Dar: CHADEMA wazungumza na wanahabari kuhusu mauaji, barua ya Msajili na mahabusu wenye majeraha ya risasi

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
CHADEMA watakuwa na mkutano na Wanahabari kwenye Ofisi za Makao Makuu ya CHADEMA kuanzia saa 7.30 mchana (muda utazingatiwa), ambapo mambo makubwa matatu yatazungumziwa;

1. Mauaji ya kikatili na kutisha ya Diwani wa CHADEMA Kata ya Namala, Mlimba, Morogoro, Mh. Godfrey Luena yaliyotokea jana.

2. Barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa CHADEMA kuhusu kilichotokea Ijumaa, Februari 16, mwaka huu.

3. Mahabusu wenye majeraha ya risasi wanaondelea kushikiliwa mahabusu za polisi.
IMG_20180223_140413.jpg


========


Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya utangazaji wameshaanza kuwasili.
Viongozi wa Chadema wakiongozwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Salim Mwalim wameshafika ukumbini.

| CHADEMA inatoa tamko kuhusu Diwani wao aliyeuwawa kwa kupigwa mapanga na pia kuhusu barua waliopewa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.

==>> John Mnyika: Katika hali ya kawaida tungeweza kutoa tamko la kulaani mauji ya viongozi wetu na wafuasi wa CHADEMA lakini inachoonekana kulaani peke yake haitoshi. Serikali haitilii maanani mauji haya na kwanini yatokee kwa CHADEMA tu?
katika hali hii ya sasa ya kufululiza kuuwawa kwa viongozi wetu wa CHADEMA, inaonekana sisi ndio walengwa. Sasa tunatoa wito kwa wanachama wetu na viongozi wa CHADEMA tuchukue tahadhari sana mana hawa watu wamedhamiria kutumaliza .

==>> John Mnyika :Msajili wa Vyama vya Siasa alitutaka tuandike barua kujibu yaliyotokea kwenye uchaguzi mdogo Kinondoni kwa kile kinachoitwa tumevunja sheria na sisi tumemjibu mengi. Msajili anasukumwa na Rais Magufuli -

==>>John Mnyika : Msajili wa vyama vya siasa anasukumwa , dhamira yao ni kutafuta mwanya wa kukifuta Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jambo hili hawaliwezi na kama wanafikiri wanauwezo wa kuifuta CHADEMA wajaribu kufanya hivyo. Wafahamu kwamba wakizuia mlango wa demokrasia, watu watafanya siasa kwa njia nyingine, sisi tutakabiliana na msajili kwa njia yoyote kuhakikisha jambo hili halifanikiwi"

==>> John Mnyika :unashangazwa na ukimya wa Msajili wa Vyama vya Siasa kwenye haya matukio ya kuuawa kwa wanachama wetu. Yeye ndio mlezi wa vyama hivi, tulitarajia aseme kitu lakini kakaa kimya. Ina maana kwamba haoni?

==>> John Mnyika:Tunawaomba wadau wa Haki za Binadamu wafuatile watu takribani watatu waliopigwa risasi wako mahabusu na wamenyimwa dhamana hali zao ni mbaya na Polisi hawajawapa matibabu. Hivi huu ni ubinadamu? Wanafurahi kuona hawa majeruhi wanaolalamika maumivu.

==>>John Mnyika :Kuhusu kufungua kesi juu ya unyama wanaotufanyia hadi sasa wanatuzungusha. Muda huu mawakili wetu wamekaa mahakamani kuhakikisha kesi hii inafunguliwa leo na tunajua huu ni mchezo tu wanatuchezea.

==>> John Mnyika:Mashirika ya Kimataifa yanapaswa kufahamu kuwa Tanzania hivi sasa kuna mauaji ya kisiasa na tunawaambia watanzania hivi sasa hali ilipofikia msikubali kuwafungulia mlango usiku wa manane watu hata kama wanajitambulisha ni askari

Habari zaidi...

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimejibu barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi inayowataka ndani ya siku tano kuwasilisha maelezo ya tuhuma za uvunjifu wa Sheria ya Vyama vya Siasa na ya maadili ya vyama vya siasa kwa kufanya maandamano Februari 16, 2018.

Katika majibu yake, Chadema wamejibu hoja mbalimbali za msajili na kuhoji hatua alizochukua mpaka sasa kufuatia mfululizo wa matukio ya mauaji ya viongozi wa chama hicho.

Akizungumza leo Februari 23, 2018 na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho-Bara, John Mnyika amesema msajili kwenye barua yake anakituhumu Chadema kwa kukiuka kifungu cha 9(2) cha Sheria ya Vyama vya Siasa.

Mnyika amefafanua kwamba kifungu hicho hakihusu vyama vyenye usajili wa kudumu bali vyama vya siasa vyenye usajili wa muda mfupi ambavyo vinaahidi kwamba vikipata usajili wa kudumu vitadumisha amani katika shughuli zao.

Mnyika amekosoa pia barua ya msajili ambaye anahoji ushiriki wa Chadema kwenye uchaguzi wa ubunge katika jimbo la Ubungo wakati uchaguzi huo ulifanyika katika jimbo la Kinondoni, kuongeza kuwa hiyo inaonyesha kwamba msajili amekosa umakini katika majukumu yake.

"Tunaelewa kwamba msajili anasukumwa na Serikali. Dhamira yao ni kukifuta Chadema. Nawaambia tu jambo hilo hawaliwezi," amesema.

Mnyika ambaye pia ni mbunge wa Kibamba amesema msajili amebainisha kwenye barua yake kwamba wamekiuka kanuni ya 6(1)(b) ya maadili ya vyama vya siasa ambayo inampa mamlaka ya kupokea malalamiko na kuzisikiliza pande mbili.

Akijibu jambo hilo Mnyika amesema msajili hajabainisha mlalamikaji ni nani katika malalamiko aliyoyapokea.

Chama hicho pia kimelaani mauaji ya diwani wake Kata ya Namala, Godfrey Luena na kutaka Polisi kufanya uchunguzi wa haraka na kumchukulia hatua za kisheria kila anayehusika.

"Katika Taifa letu kwa sasa, kuna vikundi vya watekaji, vikundi vya wauaji na vikundi vya watesaji. Ni wakati wa kujilinda kwa sababu kuna mashambulizi mengi sana," amesema Mnyika.
 
Hawa hawajiulizi kuwa
Walidai mtu amenunuliwa hadi akajiuzuru
Sasa tujiulize kwamba
Kama kweli kanunuliwa halaf ameteuliwa agombee hapo hapo alipopaachia je mnunuzi atakubali pesa yake aliyotoa kwa kumnunua huyo mgombeaji ipotee???
Wakilipata hilo jibu naimani hawatapoteza hata muda wao wakulia lia hovyo kwenye Medias
 
Sawa tunasubiri utupe mrejesho ila chonde chonde yasije yakatokea maafa mengine huko bado tuna misiba mingi sana mioyoni mwetu! Kama wakija wakawaambia muondoke au tawanyikeni msibishane nao!
 
Magufuli ameipeleka nchi kubaya. Kila uchao mtu lazima auawe au kupotea asijulikane aliko. Hofu imetanda hapa nchini. Mbinu za Kagame zimeanza kufanikiwa huku watanzania tukichekelea.
 
Kuua mnauwana wenyewe.....Mimi kwa upande wangu SERIKALI IWACHUNGUZE SANA HAWA VIONGOZI WA CHADEMA this GUYS ni mafia....

Kinachofanyika sasa ni wao kuwadhuru viongozi wao wenyewe kwa lengo la kutengeneza picha ya kuihusisha serikali na CCM kwenye huu uchafu wao na kufanikisha lengo lao kuu la kuichafua TANZANIA kimataifa

Maana hii ndio option kubwa walio baki nayo kupambana na MAGUFULI....
Mauaji ya namna hii tutaendelea sana kuyasikia kwenye utwala huu wa AWAMU ya tano....

Nani ndani ya NCHI hii anaweza kukataa ya kuwa MAGUFULI kawashika vibaya hawa WAPINZANI???.....sasa haya mauaji ni njia mbadala ya kupamban na MAGUFULI ...MKUBALI MKATAE HUU NDIO UKWELI......

Na mtambue kabsa huyu Mkiti wenu hii njia ndio kinga na salama yake ya kuendelea kuwa M/kiti wa maisha hapo chamani......

SERIKALI CHUNGUZENI MBOWE,LEMA NA MREMA ipasavyo hawa watu wanachafua AMANI ya nchi yetu.......

Mfano mdogo tu hivi kweli ingekuwa si wao waliohusika na UPOTEVU wa BEN SAANANE kweli wangekuwa kimya namna hii???ACHENI MASIHARA...kuna mchezo unachezwa na hawa watu....

Kiashiria kingne ni JAMAA NI MUOGA KWELI KUITIKIA WITO WA POLISI(NA hizi huwa ni sifa kuu za watenda maovu).....akisikiaga wito ndio safari ndio zinatokea...rejea ISHU YA MADAWA YA KULEVYA na wito wa juzi wa maandamano......na mengne mengi
They are playing this very smart.........
 
Back
Top Bottom