Kubenea: Kweli kwa ulaji kama huu ni rahisi mtu kuachia ubunge? Yaani kirahisi rahisi tu?

Kwanza TV

Verified Member
May 2, 2017
33
125
Leo mbunge wa Ubungo (CHADEMA) Saed Kubenea alikuwa na mkutano na waandishi wa habari na ameeleza kuwa hana mpango wa kukihama chama chake cha Chadema na kwamba hana bei bali kinachoendelea ni propaganda za CCM ili wasiulizwe maswali magumu.

Katika kujenga hoja, Kubenea ameainisha mapato ya mbunge na amehoji je mtu anaweza kuachia nafasi kama hii kirahisirahisi?

Hebu msikilize:

 

Avaae

Member
Nov 30, 2017
39
125
Kama hoja ndio hiyo atueleze na Nyalandu walimlipa bei gani....kua zwazwa kama Kubenea na Chadema yake inataka moyo
 

Jay One

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
14,098
2,000
Nyalandu pia alinunuliwa aiseeee.. Haiwezekani aache ubunge na mapesa yote hayo aende Chadema, lazima biashara ya kumnunua ya utumwa ilifanyika..!!
 

gnassingbe

JF-Expert Member
Jun 14, 2015
4,836
2,000
Swala la Nyalandu lina uhusiano wa moja kwa moja na Madhila ya Mhe.Lissu wala siamini kama kuna Biashara ya utumwa hapo na isitoshe nahisi anajiamini jimboni anarudi hata kama ni kwa tiketi ya TLP kwa hiyo alienda likizo tu bungeni anarudi!
 

jonas amos

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
2,310
2,000
Ukitoka ccm ukaenda chadema wewe ni mzalendo wa taifa lako Ila ukitoka chadema ukaenda ccm wewe umenunuliwa hahaa hamuwezi kuwa hamjalewa
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
48,101
2,000
Swala la Nyalandu lina uhusiano wa moja kwa moja na Madhila ya Mhe.Lissu wala siamini kama kuna Biashara ya utumwa hapo na isitoshe nahisi anajiamini jimboni anarudi hata kama ni kwa tiketi ya TLP kwa hiyo alienda likizo tu bungeni anarudi!
Chama nuksi hiki, utasikia mgombea wa CCM amepata kura 10,000 na mpinzani wake kura 3,000. Ajabu ni kuwa wapiga kura wote ni 7,000.
 

Annael

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
16,821
2,000
Chadema imekosa direction. Badala ya kuweka sera zao hapa wanatueleza biashara ya siasa wanayopiga. Niliwambia hawa jamaa wanafanya biashara ya siasa. Hawana nia ya musaidia wananchi. 2020. Ondoeni wote hao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom