Kubadili matumizi ya kiwanja kama hakuna mlalamikaji na kero ziko wazi kwanini serikali iruhusu?

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
Wana JF.

Kumekuwepo ubadirishwaji holela ya matumizi ya viwanja kutoka makazi na kuwa kitu kingine. Rai yangu ni kwamba wakati wa kuweka tangazo wengine ambao ni majirani wanakuwa hawapo labda wewe umewahi kujenga kabla yao.

Wakija kujenga ndio wanakuta kero hiyo. Mfano. Makanisa ya kilokole yanajengwa hivyo, kumbi za starehe. Apartment, shule za awali na gereji.

Wizara ilikuwa ikitoa vibari vya kubadili matumizi ili ali wizara iliona yenyewe kuwa panafaa kwa kilichokusudiwa kama makazi si vinginevyo. Lakini kwa sababu za kibiashara inakubaliana na mbadiri matumizi kufanya uharibufu wa mazingira.

Wizara kwa nini isishauri mtu auze yabaki makazi huyu mtu atafute palipopangiwa shughuli kama hizo!.

Serikali kupitia bwana ardhi Ikae ikijua sio wote wanaoona matangazo ya kubadili matumizi, pią sio wote watakaoharibu ujirani mwema kwa ajiri ya kuweka pingamizi bali i ikatae maombi haya na kuwashauri wanunue panapofaa.
 
Back
Top Bottom