Kubenea athibitisha umiliki wa kiwanja alichokataa Hussein Mwinyi, ataka ajiuzulu kama alivyoahidi

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968


Mbunge wa Ubungo Said Kubenea ameonyesha nakala zinazothibitisha umiliki wa kiwanja alichokataa waziri wa ulinzi Hussein Mwinyi na ametaka mbunge huyo kujiuzulu.

Amesema kiwanja hicho alikitaja bungeni na Dk. Mwinyi akadai madai yake yote ni ya uwongo mtupu na kukiwa hata na chembe ya ukweli atajiuzulu na sasa amemtaka ajiuzulu kweli kama alivyoahidi.

Mbunge huyo pia amesema ameapanga kumshitaki naibu spika kwenye kamati ya maadili kwa madai kuwa anatumia kanuni za bunge isivyo kikanuni
 
Hahahahaah nilikua naingalia hio clip, nashauri CCM hii ngoma waicheze taratibu, watashindwa mchezo kabla ya dakika tisini, wanajifanya wanawakomoa Wabunge wa upinzani kumbe ndio wanajichimbia kaburi. Ni wakati sasa Bunge kama Kweli linatenda haki limuombe Mwinyi asimamie maneno yake
 
Tatizo la kubenea amekuwa muongo muongo tangu kitambo sana na inaelekea ndio staili ya kutokea. Alituandikia kuwa lowassa fïsadi lakini baadaye akasema lowassa hakuwa fiŕadi. Amekuwa kigeugeu.
 
Ikidhibitika hizo nyaraka ni halali, Hussein Mwinyi ajiuzulu haraka sana.

Afate nyayo ya Baba yake Rais Mstaafu Ndug. Ali Hassan Mwinyi.
Mkuu hawa mawaziri wanatumia vibaya mwanya huu wa kuwabana wapinzani
 
Asante sana mh Kubenea kwa kulisimamia unalo liamini na huyo waziri asitake kuiaibisha serikali awachie ngazi tu
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom