Kubadili dollar kwa pesa ya tanzania

naona mkuu unatega kuku kwa kurusha mahindi mdogo mdogo hadi aingie chumbani...
unipeleke dubai tufanye shoping ya dolari!!!!!!
leo unauliza kuchange dollar,kesho uje uulizie spare za range ,kesho kutwa kodi ya ghorofa mbezi ...eheheee
 
Kuna BUY SELL
e.g. US$ 1620 1650

BUY, Hii ina maana wao (e.g Bureau de change/Bank) wana nunua US dollar kwa Tshs 1620/=, hivyo basi una wapa US $1 wanakupa Tshs 1620/=. SELL hii ina maana wao (e.g. Bureau de Change/ Bank) wanauza US dollar kwa mtu mwenye kuhitaji US dollar kama wewe unawapa Tshs 1650/= wanakupa US dollar 1. Mfano una Tshs 10,000,000/= za kununua Toyota IST; Tshs10M/1650 US $=6060.6060606 US$. Hivi viwango nimevikadiria tu japo hubadilika mara kwa mara ndani ya siku 1 au baada ya siku moja au kadhaa. Ukifika pale Bureau De Change wewe utahusika na SELL PRICE, achana na buy kwa mtu mwenye hitaji kama lako na kinyume chake ni sawa pia (kwa mtu mwenye hitaji tofauti na lako/kuuza US$).


ILA MADA YAKO UMEPOST KWENYE JUKWAA LA MAHUSIANO/MAPENZI-URAFIKI BADALA LA BIASHARA/UCHUMI. Kwa namna moja au nyingine naweza ungana na Smile.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom