Bubu Msemaovyo
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 3,941
- 3,042
WAkati ule ulikuwa ni wakati wa "UKWELI na UWAZI" Kauli yako hii ndiyo Azimio lako utabaki nalo milele na kamwe itakuwa hivyo kama Mwl Nyerere alivyotetea Azimio la Arusha hadi sasa. Sisi wananchi tupo pamoja nawe katika mchakato wa kuzungumza kwa UWAZI na UKWELI. Tuache tuseme. Yapo mengi mazuri uliyoyafanya lakini pia yapo mengi mabaya ambayo pia uliyafanya wewe mwenyewe ama watendaji wako ukayapa baraka na sasa yamekuwa kama uonavyo. Kuwa muungwana ni jambo la msingi kwako lakini tunajaribu kujiuliza kwanini unajitetea kwa kitu ambacho kiko wazi? Nikimkumbuka siku Ballali alipozungumza na waandishi wa habari na kukanusha kwamba BoT ni shwari na nikijua kwamba yeye si mwanasiasa na nyie ndiyo wanasiasa nakamilisha mawazo yangu kwamba yapo mengi sana ninyi wanasiasa hamjatutendea haki sisi wananchi. BoT mnahusika sana mengi mtasema lakini sisi wananchi hatukubali kamwe. Mliiba fedha BoT na ili kufidia pengo hilo mkaongeza kodi kwa makampuni kwa manufaa yenu, tunawalaani sana. Hata hivyo "Sauti ya watu ni sauti ya Mungu" Mungu ametusikia na ataendelea kutusikiliza vilio vyetu.