega na EL na baadae wakafanikiwa kujipenyeza CHADEMA kupitia Dr. Slaa.. CHADEMA ikawa juu lakini nyuma yake kulikuwa na mkono wa EL hasa kwenye connection na kitengo

Mambo yalipoharibika kabisa CCM EL alikimbilia CHADEMA ili akatimize ndoto yake.. Lakini ujio wake haukumfurahisha hata kidogo Dr. Slaa kwakuwa kama EL angefanikiwa kuwa rais thamani ya Dr Slaa ingeshuka sana kwakuwa connection yake sasa ina connect yenyewe... Yaliyofuatia yote yanajulikana.


SK amekuwa kiungo muhimu sana kwenye siasa za upinzani hasa CHADEMA na EL na Slaa.. Amefaidika pia.. Ametengeneza na kujenga jina lake ana mchango wake mkubwa tu.. Ndio maana nikahoji kama anaweza kuvaa uso wa mbuzi na kumuua nyani... Bahati nzuri amekuwa na tafakuri kuu

Jr

Jr
Mkuu hapo nilipo bold, umeandika mambo mazito,

Kwamba kabla ya kuhamia huko ufipa EL ndiye alikuwa koneksheni ya ufipa na kitengo?? Duuh!!
 
Alishaona mambo yanabadilika kwa kasi kubwa na baada ya hapo alitoa kitabu chake alichokiita UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA
Ningependa siku moja nisikie jinsi ulafi wa madaraka ulivyomuondo mwalimu jkn mapema
81KOPCXDZML.jpeg


Jr
 
Aisee wewe ni mwamba. Kweli gari ya kubenea Suzuki samurai ipo kilindoni mafia kubenea alilileta wakati wa GE 20215. Wakati huo alikuwa anataka kugombea mafia. Duh jamaa nilimuamini sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom