maatope
JF-Expert Member
- Sep 19, 2013
- 1,424
- 956
Kingwendu: Ningepewa airtime ningekuwa level moja na Diamond na Alikiba
Mchekeshaji maarufu nchini, Kingwendu amesema kama nyimbo zake zingepata promotion ya kutosha, angekuwa anashindana na wasanii wanaofanya vizuri kwa sasa, Diamond na Ali Kiba.
Kingwendu ambaye alikuwa katika show za mwisho wa mwaka nchini Ujerumani hivi karibuni, ameiambia Bongo5 kuwa hali hiyo inamfanya aanze kutafuta maneja ili aweze kusimamia kazi za muziki wake.
“Mwaka jana nimetoa nyimbo tatu lakini zote hazikupata airtime ndio maana hazikufanya vizuri lakini kwa sababu ni nyimbo nzuri zingepata airtime ningeshindana na akina Ali Kiba na Diamond ambao wanafanya vizuri,” amesema.
Aliongeza, “Sijakata kataa, mwaka huu kuna kazi mpya nimeziandaa pamoja na video mpya. Pia nikifanikiwa kupata meneja wa kusimamia muziki wangu natumaini nitafika mbali sana kwa sababu muziki wa sasa ni mipango tofauti na ule wakati nimetoa Mapepe.”
Kingwendu anadai anapenda kufanya muziki na filamu kwa pamoja kwa sababu vyote vinamlipa vizuri.
My take:hii sio fair kwa legendary wa music mtamu kama wa Kingwendu