Kubenea atumia ‘Wheel chair’ kwenda mbele ya kamati, ashindwa kuhojiwa

Hiyo kamati ya watu wa ajabu,unafiki,upambe,kujipendekeza kma spika wao,mbna makondakta aliwadharau hawakumfanya lolote,kumkamata na kumpeleka bungeni kazi yao kuonea upinzani tu,
Kama hawataki kusemwa wajiue waende ahera tu,kuwashwawashwa sio kitu kizuri
 
Kubenea haumwa chochote,alidhani angeweza kuvimbia mamlaka,kaona akodi kiti cha wagonjwa kikao kiahirishwe apate kwenda kumuomba radhi spika,kesho mtamuona kubenea akiwa kasimama na afya yake
 
pic+kubenea+2.jpg


Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, imeahirisha kumuhoji Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea kutokana na kufika mbele yake akiwa mgonjwa.

Kubenea amefika mbele ya kamati leo Jumatano saa nne asubuhi akiwa katika baiskeli ya wagonjwa (Wheel chair) chini ya ulinzi wa askari wa Jeshi la Polisi.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Kapteni mstaafu George Mkuchika amesema walikutana kutokana na kupelekewa shauri na Spika la kumuita Kubenea akidaiwa kudharau mamlaka ya Spika kwa kauli alizozitoa katika kanisa moja jijini Dar es Salaam.

“Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge inakutana pale inapoletewa shauri na Spika, tumeletwa mashauri ya Kubenea ya kudharau mamlaka ya Spika kwa kauli ambazo amezitoa katika kanisa huko Dar es Salaam,” amekaririwa Mkuchika katika taarifa iliyotolewa na Bunge.

Amesema utaratibu unamtaka mtu anayetakiwa kufika mbele ya kamati hiyo kupelekewa hati ya kuitwa na kwamba alishapelekewa.

Mkuchika amesema Kubenea amepelekwa akiwa katika baiskeli ya wagonjwa na kuiomba kamati impangie siku nyingine kwa hiyo wameridhia ombi lake.

“Kamati baada ya kumsikiliza Kubenea imeridhia ombi lake la kumpangia tarehe nyingine kwa kumpa muda wa kuangalia afya yake mpaka atakapopona,” amesema.
Mkuchika aliagiza Kubenea apelekwe katika Zahanati ya Bunge ili apewe huduma ya kwanza.

Awali, Kubenea baada ya kuhojiwa na kamati kama ataweza kuzungumza katika kikao hicho aliiomba kamati kumpangia siku nyingine kwa kuwa asingeweza kuzungumza kwa wakati huo kutokana na kuwa katika maumivu makali.

Septemba 12, Spika wa Bunge, Job Ndugai aliagiza mbunge huyo kufika mbele ya kamati hiyo kuhojiwa kuhusu tuhuma alizozitoa wakati wa ibada Septemba 10 kwamba Spika alisema uongo bungeni wakati akitangaza idadi ya risasi zilizopigwa kwenye gari la Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Tunaandika sana lakini sijui kama inasaidia.Ngoja tuendelee kwa sababu hapa ndio kwetu.
Kuna mambo ambayo hayahitaji kupaza sana sauti hasa ukishakosea!!
Tangu awamu hii imeingia pamekuwa na malalamiko ya kuwa mhimili wa serikali unaingilia bunge na mnakumbuka hata vurugu za upangaji wa kamati.
Pia mnakumbuka Tulia Ackson alivyoingia na kupata u naibu spika.
Ndugai alipaswa kufanya ambayo yangeonyesha hata kwa nje tu bunge sivyo kama tunavyoaminishwa,HAKUFANYA.
Funga kazi ni juzi wakati Raisi alipoeleza hadharani kuwa wakati wa kuunda kamati ya almasi na vito Spika alimpigia simu kuhusu wajumbe,AIBU ya mwaka!!Ndugai utajitetea nini katika hilo,badala ya kuomba ushauri wa hata naibu spika wako unakwenda kwa Raisi (Mhimili mwingine)na Raisi kalitoa kama lilivyo.
Ni bora ungenyamaza lakini hii nguvu inayotumika kwa ajili ya kauli ndogo kama kupishana idadi ya risasi ni kupoteza muda bure.
Leo nimesikia Zitto afikishwe haraka,mtu aliyeunguliwa na nyumba na vitu vyote.Haiwezi ikasubiri bunge la Novemba?
Hivi ukipiga magoti na kusali unazungumza maneno gani?
"Haikuwa dunia ila starehe zenye kupita na kudanganya"
 
My Take
Spika Ndugai anawezaje kulazimisha mtu akamatwe akiwa hospitalini na kupelekwa bungeni kwa nguvu na hatimaye kushindwa kumuhoji. Huyu ni kielelezo cha viongozi walio na akili ndogo kupewa majukumu makubwa
Kuwa Kichaa Sio Mpaka Kuokota Makopo!. Jee Tanzania Tuna Vichaa ...
Wanabodi,
Vichaa Viongozi, au Viongozi Vichaa?.
Kwa muktadha huo wa ukichaa, ukiwasikiliza matamko wanayotoa baadhi ya wanasiasa na viongozi wa serikali, vyama na taasisi hata wa mihimili, na ukafuatilia matendo yao,amri zao na maamuzi yao, utakubaliana na mimi kuwa, sisi Watanzania tuna vichaa wengi zaidi kuliko tunavyo jidhania.

What to do to help out.
iwekwe kabisa kwenye sheria, taratibu na kanuni, moja ya vigezo wa kuwa kiongozi wa ofisi za umma ni pamoja na kupimwa afya ya akili, ili kuepuka kuwa na viongozi vichaa?.

Paskali
Paskali
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom