Kubali ama kataa, ukweli ni kwamba kwa hapa Tanzania mtu asiyejua Kiingereza hajaelimika

Kuna mwamba mmoja alikuwa anaumwa... Nikamuuliza " what r u suffering from" akanijibu 'Town'..

Nilichukua dakika 2 kumuelewa.. aisee nilipofika nyumbani nilicheka kama chizi.

Najua hata nyie hapa hamtaelewa kirahisi.
 
Yote kwa yote lugha hii waTZ inatutesa sana. Labda kizazi hiki cha English Medium kitakuja tufutia aibu.

Imagine Rais anasoma tu mahotuba...hata mambo ambayo inabidi aongee yeye live..anasoma. sio poa.
 
Kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya kuelimika na kujua kiingereza hapa nchini kwetu. Kwasabb lugha yetu ya kufundishia ni kiingereza.

Hivyo ili mtu aweze kuipata elimu kwa kiwango kikubwa lazima aifahamu vema lugha ya kiingereza maana ndiyo iliyobeba taarifa zote zinazotakiwa na mwanafunzi. Kama mwanafunzi atakuwa hajui kiingereza ni dhahiri.kwamba kuna kitu atakikosa.

Wachina, wajapani na warusi wanatumia lugha zao kufundishia ndiyo maana wao kiingereza hakina umuhimu kwenye kuelimika.

Baba wa taifa JK alikifahamu vema kiingereza ndiyo maana aliweza kukitumia kupigania Uhuru wa nchi yetu bila bunduki. Alikuwa na ushawishi kwa wazungu.

Jiwe ndiye aliyekuwa na uelewa mdogo kuliko marais wote waliopita ktk taifa hili. Hakuna alichokuwa anakifahamu zaidi ya ubabe. Maana kwenye maisha yake alichojifunza na kukielewa vema ni ubabe wa kuswaga ng'ombe.
Kwa kiasi fulani alituswaga kwa kweli, kama ng'ombe, ukiwa mkaidi, unachinjwa!
 
Watanzania wengi wamesoma hadi form four lakini Kingereza za mawasiliano hawakijui hasa waliosoma shule za serikali ni majanga. Wachache sana wanakijua hasa wale waliosoma English medium na private schools.

Kwahiyo kwa mada yako hii jiandae kupingwa kwa nguvu zote! But ukweli usemwe, huwezi kuelewa content kwa kiwango kizuri halafu lugha inayotumika kukupa hiyo content huijui vizuri, haya ni maajabu yanayopatikana Tanzania tu.
Huijui vizuri kwenye upande gani?

Maana tatizo kubwa la watanzania ni kushindwa kuongea na kuandika vizuri ila wapo wengi wenye kujua kusoma kiingereza na wakaelewa na pia wanaweza kusikia kiingereza na kuelewa, sasa hayo ya kutoweza kuongea vizuri yana sababu zake na ndio maana wapo watu wanaandika kiingereza vizuri na wamekariri mi grammar kushinda muingireza ila kiingereza cha kuongea ni shida hawezi kuongea vizuri.

Jaribuni kuangalia hivi vitu msitoe tu majibu ya jumla jumla.
 
Shida ya sisi watanzania sio kwamba sehemu ya ubongo kuhusu kiingereza imepooza. La hasha. Shida ni kuwa practice wapi unafanya. Kila ukigeuka kila mtu anaongea Kiswahili.
Sasa utamudu vipi lugha kama inapita miezi 6 au 12 hujaongea na mtu.
 
Kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya kuelimika na kujua kiingereza hapa nchini kwetu. Kwasabb lugha yetu ya kufundishia ni kiingereza.

Hivyo ili mtu aweze kuipata elimu kwa kiwango kikubwa lazima aifahamu vema lugha ya kiingereza maana ndiyo iliyobeba taarifa zote zinazotakiwa na mwanafunzi. Kama mwanafunzi atakuwa hajui kiingereza ni dhahiri.kwamba kuna kitu atakikosa.

Wachina, wajapani na warusi wanatumia lugha zao kufundishia ndiyo maana wao kiingereza hakina umuhimu kwenye kuelimika.

Baba wa taifa JK alikifahamu vema kiingereza ndiyo maana aliweza kukitumia kupigania Uhuru wa nchi yetu bila bunduki. Alikuwa na ushawishi kwa wazungu.

Jiwe ndiye aliyekuwa na uelewa mdogo kuliko marais wote waliopita ktk taifa hili. Hakuna alichokuwa anakifahamu zaidi ya ubabe. Maana kwenye maisha yake alichojifunza na kukielewa vema ni ubabe wa kuswaga ng'ombe.
Kuendelea kupiga bomu montuar ni kupoteza silaha za bure.

Pambana na walio hai.
 
Kuendelea kupiga bomu montuar ni kupoteza silaha za bure.

Pambana na walio hai.
Kijeshi inapigwa tu!! Mortually inaweza tumika km maficho ya adui!......hatuwezikudharau mortually department! labda km huna akili
 
Back
Top Bottom