Kubena is back & doing fine

Invisible

JF Admin
Feb 26, 2006
16,285
8,340
Kubena is back & doing fine.

Ndio kafika airport kutokea india alipokwenda kutibiwa.

Stay tunned
 
Karibu sana Tanzania maana nilikuwa na wasiwasi nilivyoona yule mama waziri Ghasia (inasomeka fujo au ukosefu wa amani) alivyokwenda India kumtembelea!
 
Asante kwa ujumbe huu,

Ninamtakia kila la kheri na mafisidi wasimsogelee,


very good news indeed.
 
Wasiwasi wangu mkubwa ulikuwa kwamba he was going to lose his sight, naomba mtujulishe kama bado anaona- bado anaweza kuendelea kuwaona na kuandika habari nzito za mafisadi?
 
Nakuja sasa hivi airport Invisible kumpokea ili nijionee mwenyewe thanks natoka sasa
 
Mungu Ibariki,Habari Njema. Hawa jamaa walitaka kuua kabisa.

Najaribu kupata Jawabu ni kwa nini Sirikali ilikuwa mstari wa mbele kabisa katika suala hili?

Je ni kwa kuhofia wanamtandao waliojaribu kuua magazeti kwa njia ya kuyanunua na baada ya kuona yanachipuka mengine wakaamua kuyazima kwa kuwazima wanaoyachipusha? Nipeni Jibu
 
Posted Date::1/16/2008 Mhariri aliyeshambuliwa arejea toka India adai vigogo,mafisadi wanahusika
Na Muhibu Said
Mwananchi

MHARIRI Mtendaji wa magazeti ya MwanaHalisi na Mseto, Saed Kubenea, aliyekuwa amelazwa hospitali India akipatiwa matibabu ya macho, amerejea nchini na kudai kuwa baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi, wakiwamo vigogo wa serikali, ndio walihusika na kushambuliwa kwake.

Kubenea (37) ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited, inayochapisha magazeti hayo, amesema anaamini hivyo kwa kuwa tukio la kushambuliwa kwake lilitokea katika mazingira ya kazi yake na pia baada ya moja ya magazeti yake kuyaweka majina na picha za watuhumiwa hao hadharani.

Alisema hayo alipozungumza na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na nje ya nchi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam jana.

"Suala, hapa kuna mkono wa mtu. Wanaweza kuwa viongozi wa serikali kwa kuwa wapo baadhi yao walituhumiwa kuhusika na ufisadi na gazeti langu likaweka hadharani majina yao na pia wanaweza kuwa watu wengine," alisema Kubenea.

Kutokana na hali hiyo, aliitaka timu ya wataalamu kutoka jeshi la polisi inayochunguza tukio hilo, kuhakikisha inatoa ripoti ya uchunguzi huo baada ya siku 15 ilizopewa kukamilika, vinginevyo, ataingia mtaani kueleza anavyofahamu yeye Jumatatu wiki Ijayo.

Kubenea ambaye alipoteza uwezo wa kuona kutokana na kumwagiwa kemikali usoni na watu wasiojulikana ofisini kwake Kinondoni, jijini Dar es Salaam Januari 5, mwaka huu, alilazwa katika Hospitali ya Apollo iliyoko India baada ya kuhamishwa kutoka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), jijini Dar es Salaam alikolazwa awali.

Alirejea nchini jana saa 8:10 mchana na ndege namba E 805 ya Shirika la Ndege la Ethiopia (Ethiopia Airlines), huku akiona kwa kutumia msaada wa miwani na kulakiwa na umati mkubwa wa wananchi waliofurika uwanjani hapo, kuanzia saa 7:00 mchana jana.

Akielezea afya aliyorudi nayo kutoka India, alisema kutokana na matibabu aliyoyapata katika kipindi cha siku kumi alizokuwa akitibiwa huko, hivi sasa anaona kidogo tofauti na hali aliyokuwa nayo kabla hajaondoka nchini.

Hata hivyo, alisema hadi sasa madaktari wanaomtibu nchini humo, bado hawajabaini aina ya kemikali aliyomwagiwa usoni. "Madaktari walichosema ni kwamba, nilichomwagiwa usoni, ni moja ya sumu kali," alisema Kubenea.

Hata hivyo, alisema atakuwapo nchini kwa miezi mitatu akitumia dawa alizopewa na madaktari wa hospitali hiyo na baada ya kipindi hicho, atarudi India kuendelea na matibabu katika hospitali hiyo.

Alisema awali, aliandikiwa na madaktari hao kulazwa katika hospitali hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu, lakini ameona ni vema arejee nchini na aendeleea kutumia kwanza dawa hizo ili kuokoa gharama kubwa za kukaa hospitalini hapo kwa kipindi hicho ambacho angelazimika kutumia zaidi ya dola 36,000 (sawa na Sh37 milioni). Aliwashukuru Watanzania wote walioungana naye katika tukio hilo.

Alisema pamoja na masaibu yaliyomkuta, hawawezi kulegeza kamba na badala yake, wataendelea na msimamo wao wa kupambana na maovu na waovu katika jamii. "Nitaendelea na mapambano. Aluta Continua," alisema Kubenea.

Januari 5, mwaka huu, saa 3:00 usiku, watu watatu wenye silaha, walivamia ofisi za magazeti ya MwanaHalisi na Mseto zilizoko Kinondoni, jijini Dar es Salaam walimjeruhi Kubenea kwa kupimga na kitu kizito karibu na jicho la kulia na kisha kummwagia kemikali usoni. Pia walimjeruhi mshauri na mwalimu wa habari wa magazeti hayo Ndimara Tegambwage kwa mapanga.
 
yetu macho na masikio,sasa kazi ndio kwanza inaanza maana hizi ni mvua za kupandia masika yenyewe bado,wapi makamba na mudhiri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom