Kubenea acharuka, apinga bajeti ya jiji la Dar kupelekwa bungeni

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,744
239,394
Mbunge huyo makini ambaye Wengi wanapenda kumwita mbunge wa Taifa kutokana na uzalendo wake wa kulinda maslahi ya nchi , amesema ni lazima kwanza bajeti ijadiliwe na madiwani wa jiji kabla ya kupelekwa bungeni .

Haiwezekani bajeti iliyoandaliwa na watendaji wa jiji ipelekwe moja kwa moja Tamisemi badala ya kupitia kwanza kwenye baraza la madiwani ili ijadiliwe na mapungufu yarekebishwe .

Mh huyo kwa msisitizo amepanga kupeleka barua kwa spika kumjulisha juu ya jambo hilo .

My Take - ninaona harufu ya UKAWA kuhujumiwa kwa udi na uvumba katika mikakati yao ya kuboresha jiji .
 
Hivi CCM kwa nini wasiwape UKAWA uhuru wa kuendesha halmashauri ili tujue uwezo wao.

Kwa nini wanawazonga zonga kila wanapotaka kuonyesha weledi.

CCM waelewe hawawakwamishi UKAWA ila wanatukwamisha wananchi tunaotaabika kila siku.
 
idawa

Swali hilo na mie linaniumiza sana. Hivi ni dhambi gani kwa mtanzania mwenzako aliyepewa ruhusa ya kikatiba na watanzania wenzake kusimamia mali na maendeleo ya mahali flani, wewe uliyeshinda karibia asilimia 60 nchi nzima na halmashauri kibao uwe na wivu juu yake?

Najaribu kwa nguvu zote kumwamini Mh. Rais kama mtu anayependa HAKI na MTANZANIA zaidi kuliko UCcm wake lakini nashindwa!
 
Nani kubenea hivi ile ajenda yake ya wabunge wanawake waupinzani kudhalilishwa na polisi kwa kuvuliwa vyupi na chachanduu imeishia wapi??? Mbimbinyo hiyoo hajielewi
 
idawa

Swali hilo na mie linaniumiza sana. Hivi ni dhambi gani kwa mtanzania mwenzako aliyepewa ruhusa ya kikatiba na watanzania wenzake kusimamia mali na maendeleo ya mahali flani, wewe uliyeshinda karibia asilimia 60 nchi nzima na halmashauri kibao uwe na wivu juu yake?

Najaribu kwa nguvu zote kumwamini Mh. Rais kama mtu anayependa HAKI na MTANZANIA zaidi kuliko UCcm wake lakini nashindwa!

Mkuu hapo ukiangalia kwa jicho la tatu utagundua ccm huenda wanadhambi nyingi kuliko tunazozifahamu au kuzisikia ama ni hofu ya kupokwa madaraka.
 
Back
Top Bottom