Kubadilishwa kwa Uongozi ndani ya kikosi cha Simba

The real Daniel

JF-Expert Member
Jan 5, 2017
2,117
7,817
Nafikiri kwa hizi mechi 2 tumethibitisha kwamba uongozi ndani ya kikosi cha Simba umebadilika
First captain: Bocco
Second captain: Chama
Third captain: Kapombe

Ingawa haijathibitishwa na Uongozi wa simba
 
Mfa maji hakosi kutapatapa ndicho wanachopitia sasa mikia na Nov 7 tunawapigilia msumari wa moto wa inch 3.
 
Kiujumla molari imeshuka ktk team

Hata tunapofunga goli huoni wachezaji wakishangilia kama zamani, zaman tulikuwa na uchu kwelikweli, tunaufata mpira wavuni na kuupeleka kati hivi sasa sion hiyo hali.

Kasi yetu uwanjani imepungua sio kama msimu uliopita,

Sitoshangaa msimu huu tukiukosa ubingwa.

Unaona bocco anavokosa magoli ya wazi kabisa

Tunapiga pasi nyingi nusu ya uwanja kurudi nyuma kitu ambacho kinapungusa kasi uwanjani,

Lile goli alilofunga Ndemla ndio style yetu sasa, pasi tatu mko golini.
 
Tatizo kocha wetu kishingo anakariri wachezaji hivyo ushindani wa namba umepungua siamini Kahata aliyekuwa kwenye fomu uwezo umepungua, Shabalala hata afanye madudu gani bado ataanza, timu ameijenga kwa kumtegemea Chama kiasi asipokuwepo hamna kitu.
Ushindi wa simba ni juhudi binafsi za wachezaji kuliko uwezo wa kocha
 
Nakubaliana na ww.
Hii timu tusitegemee makubwa msimu huu

Usajili wa mihemko Kumleta BM ambaye hadi sasa sijaona impact yoyote zaidi ya kuanguka anguka uwanjani hana stamina kabisa kupiga wenzie makonzi hadi kupata adhabu. Kahata ni muhimu kuliko BM,
 
Nyoni kaisha kabisa hata kama umri umeenda
Ajibu akipewa nafasi haitumii vile inavotakiwa
Bocco ndo huyo nafasi tano za kufunga anapata moja
Kagere + Mugalu majeraha yanawasumbua sana
 
Tuwaachie viongozi wanajua.
Kikubwa timu ifanye vizuri ,lengo letu NI moja Haina haja kurumbana yeyote Yule NI captain wetu.
 
Back
Top Bottom