Kubambikizwa kesi na Mwajiri

Myhope

Senior Member
Jul 20, 2017
154
67
Mwajiri wangu amenibambikizia kesi ya wizi, akanishitaki Polisi kisha uchunguzi ukafanywa na jeshi hilo la Polisi majibu yakaja kwamba sina kosa hilo na wakashindwa kunipeleka mahakamani.

Baadaye Mwajiri akaamua kunifukuza kazi nikiwa na mkataba wa kudumu. Niliamua kumburuza CMA Mwajiri wangu.

Swali langu ni kwamba " Nikishinda hii kesi huko CMA na kurudi kazini. Je, naweza kumfungulia Mwajiri wangu kesi ya Madai kutokana na kubambikizwa kesi ya wizi?

Naomba msaada wa kisheria kuhusu hili.
 
Mkuu owomkyalo nashukuru kwa kuniita hapa, ubarikiwe. Mkuu sana Katus Manumbu , kwanza nakupa pole. Pili, fahamu kuwa ili kumshtaki mtu yeyote(akiwemo mwajiri) kwa Kushtakiwa kwa Hila (Malicisious Prosecution) kuna vigezo vyake.

Jambo kubwa ni kwamba kesi husika inapaswa kusikilizwa na Mahakama yenye mamlaka ya kufanya hivyo na hukumu kutolewa ikikupa ushindi kuwa huna hatia. Yaani Jamhuri na wewe kusikilizwa na wewe kuachiwa huru.

Kwa mujibu wa taarifa yako hiyo, hakukuwahi kuwa na kesi ya jinai dhidi yako achilia mbali kusikilizwa mahakamani. Hadi hapo, huwezi kumshtaki mwajiri wako kwa kukushtaki kwa hila.

Lakini, unaweza kuunganisha kitendo cha Mwajiri kukukabidhi polisi kwa uchunguzi na kuachishwa kwako kazi katika kuonesha nia ovu ya mwajiri wako kukuachisha kazi kinyume na sheria. Tena, waweza kuomba fidia kwa madhila uliyoyapata kwa kuachishwa kazi na hata kukabidhiwa polisi.

Nakushauri kwasasa ujikite na mgogoro wako wa kikazi na uunganishe humohumo mambo yote yakiwemo yanayowahusu polisi. Kila la heri!
 
Back
Top Bottom