Kubemenda ni nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kubemenda ni nini?

Discussion in 'JF Doctor' started by Ndibalema, Feb 24, 2010.

 1. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,937
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 160
  Wana JF.

  Kuna rafiki yangu ana mtoto mchanga, amekuja nimpatie ushauri na maelezo juu ya swala zima la kubemenda (Sina hakika kama ni neno rasmi).
  Hasa ningependa kujua 'mechanism' na njia zinazosababisha jambo hili.
  Je, kutoka nje ya ndoa ndio sababu ya jambo hili?
  Wengine wanasema ukitoka kufanya mapenzi na mpenzi mwingine kisha ukaja ukambeba mtoto wako (anae nyoya) basi tayari unamsababishia tatizo hili.
  Naomba msaada wenu wana JF
  ili nipate cha kumweleza swahiba wangu.
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,640
  Likes Received: 625
  Trophy Points: 280
  Nasikia ni kumuharibu mtoto mdogo kama ananyonya harafu mwanamke anakuwa sio mwaminifu katika mahusioni..sijui ni wote Mke/mme au Mke
  wajuzi watatuhabarisha !
   
 3. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #3
  Feb 24, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,318
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Wanasema ni wote inabidi muwe waaminifu, maana inasemekana hata baba akitoka nje ya ndoa then akaja kumshika mtoto kabla hajaoga tatizo hilo pia litatokea. sijui sayansi yake hapo imekaa vipi, labda madakitari watatuambia
   
 4. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #4
  Mar 4, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,608
  Likes Received: 1,813
  Trophy Points: 280
  ila mara nyingi huwa inatokea kama mama atapata Mimba wakati bado mtoto ananyonya
   
 5. Katibukata

  Katibukata Senior Member

  #5
  Mar 4, 2010
  Joined: Dec 27, 2007
  Messages: 183
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ninavyoelewa mimi, kumbemenda mtoto ni kudhoofu afya yake kutokana na kunyonya maziwa machafu. Mama akishakuwa mjamzito maziwa yake huwa yanabadilika na hivyo huwa si salama kwa mtoto.
  Mtoto anahitaji uangalizi wa khali ya juu ktk usafi. Hivyo mkono wowote unaomshika lazima uwe msafi hata kama hukutembea nje ya ndoa. Jasho, na vitu vingine vichafu huathiri afya ya mtoto... sharti kuoga kabla ya kumshika, vinginevyo UTAMBEMENDA.
   
 6. Jerome

  Jerome Senior Member

  #6
  Mar 4, 2010
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unajua sisi watu wa zamani tulikuwa tunalea kikwelikweli mama akijifungua wanatengana mahusiano ya kimapenzi na baba mpaka miaka miwili au zaidi mtoto akue aache ziwa kabisa,baba alikuwa anavumilia wala hatembei nje muda wote huo ndiyo maana tulikuwa na afya za kweli siyo sasa mama hata nyuzi hazijapona vizuri anaanza kisa anshindana na baba mtambemenda mtoto hapo mwisho atakuwa fundi viatu na maneno mengi urefu futi tatu na nusu
   
 7. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #7
  Mar 5, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Teheehee tehe
  Wanaume mmesoma hapo!
   
 8. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #8
  Mar 5, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  kwahiyo mke na mume wakilibeneka wao kwa wao haina shida eeh?
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...