Kubenea afuta kusudio la kumshitaki Makonda na DPP

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,206
42,068
Mahakama ya Hakimu mkazi Kinondoni imeridhia ombi la mawakili wa Mwandishi wa Habari, Said Kubenea la kuondoa maombi ya kuwashtaki Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaama, Paul Makonda.

Hatua hiyo imejiri leo Ijumaa, Desemba 3, 2021 mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Aron Lyamua ambapo upande wa mleta maombi, Said Kubenea mawakili wake, Hekema Mwasipo umedai kuwa wamefikia hatua hiyo kutokana na kasoro mbalimbali zilizojitokeza katika maombi ya kufungua kesi hiyo na kwamba wanakusudia kuongeza mashtaka ambayo awali hayakuwepo kwenye maombi hayo.

Miongoni mwa kasoro zilizojitokeza ni uandishi wa majina ya mpelekewa maombi na ya aliyeapa ambayo yapo tofauati jambo ambalo wanahofia kuwa yanatakiwa kufafana. Wamedai kuwa wanakusudia kuwashtaki wa watu hao kutokana na madai ya kushindwa kutimiza vyema wajibu wao.

Baada ya maombi hayo wakili wa serikali, Daisy Makakala amekubaliana na ombi la mawakili wa Kubenea bila pingamizi. Hata Hivyo Mawakili wa Kubenea tayari wamewasilisha maombi mengine ambayo yamefanyiwa marekebisho ambayo awali kulikuwa na mapungufu.

Kinachosubiriwa sasa ni mahakama kupanga tarehe ya kusikiliza kesi hiyo pamoja na kuweka wazi namba ya kesi na aina ya mashtaka yanayowakabili.
 
Aibu kubwa sana kwa wanafiki na wasaliti Chadema wameanzisha kijigazeti uchwara kinaitwa raia mwema ambako kila siku kichwa cha habari ni Makonda na Sabaya.

Acheni hizo biashara ya madawa ya kulevya itawalaani vizazi vyenu hapo ufipa.
 
Laana utawatafuna kubenea na watu waliomtuma kulipiza kusasi kupitia mgongo wake, ikumbukwe kwamba hao wanaomtuma na wao hawatokaa madarakani siku zote na hao wahuni wanajulikana;kama tanzania tumefikia hatua hiyo kila kiongozi akipata nafasi ya juu atakuwa analipiza visasi kupitia migongo ya watu kama kubenea marope na nape achen tabia hiyo hii nchi siyo ya kwenu mtakuja kujuta maishani mwenu hayo mnayoyafanya yanajulikana na wengi wabayajuwa mimi nimewaletea ujumbe
 
baada ya andiko la Mayalla ambapo alishauri kisomi na kitimamu leo....makofi kwa mayalla
Said Kubenea mawakili wake, Hekema Mwasipo umedai kuwa wamefikia hatua hiyo kutokana na kasoro mbalimbali zilizojitokeza katika maombi ya kufungua kesi hiyo na kwamba wanakusudia kuongeza mashtaka ambayo awali hayakuwepo kwenye maombi hayo.
 
Mkuu,hii inchi ina mambumbumbu na mazuzu mengi sana kwa hisani ya Chama Cha Majambazi/Mafisadi.
Hata kuelewa sentesi ya maneno 12 inatakiwa wawe na ubongo wa "mhitimu wa M.I.T." kweli!!??
CCM mlichowafanyia hawa watu kitaambukiza kizazi chao kuwa mazuzu hadi kizazi cha nne.
 
Aibu kubwa sana kwa wanafiki na wasaliti Chadema wameanzisha kijigazeti uchwara kinaitwa raia mwema ambako kila siku kichwa cha habari ni Makonda na Sabaya.

Acheni hizo biashara ya madawa ya kulevya itawalaani vizazi vyenu hapo ufipa.
GAZETI LA UHURU LILIANDIKA RAIS SAMIA HANA NIA YA KUWANIA URAIS 2025, LIKAFUNGIWA SIKU 7 NA RAIS SAMIA AKALIITA " KIGAZETI". KWA HIYO UHURU NI KIGAZETI.
 
Laana utawatafuna kubenea na watu waliomtuma kulipiza kusasi kupitia mgongo wake, ikumbukwe kwamba hao wanaomtuma na wao hawatokaa madarakani siku zote na hao wahuni wanajulikana;kama tanzania tumefikia hatua hiyo kila kiongozi akipata nafasi ya juu atakuwa analipiza visasi kupitia migongo ya watu kama kubenea marope na nape achen tabia hiyo hii nchi siyo ya kwenu mtakuja kujuta maishani mwenu hayo mnayoyafanya yanajulikana na wengi wabayajuwa mimi nimewaletea ujumbe
Yaani kupeleka jambo mahakamani kutafuta haki ndio unasema ni kulipiza kisasi. Hivi kila mtu akikosea unataka hatua zisichukuliwe kisa tu itaonekana ni kulipiza kisasi, je tutakuwa na jamii ya namba gani.

Unataka kila atakayepata nafasi ya madaraka afanye jinsi anavyotaka hata kunyanyasa watu.

Kama mtu anaona kuna ukiukwaji wa sheria anayo haki ya kulifikisha ktk vyombo vya haki
 
Laana utawatafuna kubenea na watu waliomtuma kulipiza kusasi kupitia mgongo wake, ikumbukwe kwamba hao wanaomtuma na wao hawatokaa madarakani siku zote na hao wahuni wanajulikana;kama tanzania tumefikia hatua hiyo kila kiongozi akipata nafasi ya juu atakuwa analipiza visasi kupitia migongo ya watu kama kubenea marope na nape achen tabia hiyo hii nchi siyo ya kwenu mtakuja kujuta maishani mwenu hayo mnayoyafanya yanajulikana na wengi wabayajuwa mimi nimewaletea ujumbe
Soma habari uelewe kenge wewe
 
Aibu kubwa sana kwa wanafiki na wasaliti Chadema wameanzisha kijigazeti uchwara kinaitwa raia mwema ambako kila siku kichwa cha habari ni Makonda na Sabaya.

Acheni hizo biashara ya madawa ya kulevya itawalaani vizazi vyenu hapo ufipa.
Wao ni wasaliti wa Chadema halafu unadai wanauza madawa ya kulevya makao makuu ya CDM ?😅
Chuki isiyo nasingi inakupofusha amigo
 
Aibu kubwa sana kwa wanafiki na wasaliti Chadema wameanzisha kijigazeti uchwara kinaitwa raia mwema ambako kila siku kichwa cha habari ni Makonda na Sabaya.

Acheni hizo biashara ya madawa ya kulevya itawalaani vizazi vyenu hapo ufipa.
Hahahah

Usilolijua ni sawa na usiku wa giza

Ova
 
Back
Top Bottom