Kubemendwa: Hiki kitu kweli kipo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kubemendwa: Hiki kitu kweli kipo?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Malila, Jul 3, 2009.

 1. M

  Malila JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Kule uswahilini mara nyingi ndiko kunakosikika hili neno,naomba kuuliza, jambo lenyewe ni kubemenda mtoto. Sijawahi kuona mtoto aliyebemendwa. Hivi ni kweli kitu hicho kipo? na kinasababishwa na nini hasa? Kwa anayejua tafadhali mwaga hapa.
   
 2. GP

  GP JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  kubemenda mtoto ni ile hali ya kufanya mapenzi na mama mjamzito aliyekaribu kujifungua say miezi 7.5 hadi 9, na kutoa mbegu za kiume ambazo huweza kumwathiri mtoto tumboni
  mara nyingi mtoto aliyebemendwa anakua na mabaka mwilini meusi hivi, mara nyingi tumboni, kwenye mbavu au sehemu za mikono(watoto nilio wahi kuwaona)
   
 3. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,581
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  George_Porjie, Mimi nilidhani kummbemenda mtoto kunatoka na mama kufanya mapezi wakati akiwa na mtoto mchanga, kumbe nilikuwa na tafasiri isiyo sahii, Asante mkuu.
   
 4. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2009
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Are you SURE???

  nimesoma kwamba mwanamke mjamzito anashauriwa afanye mapenzi ili njia ya uzazi iweze kupanuka na iwe tayari kwa mtoto kupita!!! Sasa unaposema hii ndo kubemenda then i think most or all the children have been bemendwad!!!

  Ni hatari... any one with relevant info wasaidie wazazi
   
  Last edited: Jul 3, 2009
 5. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  George_Porjie you are wrong, The farmer you half correct:

  Kubemeda mtoto ni matokeo ya Mama na Baba wenye kichanga kufanya zinaa (kutembea nje ya ndoa yao) wakati kichanga kile bado kinanyonyeshwa. Hii dhana kwa tafsiri ya kisasa maana yake ni "malnutrition".

  Endapo Mama ataendekeza ebeneke wakati anayonyesha most likely lishe kwa mtoto itapungua sana and equally endapo Baba ataendekeza "nyumba ndogo" kipindi hicho Mama atakuwa stressed na hataweza kumpatia mtoto lishe ya kufaa (esp kama anamnyonyesha unakuta hata maziwa hayatoki ifaavyo).

  Kubemenda = Kwashakoo

  Weekend Njema
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kubemenda mtoto ni ile hali ya mama akiwa ananyonyesha mtoto alafu kitoto bado kidogo anapigwa mimba ingine basi mtoto hapo unambemenda.
   
 7. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,790
  Likes Received: 2,452
  Trophy Points: 280
  Baba enock you are almost true.

  Kwa kuongezea tu ni kwamba kubemenda si tu kutembea nje ya ndoa kwa wazazi wote wawili;unaambiwa kwamba utamubemenda mtoto endapo utafanya mapenzi aidha ndani ya ndoa au nje ya ndoa halafu bila hata kufanya usafi toshelezo ukaamua kwenda kumshika mtoto au kumnyonyesha mtoto na shombo za majasho basi atakuwa affected hna hiyo malnutrition.

  Hivyo si kwamba lazma uende au utoke nje ya ndoa ila hata ndani inaweza kutokea kama hakuna usafi mara tu mmalizapo shughuli zenu.

  Unashauriwa mnapomalizo shughuli zenu unashauriwa kuwa msafi kabla hata kumnyonyesha mtoto kwa mama na kwa baba kumshika au kumbeba mtoto.
   
 8. M

  Malila JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Bonge la somo leo,sasa hapa kipi ni kipi, usafi,uzinzi,lishe(malnutrition), mimba kabla ya muda kwa mtoto aliyetangulia,hata hivyo bado naomba tuendelee kukata issue. leo mmenifumbua macho.
   
 9. kamau

  kamau Member

  #9
  Jul 3, 2009
  Joined: Nov 8, 2008
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nadhani kubemenda ni mtoto kukosa matunzo na afya kudorora,haijalishi utoke au uingie katka ndoa
   
 10. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2009
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,272
  Likes Received: 558
  Trophy Points: 280
  Kubemendwa sio malnutrition. Wala havina uhusiano. Mtoto anaweza akawa anapata chakula vizuri kabisa na bado akabemendwa. Kwangu mimi na ambavyo nafahamu ni ile hali ya mama kufanya mapenzi na kumnyonyesha mtoto baada ya muda usio mrefu. Inakuwaje. Mama anayenyonyesha anapofanya mapenzi (katika hali ya kawaida, yaani staili ya kifo cha mende) kutakuwa na msuguano kati ya mwili wake (na hasa sehemu za matiti) na ule wa mwanaume. Msuguano huo utasababisha joto la maziwa ndani ya matiti kuongezeka (kwa lugha nyingine maziwa hayo yanakatika, yanakuwa hayako katika hali ya kawaida ya utulivu). Sasa kabla maziwa hayo ndani ya matiti hayajakaa sawa, mtoto akanyonyeshwa, lazima ataharisha, tena ataharisha maziwamaziwa. Kitendo cha kuharisha maziwamaziwa hivi ndio kinaitwa kubememdwa. Kwa hiyo inawezekana kabisa baba na mama ndani ya ndoa wakambemenda mtoto.
   
 11. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Very correct and insightful. Ni maneno yenye tafsida. Kwa wengine hupitishwa kizazi na kizazi bila kujua maana. One has to think outside the box sometimes
   
 12. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #12
  Jul 3, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mtoto akiwa tumboni anakuwa yuko ndani ya kifuko, mbegu zinaingia ingiaje tena na kumwathiri?! Uliyoyasema kuhusu mtoto kuwa na mabaka mabaka, sidhani kama sababu ndiyo hiyo, sidhani. In fact uliyoyasema mimi naona ni aina mojawapo ya mwendelezo wa imani zilizokuwa unfounded zenye lengo la kunyanyapaa baadhi ya watu (wenye mabakamabaka). Kwani naamini kuna jambo lingine kabisa tofauti na hiyo sababu uliyotoa inayosababisha hayo mabakamabaka.
   
 13. L

  Lukundo Member

  #13
  Jul 3, 2009
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jf, the home of great thinker? Hii inatia shaka kwa majibu hapo juu. Waliogusia malnutrition na malezi hafifu wako right, walioongelea ngono , hizo ni misconception. Nimefanya thesis kwa hii kitu. Mwanzo wa neno ni pwani, ni inatokana na malezi hafifu ya kimlo kwa mtoto baada ya kuingiliwa na mapenzi mapya au stress kwa mlezi wa mtoto.
  Haina tofauti na maana ya kwashiorkor, ambayo mwanzo wake ni ghana, ikiwa na maana ya mtoto aliyetelekezwa baada ya mama kupata mtoto mwingine kabla ya aliyefuatishwa kukua, au kuweza kutokuwa tegemezi. Ingieni google wakubwa.
  IELEWEKE KUWA KUFANYA MAPENZI NA MAMA MJAMZITO, HAKUNA UHUSIANO NA MTOTO ATAKAYE ZALIWA KAMA YAI LILISHATIWA KIINI CHA KIUME. MADHARA PEKEE NI KAMA MAMA ANACERVICAL INCOPETENCE[SHINGO YA KIZAZI ILIYOLEGEA] . JF HII IWE MADA MAALUMU TUWATOE WATU MITONGOTONGO.
   
 14. M

  Malila JF-Expert Member

  #14
  Jul 3, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  asante mkuu kwa mchango wako,ngono na ukuaji wa mtoto anayepata lishe ya nguvu uhusiano uko wapi hapo.
  Mkuu leta nyingine,ili tukiunganisha na wenzetu tunapata jibu safi.
   
 15. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #15
  Jul 4, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  sahihi kabisa congo, ningependa kuongezea

  mama ambaye ananyonyesha akishamaliza kufanya mapenzi anatakiwa ayakamue yale maziwa machafu (maziwa yanayokatika) mpaka maziwa masafi yaanze kutoka, alafu aoge(au ajikoshe sehemu za matiti na kifuani) kabla ya kumnyonyesha mwanawe.
  mama akiweza kufanya hivi hambemendi mtoto hata siku moja na kama hawezi kufanya hivi ni bora amwenyeshe mtoto wake maziwa ya chupa
   
  Last edited: Jul 4, 2009
 16. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #16
  Jul 4, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...kwa jinsi mlivyoelezea naona Fidel80 pekee ndiye yupo 'njia' sahihi.

  ...kichanga kinahitaji sana maziwa ya mama hususan kutokana na lishe bora yatokanayo na maziwa hayo na psychological bonding.
   
 17. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #17
  Jul 4, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Lakini mbona mambo haya yapo zaidi uswahilini? Siyasikii sana maeneo mengine!
   
 18. L

  Lugaon Member

  #18
  Jul 4, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mmmh sijui kama ni kweli!!!
   
 19. tzengo

  tzengo Member

  #19
  Jul 4, 2009
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  sijui maana halisi ya mnachokiengelea,lakini bado napata wakati mgumu kuelewa hizo 'imani' za wengi.maana naona maelezo mengi hayaelezei ukweli.
  mmh ngoja tusubiri tuone wengine watasemaje huenda ukweli ukaja baadaye.
   
 20. M

  Mrekebishaji Senior Member

  #20
  Jul 4, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 168
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Jamani mimi ni mgumu kuamini mambo mengine. Ukweli hapa inabidi kutenganisha athari za kiafya na zile za kiimani potofu. Kwa mfano sitetei mzazi kutoka nje, lakini hii haimanishi kumuathiri mtoto, ila kama hiyo itapunguza matunzom kwa mtoto ndiyo inaathiri.
  Mtu anaweza asitoke nje ya ndoa na asimtunze mtoto. Japo ukweli ni kwamba kutoka nje ya ndoa mara nyingi(sio mara zote) huathiri ku-care familia.
   
Loading...