Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,184
- 671
Shahidi kesi ya Kubenea: Watuhumiwa waliahidiwa mil. 2/-
na Mwandishi Wetu
SHAHIDI wa kwanza katika kesi ya kuwajeruhi na kuwamwagia tindikali waandishi wawili wa magazeti ya Mwanahalisi na Mseto, amedai watuhumiwa waliahidiwa kulipwa sh milioni mbili na bosi wa Kampuni ya Bakhresa, endapo wangefanikiwa kumzuru Saed Kubenea.
Shahidi huyo, Sajenti David, aliiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana kuwa, maelezo hayo yalitolewa na mshitakiwa, Frednand Mtepa na kuongeza kuwa bosi huyo alidai Kubenea alikuwa akitembea na mke wake.
Alidai baada ya watuhumiwa kuahidiwa fedha hizo, walifanya kikao katika baa ya Mtepa iliyoko Mwananyamala kwa lengo la kufanikisha tukio hilo.
Mtuhumiwa Frednand kwa ridhaa yake mwenyewe alieleza walifanya kikao Desemba 25 mwaka jana na Januari 5 mwaka huu, kabla ya kutenda kosa walikuwa na wenzao wanne, alieleza shahidi huyo.
Shahidi huyo aliwataja watuhumiwa wanaodaiwa kuwepo kwenye kikao hicho ni Alex Mwandembele, Hashim Ally, Augustino Joseph na mtuhumiwa mwingine aliyetambuliwa kwa jina moja la Maneno ambaye shahidi alieleza kumtafuta mshitakiwa huyo ili aweze kuunganishwa na wenzake.
Alieleza Mwandembele ndiye aliyekuwa amekabidhiwa fedha hizo ambazo walitakiwa kugawana baada ya kukamilika kwa tukio hilo.
Shahidi huyo alidai tuhuma za kujeruhiwa kwa Kubenea hakuhusiani na masuala ya kisiasa, bali ni kama matukio mengine ya ushambuliaji yanavyoweza kutokea.
Kesi hiyo inaendelea na ushahidi wake leo ambako Kubenea anatarajiwa kutoa ushahidi wake.
Washitakiwa katika kesi hiyo wanadaiwa kutenda kosa hilo Januari 5 mwaka huu, eneo la Kinondoni, Dar es Salaam.
tanzania daima