Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 12,434
- 19,452
Part One
Title: KUBADILISHA MFUMO WA ELIMU ILI KUPATA SHULE ZINAZOJITEGEMEA NA KUJIENDESHA KWA FAIDA BILA KUTEGEMEA KARO, VILEVILE KUZALISHA WAHITIMU WENYE UJUZI WA MAZINGIRA YAO NA UHAKIKA WA KIPATO
Utangulizi
Kuna jambo halipo sawa kwenye mukstabali wa Elimu yetu nchini pamoja na dunia kwa ujumla. Vijana wengi wanaohitimu wanakosa ajira hivyo kutokuwa msaada kwa jamii yao, kama hio haitoshi wastani wa mtu kuja kupata ajira au kuanza kazi kwa manufaa yake na ya jamii ni zaidi ya miaka 20. Hapo ni baada ya kusoma chekechea, kuanza la kwanza akiwa na miaka sita na kumaliza la saba akiwa na miaka 12, ukiongeza miaka minne ya sekondari na mingine miwili hapo utaona kwamba elimu ya sekondariTitle: KUBADILISHA MFUMO WA ELIMU ILI KUPATA SHULE ZINAZOJITEGEMEA NA KUJIENDESHA KWA FAIDA BILA KUTEGEMEA KARO, VILEVILE KUZALISHA WAHITIMU WENYE UJUZI WA MAZINGIRA YAO NA UHAKIKA WA KIPATO
Utangulizi
atamaliza akiwa na miaka 18 au zaidi na hapo chuo bado kinamsubiri.
Masomo yanayofundishwa sio tu hayaendi sambamba na uhitaji wa soko la ajira na uzalishaji bali kuna tasnia kama michezo na sanaa inaonekana kama ni burudani hivyo hayapewi kipaumbele katika mitaala.
Kama hio haitoshi elimu imekuwa ghali sana, na ni moja ya matumizi yenye gharama katika familia kuliko mahitaji mengine. Yaani familia inagharamika sana hata kuingia katika umasikini ili kuwatafutia ufunguo wa maisha watoto wao, ila mwisho wa siku kujikuta ufunguo huo hauna msaada katika maisha ya huyo kijana zaidi ya madeni kwa kijana na jamii kukosa nguvu kazi kwa kutokunufaika na ujuzi wa kijana huyo, manufaa ambayo yangepatikana iwapo huyo kijana angepatiwa mafunzo yanayohitajika katika jamii.
Kwenye andiko hili muandishi amejitahidi kuonyesha njia mbadala ambazo zitahakikisha yafuatayo: -
- Kuhakikisha gharama ya Elimu inakuwa rafiki kwa kila mzazi kuweza kumudu na wale wasio na uwezo wanapata ujuzi kwa manufaa ya Taifa la kesho.
- Kuhakikisha Shule zinajiendesha zenyewe kwa kutokutegemea karo, ruzuku au michango ya wazazi.
- Kuhakikisha shule sio tu zinafundisha bali zinazalisha na katika uzalishaji huo wanafunzi wanapata ujuzi unaoendena na mazingira yao.
- Badala ya wanafunzi kulipa na kuondoka na madeni wakihitimu, kuwepo na mfumo ambao kijana akihitimu anakuwa na kianzio cha pesa cha kumuwezesha kupata elimu ya juu au kwa wale wanaoanza maisha kuweza kujikimu. Yaani kama vile mzee anavyopata kiinua mgongo akistaafu, kijana huyu anapata kilainisha mgongo kabla ya kuingia mtaani.
Andiko hili linatambua fika umuhimu wa elimu kama nguzo ya jamii na badala ya elimu kuwa chanzo cha umasikini wa familia kwa kuingia kwenye madeni ili kusomesha watoto wao, tunahitaji kurudi kwenye reli ili Elimu ifanye kile kilichokusudiwa nacho ni kumuwezesha binadamu kupambana na kuyamudu mazingira yake.
Ni ukweli usiopingika ustawi wa jamii na ongezeko la uchumi halitegemei mali asili, mitaji na teknolojia pekee bali idadi na ubora wa nguvukazi pia.
Andiko hili lina sehemu kubwa mbili ya kwanza ni kuelezea jinsi ya kubadilisha mfumo wa shule uwe wa kujitegemea na kuzalisha wahimu wenye ujuzi na tija, na sehemu ya pili itaelezea jinsi ya kutatua changamoto zinazoikumba elimu ya sasa. Baadhi ya changamoto hizo
ni: -
- Ukosefu wa Mitaji kwa Mashule na Gharama Kubwa ya Kusomesha kwa Wazazi.
- Elimu kutoenda sambamba na mfumo wa ajira, au uzalishaji
- Mfumo wa Elimu unaochukua muda mrefu kabla ya Wahitimu kupata fursa ya kuanza kazi na kuzalisha.
- Mitaala kutotoa kipaumbele kwa baadhi ya mafunzo kama Sanaa na Michezo, hivyo taifa kupoteza vipaji.
- Kipimo cha ufaulu kinaangalia ufaulu wa mitihani na sio vigezo vingine jambo linalowatenga watu wenye Uwezo tofauti ambao hauwezi kupimwa kwa mitihani ya darasani.
- Wanafunzi kutokujifunza vitu wanavyopenda bali masomo ambayo watapata chuo kizuri au kazi yenye mshahara mkubwa.
- Elimu inahamasisha mashindano ya nani kapata maksi nzuri zaidi na sio uelewa.
- Ualimu sio Wito tena bali kazi ya kujipatia Kipato, wengi wanafundisha sio kwa mapenzi bali njia ya kujikimu kimaisha.
- Wanafunzi kujifunza ili kupata Kazi na sio Kujifunza ili kuongeza Uelewa, au Kujifunza wanachopenda ili kutimiza ndoto zao.
- Elimu inafundisha kukariri badala ya kukuza fikra na tabia ya kuhoji
ITAENDELEA...