Kubadilisha Marais & vyama vingi ndio sababu pekee ya kukua kwa uchumi wa Tanzania

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,108
18,326
Pamoja na mambo mazuri mengi ambayo Mwalimu Nyerere aliyeyafanya ambayo pengine hayatakuja sahaulika hata kizaizi na kizaizi lakini Tanzania imerudi nyumba sana kipindi cha Mwalimu Nyerere kutokana na kukaa muda mrefu madarakani. Laiti kama Nyerere angeachia madaraka mapema na kuruhusu vyama vingi kama Katibu wa KANU bwana Kambona alivyo pendekeza ,Tanzania ingekua nchi mfano Africa.

Mfumo wa kubadiri viongozi huleta mawazo mapya na ari ya maendeleo kwa viongozi kwa sababu kila mmoja atataka kuacha legacy kwenye nchi yake. Hili linajidhihirisha baada ya kila Rais kuja na jambo la marekebisho toka Nyerere alipo achia madaraka.

Nchi nyingi za Africa zimeshindwa kupata maendeleo kwa sababu ya viongozi kukaa muda mrefu madarakani hadi kufikia kazi kubwa Urais ni kulinda kibarua chao.

Tanzania inaweza kwenda kwa kasi Zaidi kama itapunguza muda wa Urais kutoka Miaka 5 hadi 4 na kuimarisha vitengo vya uandaaji na usimamizi wa sera za Taifa. Rais asiwe mtu wa kupanga sera bali awe ni msimamizi wa maono ya taifa.

Kuongeza muda wa Urais ni kuto kukubali mawazo mapya na kuamini katika udhaifu na ujinga. Moja ya siri kubwa ya Marekani ni uwezo wake wa kutafuta mtu ambaye anaweza fanyia kazi maono na sera za nchi na sio mtu ambaye ataleta maono yake na sera zake.

Cheo cha Urais kinatakiwa kiwe ni cheo cha kufanikisha utekelezaji na usimamizi na sio uwekaji wa sera au maono.

Tanzania imesha toka kwenye umaskini wa kutupwa , hii yote ni baada ya kukubali kubadirisha viongozi hata kama viongozi wote wanatoka chama kimoja lakini tumeona tofauti yao katika utendaji na kila mmoja ameacha legacy tofauti kabisa.

Tanzania itakimbia Zaidi kimaendeleo pale itakapo kuwa tayari kuwa na ushindani wa kweli na kukubali vyama vyote vya siasa view na haki sawa ya kuleta maendeleo katika nchi hii maana hadi sasa kuna ushindani ndani ya chama kimoja hata kama vyama vya siasa vimeleta changamoto kubwa sana kimaendeleo.

Hivyo tukipunguza muda wa Urais na kuimarisha uandaaji wa sera Tanzania inaweza ikawa nchi bora Duniani.

Kwa hiyo siri ya maendeleo ya Tanzania ni mabadiliko ya uongozi, n ahata aliyeko madarakani aamini kwamba atakaye kuja atafanya vizuri kuliko yeye, hivyo ni vema kuheshimu katiba. Pia vyombo vya dola kama TISS na Police wanatakiwa kujua wamefanyika sehemu ya kurudisha nyumba maendeleo ya nchi hii kwa kukiuka matakwa ya uanzishwaji wake kikatiba kwa kuendelea kuwa sehemu ya chama cha Mapinduzi.

Tanzania sasa inashikilia nafasi ya 10 africa kwa GDP $62Bil lakini tungekua mbali Zaidi kutokana na utulivu wa nchi na resources zilizopo.

Ifike wakati vyombo hivi view sehemu ya mapinduzi ya kiuchumi katika taifa letu.

Mungu mbariki Rais Magufuli na wote Marais wote waliotangulia

Mungu wabariki watanzania wote

Tanzania Oyeeeeee..
 
Uko sawa. Nakubaliana na wewe. Ila marais wengine ndio hawa wakina Mbowe na Lissu? Utani huu.
 
Kama kunanushindani wa kweli kama hawafai hawata pita.. kinacho hitaji ni fare competetion.
Uko sawa. Nakubaliana na wewe. Ila marais wengine ndio hawa wakina Mbowe na Lissu? Utani huu.
 
Watu tofauti , mawazo tofauti kila mmona ana jambo jema kwa nchi hii
FB_IMG_1592041138305.jpeg
FB_IMG_1592041145927.jpeg
FB_IMG_1592041135650.jpeg
FB_IMG_1592041132312.jpeg
 
Vyama vingi ni kielelexo chankukubali mawazo mapya na ushindani wenye tija
FB_IMG_1592041160454.jpeg
 
Vyombo vya dola vitanakiwa kusimamia taifa lama taifa moja bila kubagua wala kupendelea.
FB_IMG_1592041176520.jpeg
 
Back
Top Bottom