Fahamu utaratibu na gharama za kubadili jina la mmiliki wa kadi ya gari ni kiasi gani TRA?

Document wanazohitaji ni:

1. Mkataba wa kuuzina chombo cha moto.

2. Nakala ya kitambulisho cha mpiga kura/Leseni ya udereva/Pasi ya kusafiria au kitambulisho cha Taifa. Nakala hiyo iwe imeambatishwa na pasipoti ndogo na kuwa certified na Wakili. Hii inahusu pande zote mbili (Mnunuzi na Mnunuaji).

3. Muuzaji anapaswa kulipa 1% ya kiasi alichouza chombo cha moto.

4. Mnunuzi atalipia gharama ya kuhamisha umiliki Bank kiasi cha 50,000/- (kama ni gari) kama kama ni pikipiki atalipa 27,000/-. Pia, mnunuzi a talipia 10,000/- Bank kama gharama ya kadi.

5. Polisi unalipia 5,000/- kwa magari madogo na 10,000/- kwa magari makubwa ikiwa ni gharama ya kukagua gari.
6. Kuwe na kiapo cha Umiliki.

7. Nambari ya Mlipakodi (TIN Number).
 
Document wanazohitaji ni
1. Mkataba wa kuuzina chombo cha moto
2. Nakala ya kitambulisho cha mpiga kura/Leseni ya udereva/Pasi ya kusafiria au kitambulisho cha Taifa. Nakala hiyo iwe imeambatishwa na pasipoti ndogo na kuwa certified na Wakili...
Mkuu ahsante sana. Umefafanua vizuri sana. Kwa hali ya sasa,suala la kununua Double Used Japanese Car ni tangible. Naposema Double Used naamanisha lilikua used Japan,likauzwa na sasa unamvua Mtanzania.
Tunapitia sana njia hiyo kwa sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Document wanazohitaji ni
1. Mkataba wa kuuzina chombo cha moto
2. Nakala ya kitambulisho cha mpiga kura/Leseni ya udereva/Pasi ya kusafiria au kitambulisho cha Taifa. Nakala hiyo iwe imeambatishwa na pasipoti ndogo na kuwa certified na Wakili. Hii inahusu pande zote mbili (Mnunuzi na Mnunuaji)...
Nashukuru wana jf kwa darasa zuri nimeelimika vyakutosha
 
Sijapata shida yoyote since 2017 naitumia..sioni njia ya kuifanya nibadili kadi kwa kukosa hivo viambatanishi.
Naitumia hii gari nikiichoka naichinja..
Hivi polisi wanapokakaguaga gari wakaangalia hadi hadi kadi huwa hawalingainishi majina yaliyopo kwenye kadi na kwenye leseni? Nini hasa lengo lao la kuomba kadi?
 
Back
Top Bottom