Kubenea kumwagiwa tindikali: Nini chanzo?

Status
Not open for further replies.

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
Shahidi kesi ya Kubenea: Watuhumiwa waliahidiwa mil. 2/-

na Mwandishi Wetu

SHAHIDI wa kwanza katika kesi ya kuwajeruhi na kuwamwagia tindikali waandishi wawili wa magazeti ya Mwanahalisi na Mseto, amedai watuhumiwa waliahidiwa kulipwa sh milioni mbili na bosi wa Kampuni ya Bakhresa, endapo wangefanikiwa kumzuru Saed Kubenea.

Shahidi huyo, Sajenti David, aliiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana kuwa, maelezo hayo yalitolewa na mshitakiwa, Frednand Mtepa na kuongeza kuwa bosi huyo alidai Kubenea alikuwa akitembea na mke wake.

Alidai baada ya watuhumiwa kuahidiwa fedha hizo, walifanya kikao katika baa ya Mtepa iliyoko Mwananyamala kwa lengo la kufanikisha tukio hilo.

“Mtuhumiwa Frednand kwa ridhaa yake mwenyewe alieleza walifanya kikao Desemba 25 mwaka jana na Januari 5 mwaka huu, kabla ya kutenda kosa walikuwa na wenzao wanne,” alieleza shahidi huyo.

Shahidi huyo aliwataja watuhumiwa wanaodaiwa kuwepo kwenye kikao hicho ni Alex Mwandembele, Hashim Ally, Augustino Joseph na mtuhumiwa mwingine aliyetambuliwa kwa jina moja la Maneno ambaye shahidi alieleza kumtafuta mshitakiwa huyo ili aweze kuunganishwa na wenzake.

Alieleza Mwandembele ndiye aliyekuwa amekabidhiwa fedha hizo ambazo walitakiwa kugawana baada ya kukamilika kwa tukio hilo.

Shahidi huyo alidai tuhuma za kujeruhiwa kwa Kubenea hakuhusiani na masuala ya kisiasa, bali ni kama matukio mengine ya ushambuliaji yanavyoweza kutokea.

Kesi hiyo inaendelea na ushahidi wake leo ambako Kubenea anatarajiwa kutoa ushahidi wake.

Washitakiwa katika kesi hiyo wanadaiwa kutenda kosa hilo Januari 5 mwaka huu, eneo la Kinondoni, Dar es Salaam.

tanzania daima
 
Ha ha ha, Ebwana inawezekana ingawa isije ikawa sababu pandikizi kugeuza mambo na ushindi uende kwa Mafisadi
 
Pole Kubonea, kama ndivyo ilivyo, umma wa watanzania utasikitika kwa hilo, ila kama ni kupindisha kesi Mungu atakusaidia.
 
Labda Kubenea atatuambia je hiyo ni kweli? Na yule mwandishi mwingine alikosa nini?

Kama ni kweli si wangemtaja huyo kigogo wa kwa Bakhresa?
 
sasa jamani watuhumiwa si ndio wenye kueleza sababu ya wao kutekeleza hayo mambo yao?

huyu bwana tufatilieni kama ni kweli alikuwa akikamua mke wa watu na kama ni kweli na yeye ni fisadi tena ni mtu hatari mwenye kuingilia ndoa za watu
 
kwa hiyo unataka kusema kuwa hata Kikwete amwagiwe tindikali kwa kuingilia ndoa za watu (if that is the case here)?
 
Shahidi huyo alidai tuhuma za kujeruhiwa kwa Kubenea hakuhusiani na masuala ya kisiasa, bali ni kama matukio mengine ya ushambuliaji yanavyoweza kutokea

Hiki ndicho waliomshambulia Kubenea wanajaribu kuweka kwenye hii case ili kuwatoa Lowasa na Rostam ambao ndio wanahusika na haya mashambulizi dhidi ya Kubenea kwenye hook.
 
Of all pple wa kusuta awe wewe?

Kubali kuwa umechemsha big time kwa mabandiko yako yate kuhusu hii issue ya Kubenea.

Na kama kawaida yako ukibonyezwa kidogo tu hurukia kwa JK...Vipi wewe! Naona ni wakati wako wa kukimbia hii forum kwa kujitia too much know wakati hujui chochote..
 
Hiki ndicho waliomshambulia Kubenea wanajaribu kuweka kwenye hii case ili kuwatoa Lowasa na Rostam ambao ndio wanahusika na haya mashambulizi dhidi ya Kubenea kwenye hook.

meshimiwa kumbe una majibu yako kwenye mfuko, kwa hio unaamini hili limepangwa na lowassa na wenziwe?

sasa mkweli ni nani kati ya waliofanya au hawa wenye kuhukumu kwa hisia?

ndio maana mnafedheheka na kuomba radhi mchana kweupee kwa kubwabwaja bila ya mashiko
 
Kubali kuwa umechemsha big time kwa mabandiko yako yate kuhusu hii issue ya Kubenea.

Na kama kawaida yako ukibonyezwa kidogo tu hurukia kwa JK...Vipi wewe! Naona ni wakati wako wa kukimbia hii forum kwa kujitia too much know wakati hujui chochote..

Mbona ndio mwanzo nimeanza "kujitia" kwenye hii forum! Get used to it coz I am here to stay!
 
meshimiwa kumbe una majibu yako kwenye mfuko, kwa hio unaamini hili limepangwa na lowassa na wenziwe?

sasa mkweli ni nani kati ya waliofanya au hawa wenye kuhukumu kwa hisia?

ndio maana mnafedheheka na kuomba radhi mchana kweupee kwa kubwabwaja bila ya mashiko

Unaongelea niini hapa... hueleweki!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom