Kubenea awaonya wanaopiga ramli kuhusu hatima yake CHADEMA, azungumzia Virusi vya Corona

Kubenea Ndani ya chadema umekuwa kama punching bag, kila kiongozi anakutukana na mtandaoni wame mobilize vijana kukutukana

Hawa Chadema ni watu wasio na shukran wala heshima

Chadema walikutumia Wewe kuanika ajenda zao sasa wanakutukana

Kupitia gazeti la mwanahalisi ambalo lilikuwa linaongozwa kwa kusomwa Nchini uliripoti kila hotuba za Chadema

Kila tukio la Chadema uliliandika leo hii wanakuona taka taka hii ni kweli jamani? Mimi nakasirika sana

Kupitia hoja za Chadema uliingia matatizoni na mafisadi ukamwagiwa tindikali almanusura uwe kipofu serkali ikakutibia

Bado kupitia hoja za Chadema, gazeti lako lilifungiwa hadi ukaingia kwenye madeni makubwa

Hawa ambao wakutukana leo hasa mitandaoni tukiwafatilia 2007 walikuwa hawaijui hata Chadema, walikuwa hata hawajui mwenye Chadema ni nani?

ati leo Ndio wanakuona Wewe mbaya kwa lipi?

Nikiikumbuka Chadema ya dr slaa ilyoheshimika nikiifananisha na hii ya kina mdee nagundua Chadema ina dhambi nyingi inatakiwa itubu kwa dr. Slaa

Kubenea waachie chama acha kutishwa na watu wasio jitambua

Ondoka Chadema Achana na vyama vya watu

Akufukuzay...

Kube anaondoka chadema ni swala la muda tu na hatogombea ubunge ubungo, anarudi kwao Maswa


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Wana JF kweli jana hatukuona cha ku comment leo kutoka katika ile press conference ya jana pamoja kujiandaa kote mbunge wetu wa Ubungo? Mbunge kaongelea vitu vingi ikiwemo kuchukua tahadhari juu ya CORONA Virus- Coved -19 na kapendekeza mikakati kibao.
Kama hatuna wivu juu yake basi tunamuwazia mabaya.
 
Hiyo ni dalili kapuuzwa, ni bora angechagua upande na sio kusimamisha shilingi.
 
Wana JF kweli jana hatukuona cha ku comment leo kutoka katika ile press conference ya jana pamoja kujiandaa kote mbunge wetu wa Ubungo? Mbunge kaongelea vitu vingi ikiwemo kuchukua tahadhari juu ya CORONA Virus- Coved -19 na kapendekeza mikakati kibao.
Kama hatuna wivu juu yake basi tunamuwazia mabaya.
Alichozungumza kwenye press conference na matarajio ya watu juu ya nini kingezungumzwa vimekinzana that's why hakuna comment
 
Kwanini mnamnyanyasa Kubenea? Hayo Ndio malipo yake kwa wema aliokutendeeni?
leo amekuwa mwema? ulisahau kwamba alimwagiwa sumu na kukatwa mapanga na ccm?
mangula kanyweshwa sumu na nani? tuseme ni mwenyekiti wenu? kwanini?
 
"Nataka wananchi wenzangu wa Ubungo na Dar es Salaam pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na viongozi zinapaswa kuungwa mkono na jamii ili wananchi wajue madhara ya ugonjwa huu wa Corona tufuate ushauri wa wataalam.View attachment 1406562

Kuna hatari za kiafya kutoka nchi tajiri duniani juu ya gonjwa hili la Corona sembuse sisi?, Mungu atunusuru na haya mambo ya kufanya mzaha.

Nimshukuru Spika Ndugai kwa kupunguza idadi ya wabunge Bungeni ametumia mamlaka yake kwa mujibu wa Katiba kulinda afya za wabunge lakini haitoshi, ni vizuri bunge likafungwa kama maambukizi yataendelea, kuokoa maisha ya watu.

Mapato ya serikali yanategemea kodi na mapato makubwa ni ya utalii, tutegemee uwepo wa mdororo wa uchumi duniani kwa sababu ya gonjwa hili.

Huu sio wakati wa kurushiana vijembe na kuonyeshana ubabe, hii vita vi yetu sote, wakati wa vita ya Kagera, Taifa lilikuwa pamoja na huu ugonjwa ni lazima tushikamane pamoja kuhamasisha jamii inaelimika na Serikali isaidie.

Inawezekana taarifa zinazotolewa sasa sio za kweli kwa sababu kuna shida pia ya utambuzi ambayo ni jambo serious kabisa, serikali iwekeze katika maeneo ya kuhudumia wagonjwa.

Ni jambo jema shule zilivyofungwa kwa sababu mzazi unakuwa karibu na mwanao lakini kwa misongamano iliyopo kwenye madaladala unaona bora huyo mtoto angebaki shuleni.

Baada ya Anthony Komu kutangaza kuondoka Chadema yamekuwepo maneno mengi nikitajwa na mimi nitamfuata Komu, Komu ni ndugu yangu kabisa, lakini urafiki wangu na Komu haunifanyi kila anachofanya nami nifanye, mimi bado mbunge wa Chadema.

Mimi nimeshaenda mahakamani mara nyingi sana, lakini inategemea na nafasi yangu na mimi naamini sio lazima watu wote kukusanyika katika tukio moja, mimi nashiriki kwenye shughuli za Chadema, sina shida na chama na nipo pamoja na viongozi wangu," Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo
Ukiwa mpinzani tena mpinzani wa Tanzania inatakiwa mda wote unaisema vibaya serikali na vyombo vyake. Wewe kuisifia serikali na spika huu siyo uzalendo kwa kambi yetu ya upinzani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyie ufipa hamna madhara Kwenye siasa endeleeni kula mbege
Waikumbuka hadithi ya mwenye hema na ngamia? Endeleeni kumruhusu ngamia aingize kichwa chake hemani na mwisho atamalizia mkia! Kifuatacho ni mwenye hema kulala nje na ngamia ndani ya hema ndio mtajua kuwa wapinzani Wana madhara au la!
 
Back
Top Bottom