VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Kufuatia kutolewa hadharani kwa mikataba ya kuuzwa kwa Fukwe ya Coco, uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili Mhandisi Musa Natty umekwama. Mhandisi Musa Natty alikuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kabla ya kuhamishiwa Mji wa Babati kuwa Mkurugenzi. Alisimamishwa kazi kupisha uchunguzi juu ya tuhuma zinazomkabili.
Kati ya tuhuma hizo ni ujenzi mbovu wa barabara za Manispaa ya Kinondoni pamoja na uuzwaji wa kifisadi wa fukwe za Coco. Baada ya kujitokeza kwa Saed Kubenea (Mbunge wa Ubungo-CHADEMA) na Boniface Jacob (Meya wa Kinondoni na Diwani wa Ubungo-CHADEMA) na kuanika mkataba wa fukwe za Coco, uchunguzi 'umevurugika' na kusimama.
Kubenea na Jacob waliapa kusimama kidete kumtetea asiyehusika na kutaka wahusika halisi waanikwe na kushughulikiwa. Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanaona kuwa Kubenea alianza mivutano na mamlaka na wafuasi wao mbalimbali. Ndiyo maana, Kubenea amekuwa akishambuliwa kimaneno na kubanwa.
Kubenea sasa amekuwa akizungumzwa vya kutosha kufuatia 'kujitoa muhanga' juu ya kashfa za Kinondoni. Uchunguzi unasuasua. Nani anaogopwa? Filamu inaendelea!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam