Kubenea atumia ‘Wheel chair’ kwenda mbele ya kamati, ashindwa kuhojiwa

Kwani ilishindikana kupewa wito wa kwenda kwenye kamati ya bunge.....si busara kutumia nguvu nyingi kiasi hicho na gharama ya walipa kodi namna hii .........
Spika agharamie gharama zote hizo, This is totaly un fair, viongozi wa serikali hii wajipime, kama wanaona hawatoshi waachie ngazi tuu, Ni ukatili ulioje kumsafirisha mtu toka Hospitali alikokutwa anatibiwa hadi Bungeni Dodoma? akiwafia njiani je? Hivi kumeingia nini katika serikalini? Vichwa vimevurugwa kiasi kuwa matendo ya serikali yanashangaza!!!!!
 
pic+kubenea+2.jpg


Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, imeahirisha kumuhoji Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea kutokana na kufika mbele yake akiwa mgonjwa.

Kubenea amefika mbele ya kamati leo Jumatano saa nne asubuhi akiwa katika baiskeli ya wagonjwa (Wheel chair) chini ya ulinzi wa askari wa Jeshi la Polisi.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Kapteni mstaafu George Mkuchika amesema walikutana kutokana na kupelekewa shauri na Spika la kumuita Kubenea akidaiwa kudharau mamlaka ya Spika kwa kauli alizozitoa katika kanisa moja jijini Dar es Salaam.

“Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge inakutana pale inapoletewa shauri na Spika, tumeletwa mashauri ya Kubenea ya kudharau mamlaka ya Spika kwa kauli ambazo amezitoa katika kanisa huko Dar es Salaam,” amekaririwa Mkuchika katika taarifa iliyotolewa na Bunge.

Amesema utaratibu unamtaka mtu anayetakiwa kufika mbele ya kamati hiyo kupelekewa hati ya kuitwa na kwamba alishapelekewa.

Mkuchika amesema Kubenea amepelekwa akiwa katika baiskeli ya wagonjwa na kuiomba kamati impangie siku nyingine kwa hiyo wameridhia ombi lake.

“Kamati baada ya kumsikiliza Kubenea imeridhia ombi lake la kumpangia tarehe nyingine kwa kumpa muda wa kuangalia afya yake mpaka atakapopona,” amesema.
Mkuchika aliagiza Kubenea apelekwe katika Zahanati ya Bunge ili apewe huduma ya kwanza.

Awali, Kubenea baada ya kuhojiwa na kamati kama ataweza kuzungumza katika kikao hicho aliiomba kamati kumpangia siku nyingine kwa kuwa asingeweza kuzungumza kwa wakati huo kutokana na kuwa katika maumivu makali.

Septemba 12, Spika wa Bunge, Job Ndugai aliagiza mbunge huyo kufika mbele ya kamati hiyo kuhojiwa kuhusu tuhuma alizozitoa wakati wa ibada Septemba 10 kwamba Spika alisema uongo bungeni wakati akitangaza idadi ya risasi zilizopigwa kwenye gari la Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Kumbe al badir ilimpata Kubenea mpaka anatumia wheel chair??
 
Kwani ni risasi ngapi alizosema Spika kwa kudanganya na ukweli halisi ni risasi ngapi? wahesabu maganda tu and then muongo atajulikana... Na pia Muongo ndio anatakiwa aende kwenye kamati ya maadili...
 
Nina mashaka makubwa kama Mh, Kubenea alijipanga sawasawa kwa siasa za upinzani, huku angewaachia tu virambas kama Lema, Msigwa, Mdee, Mbilinyi, Mnyika, Bulaya n.k.
 
Baada ya Bunge kutumia nguvu kubwa kulazimisha Mh.Said Kubenea kupelekwa Dodoma kwenda kuhojiwa na Kamati ya Bunge,mahojiano hayo yameshindikana kutokana kuumwa kwa Kubenea

Ikumbukwe kuwa Spita Ndugai aliamuru Kubenea akamatwe licha ya kuwa alikuwa amelazwa kwa kutokana na homa.

Kamati baada ya kubaini kuwa Kubenea hayuko sawa ilishauri akimbizwe dispensary ya Bunge kwa ajili ya huduma ya haraka. Taarifa zinasema kwamba ilitumika wheel chair kumpeleka Kubenea mbele ya kamati

My Take
Spika Ndugai anawezaje kulazimisha mtu akamatwe akiwa hospitalini na kupelekwa bungeni kwa nguvu na hatimaye kushindwa kumuhoji. Huyu ni kielelezo cha viongozi walio na akili ndogo kupewa majukumu makubwa
Ndugai kishasahau kwamba alikuwa chupuchupu !!!
 
Baada ya Bunge kutumia nguvu kubwa kulazimisha Mh.Said Kubenea kupelekwa Dodoma kwenda kuhojiwa na Kamati ya Bunge,mahojiano hayo yameshindikana kutokana kuumwa kwa Kubenea

Ikumbukwe kuwa Spita Ndugai aliamuru Kubenea akamatwe licha ya kuwa alikuwa amelazwa kwa kutokana na homa.

Kamati baada ya kubaini kuwa Kubenea hayuko sawa ilishauri akimbizwe dispensary ya Bunge kwa ajili ya huduma ya haraka. Taarifa zinasema kwamba ilitumika wheel chair kumpeleka Kubenea mbele ya kamati

My Take
Spika Ndugai anawezaje kulazimisha mtu akamatwe akiwa hospitalini na kupelekwa bungeni kwa nguvu na hatimaye kushindwa kumuhoji. Huyu ni kielelezo cha viongozi walio na akili ndogo kupewa majukumu makubwa

Mtu mwenyewe ana mtindio ndo maana alimpiga mgombea mwebzake ubunge
 
Mi kuna wakati nasikitika kwa jinsi mambo yalivyo alafu baadhi ya watu wanashangilia,huwez kumlazimisha mtu anaeumwa kwenda kuhojiwa atafanyaje utetezi wake,kina ndugai nao wajue ni binadamu mwisho wa kila jambo mungu ndo ajuae maana uspika ni hapa hapa duniani
Si ndio nasikia ni makamanda ? kuitwa kwa Supika jamaa miguu ikafa ganzi , nyumbu bwana povu povu kumbe kamanda mchuzi tu
 
Anafanya maigizo ili wanaowatumia kuleta uchochezi wanaone hayo maigizo malengo wanazolipwa. Mwisho wa siku Tanzania itaendelea kuwa imara nayeye na wachache waotumiwa watakuwa kama toilet paper ikishatumika
 
Back
Top Bottom