Kubadili Dini kwa Ajili ya Ndoa

Jack HD

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
852
1,154
Amani iwe juu yenu!!

Wapenzi wengi wamejikuta kwenye mtihani wa kupendana na wenza wao ilhali imani za dini zao huwa zipo tofauti. Jambo ambalo siku zote nimekuwa nikiliamini ili mtu awe na familia iliyo bora lazima nyumba iwe na imani madhubuti. Kuwepo kwa imani mbili ni kugawa watoto na hata imani watakayoifuata baadae mara nyingi huwa hawaitendei haki ipasavyo.

Nakubali kuwa kuna familia nyingi ambazo zipo huku wazazi wakiwa na imani zao tofauti. Binafsi yangu huwa naona hili halipo sawa kabisa. Sijui wadau mnalisemeaje hili?
 
Dini huwa ni kikwazo kikubwa kwa baadhi ya watu wenye msimamo wa dini zao... Wapo ambao hufikia kuvunja uhusiano sababu ya kikwazo cha dini.

Linapokuja suala la kubadili dini ni uamuzi wa mtu, wapo wanaokubali na wapo wanaokataa!!! Mungu tunaemwamini ni mmoja lakini kila mtu ana uhuru wa kuamua mwenyewe dini anayotaka!!!
 
Kama umeridhia na huwezi jutia ni saw tu maana Mwenyezi Mungu tunae muabudu ni mmoja

Mkuu;
Umetoa ushauri mzuri sana ila ukamalizia vibaya. Nakubaliana nawe kuwa, kama mkiridhiana kuwa pamoja regardless ya imani zenu hapo sawa tu. Lakini ninachokataa ni kule kutuaminisha kuwa mungu tunaye muabudu ni mmoja. Hata siku moja usiniambie kuwa Allah Subuhannah Wa Taallah ati ni sawa na huyo wa wagalatia. Hapanaaaaa. Tena usiwachokoze watu wake. Tena akija kwangu hamalizi mwezi kabla sijamsilimisha.
 
Dini huwa ni kikwazo kikubwa kwa baadhi ya watu wenye msimamo wa dini zao... Wapo ambao hufikia kuvunja uhusiano sababu ya kikwazo cha dini.

Linapokuja suala la kubadili dini ni uamuzi wa mtu, wapo wanaokubali na wapo wanaokataa!!! Mungu tunaemwamini ni mmoja lakini kila mtu ana uhuru wa kuamua mwenyewe dini anayotaka!!!
Do you think baada ya kuanzisha familia mambo yatakwenda vizuri na kila mtu akatumikia imani yake vizuri? vipi watoto watafuata wapi?
 
Mkuu;
Umetoa ushauri mzuri sana ila ukamalizia vibaya. Nakubaliana nawe kuwa, kama mkiridhiana kuwa pamoja regardless ya imani zenu hapo sawa tu. Lakini ninachokataa ni kule kutuaminisha kuwa mungu tunaye muabudu ni mmoja. Hata siku moja usiniambie kuwa Allah Subuhannah Wa Taallah ati ni sawa na huyo wa wagalatia. Hapanaaaaa. Tena usiwachokoze watu wake. Tena akija kwangu hamalizi mwezi kabla sijamsilimisha.
Sawa mkuu unaweza kuwa sahihi au kinyume chake
 
Do you think baada ya kuanzisha familia mambo yatakwenda vizuri na kila mtu akatumikia imani yake vizuri? vipi watoto watafuata wapi?
Nafikiri hujanielewa, uhuru wa kuamini dini unayo itaka haiingii kwenye ndoa kwa upande wangu, nimezungumzia walio kwenye uhusiano tuu. Lakini Linapokuja swala la ndoa lazima wote muwe kitu kimoja sababu ya watoto na kuwa na familia moja imara.

Ukiwa kwenye uhusiano na mtu mwenye Imani tofauti ya kidini ni lazima mmoja akubali kubadili dini
 
Ukiwa kwenye uhusiano na mtu mwenye Imani tofauti ya kidini ni lazima mmoja akubali kubadili dini
Kwa hiyo unasaliti imani yako kwa ajili ya mahusiano ya kimapenzi. Is this right pia??
 
Sio sababu ya mapenzi tuu sababu ya ndoa na familia yangu ninayoenda ianza. Kwangu mie ni sawa maana naamini Mungu ni mmoja ila dini ndo tofauti!!!
ila kwa KE inaonekana hili jambo sio gumu sana
 
ila kwa KE inaonekana hili jambo sio gumu sana
Anayebadili dini kisa tu ndoa ndio mnaweza tengeneza familia nzur mwanzoni ila mmoja wapo akifa bac aliyebadili dini kunauwezekano mkubwa sana wa kurud kweny dini yake hususan wanawake na kufanya watoto wataabike

Raha mtu abadili dini kwa hiyari yake bila sababu ya ndoa bac hapo mtajenga familia nzuri zaidi
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom