Kubali au kataa kwa hili wengi wa wabunge wa ccm ni wanafiki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kubali au kataa kwa hili wengi wa wabunge wa ccm ni wanafiki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JUST, Jul 20, 2011.

 1. JUST

  JUST JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Ndugu wana jf ni faraja kwa wabunge kwa pamoja bila kujali chama wakionekana kusimama kwa pamoja kwenye mambo ya msingi ya nchi lakini kwa hili la nishati na madini ni ukweli usiopingika kwamba wabunge wamesimamia swala la umeme kidete kwa sababu kukosekana kwa umeme kumewaathiri wao pia kwasababu wengi wanayo miradi inayotumia nishati ya umeme ambapo kwa hali ya sasa na wao gharama zimekuwa kubwa kiasi cha kuwapunguzia faida walizokuwa wanapata na kawmwe si kwa masilahi ya mtanzania wa hali ya chini.

  Ni ukweli usiofichika kuwa hakuna mbunge asiyeweza kununua na kuendesha gharama za umeme utokanao na jenereta kwa mujibu wa mshahara wanaopata kwa mwezi. Kwa haya ni wazi wameathirika kiuchumi ndio maana wamekuja juu.

  Kama kweli wabunge wetu hawa wanaO uchungu ni kwAnini hawakusimama kidete wakati ule nyalandu anatoa hoja ya misamaa ya kodi ambayo kimsingi itawanyonya watanzania bali waliamua kuwakejeli wabunge wengine waliopinga misamaha hiyo, jibu ni rahisi sana sababu na wao watapata nafasi ya kuwekeza na kufaidika na kodi.

  Ni ukweli usiopingika kuwa wabunge wote wangesimama kidete kukataa posho ni dhahiri ngeleja angepata pesa za kununua majeneretor ya kuzalisha umeme

  kwa hayo machache ni sinema iliyotokana na mgao mdogo aliotoa ndugu jairo wa bilioni moja ambapo wengi hawakutarajia kwani alitakiwa atoe zaidi ya hizo.

  Nawakilisha
   
Loading...