Kubanwa na haja kubwa kila ninapokuwa katika chombo cha safari

KALENDA

Member
Jan 21, 2011
72
28
Naomba msaada, kila ninapopanda katika basi au kukaa pamoja na watu zaidi ya watatu nahisi kubanwa
na haja kubwa(stool).

Nikienda chooni kakitoki kitu na nikiwa katika usafiri baada ya kushuka hali hiyo huwa inapotea. Nimekwenda hospitali hali hii hawaifahamu wananipa dawa za kuharisha tu.

Naomba msaada wenu.
 
Inawekana ikawa ni stress.

Labda huwa waogopa ukiwa kwenye gari au hujiamini ukiwa kati ya watu. Hii itasababisha kuongeza gastrointestinal motility na si ajabu ukawa na hisia za kutaka kutoa choo. Labda ukiwa safarini waweza ukawa wanywa dawa kama amytriptiline.

Lakini muhimu ni kupunguza hofu.
 
the boss, je unafahamu matibabu ya "anxiety kwenye public" .

matatizo ya kisaikolojia zaidi...
Chanzo ni jinsi ulivylelewa au kupata tatizo kama kubakwa hivi utotoni....

Kwa hiyo unakuwa una feel guilty mbele ya watu...

Unahisi kama watu wakikutazama wanaona aibu yako fulani ambayo unaijua mwenyewe...

Wakati ni hisia zako tu....
 
yes hiyo ni anxiety kwanza jiamini ondoa hofu then kama ikizidi ndo unaweza kutumia amityptyline ila ikizidi baada ya kfanya hayo hapo
nothing wrong with you
 
kitaalamu inaitwa IBS , mi inanitokea nikiwa nasubiria matokeo yangu ya mtihani .. i keep on refreshing page kucheck matokeo kama yameingia but for me si haja.. bali stress ulcers .. baada ya stress kwisha zinapotea.
 
kitaalamu inaitwa IBS , mi inanitokea nikiwa nasubiria matokeo yangu ya mtihani .. i keep on refreshing page kucheck matokeo kama yameingia but for me si haja.. bali stress ulcers .. baada ya stress kwisha zinapotea.

Hata mimi nadhani itakuwa Irritable Bowel Syndrome (IBS) kwani baada ya kuhangaika niliona dalili zilizotajwa kuwa za IBS ninazo, kama tumbo kuunguruma, kukosa choo kwa muda pamoja na tumbo kujaa gas. Niliambiwa nitumie pepper mint tea ingesaidia lakini kabla sijaanza m2 mwingine alinijulisha kuwa hiyo chai inatabia ya kupunguza nguvu za kiume hivyo akanishauri nitumie mafuta ya olive (olive oil).

Lakini hadi leo tatizo not solved.
 
Back
Top Bottom