Kuapishwa kwa majaji Ikulu: CAG mbele ya Rais Magufuli, akanusha Shilingi trilioni 1.5 kuibwa/kupotea

Mungu Ibariki Tanzania,
Wabariki Viongozi Wake,
Wabariki Wananchi Wake,
Dumisha Amani na Umoja,
Milele Hata Milele,
Amina.
 
Kuapishwa kwa majaji wapya Ikulu: Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali(CAG) mbele ya Rais Magufuli akanusha Tanzania shilingi 1.5 Trilioni kuibwa wala kupotea.

Majaji wapya walioapishwa mbali ya kuhimizwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma, wametakiwa kuzisoma na kuzitafsiri vyema sheria kwani kama watafanya vinginevyo wanaweza kuipoteza nchi.

Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili kwa Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela amewaambia majaji hao leo Ijumaa Aprili 20 Ikulu kuwa kazi waliyopewa inahitaji umakini na uadilifu.

“Someni sheria na kuzitafsiri vizuri… Mahakama ndiyo chombo pekee kinachotafsiri sheria na kama mtatafsiri vibaya mnaweza kuipoteza nchi,” amesema jaji huyo wakati akitoa nasaha zake baada ya majaji hao wapya kuapishwa na Rais John Magufuli.

Alisisitiza kuwa katika utendaji wa kazi kumekuwa na mgawanyiko wa majukumu wakati Bunge likitunga sheria, Serikali kazi yake kubwa ni kupendekeza sheria hizo.

“Mahakama ndiyo inayotoa tafsiri hivyo ili kuifanya vyema kazi hiyo lazima mtapaswa kusoma sana na someni kwa makini maana kile mnachokiamua nyinyi ndiyo mwongozo wa mwisho mpaka pale Bunge litakapoamua kutunga sheria nyingine,” amesema.

Kuhusu kuishi kwa uadilifu kamishna huyo aliwataka majaji hao kujichunguza mienendo mibovu itakayoweza kuwaondoelea heshima kwa jamii

“Chagueni vyema marafiki zenu ikiwezekana achaneni na wale wanaoonekana kutokuwa wema… na ikiwezekana ukitoka zao kazini nenda nyumbani na siku kama ya leo Ijumaa nenda msikitini kwa wale Waislamu na wale Wakristo nendeni kanisani Jumapili … mnaweza kwenda pia kwenye burudani lakini angalieni burudani mnazokwenda,” amesema.

Rais Magufuli leo amewaapisha majaji wapya kumi, wakili mkuu wa serikali na naibu wake na naibu mkurugenzi wa mashtaka.

Sherehe za kuwaapisha majaji hao zinafanyika Ikulu na zinahudhuriwa na wageni mbalimbali akiwamo Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi na Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma.


Rais Magufuli akiwa Ikulu katika hafla hiyo ya kuwaapisha majaji 10 anasema aliposikia kwenye mitandao kuwa Serikali inatuhumiwa kuiba/kupoteza kiasi cha Trilioni 1.5 alimpigia simu CAG kumuuliza kwanini alimficha kuhusu wizi wa kiasi hicho cha fedha alipomsomea Ripoti hiyo Ikulu ili awafukuze wahusika?

Anasema alimwambia CAG kuwa amepitia ripoti yake yote lakini hakuona ilipoibiwa Shilingi trilioni 1.5, CAG akamjibu Rais kuwa hakuna hela iliyoibiwa. Rais akasema ni kawaida ya watu kuandika uwongo kwenye mitandao na kuwaaminisha watu kwa sababu wana uhuru.

Rais anasisitiza angemfukuza mhusika hata angekuwa Waziri siku hiyohiyo kama angeona upotevu wa kiasi hicho cha fedha.

Rais anamuuliza CAG ukumbini hapo na anajibu " Hakuna kitu kama hiko Mheshimiwa Rais". Pia anamuuliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha naye anasimama na kusema " Hakuna kitu kama hicho"

Rais anasema DPP, Solicitor General, Deputy DPP na majaji washughulikie kesi kama hiyo haraka.

Rais amewataka majaji kutafuta njia ya kuwashaghulikia watu wanaojifanya ni wasemaji wao hasa ambao wanapigania maslahi yao(Tanganyika Law Society) kwani wana lengo la kuwachonganisha naye.

"Mnisaidie tu kwa hawa wanaojituma au mnawatuma kuwa wasemaji wenu kwa sababu wananichonganisha na ninyi. Kwa sababu nashindwa kutofautisha wanajituma au mnawatuma. Na kama wanajituma ninyi ni wanasheria tumieni uwezo wenu"

Rais Magufuli aliongeza pia kuwa Watanzania tunaamini kila kinachoandikwa kwenye mitandao ya kijamii na hiyo inatokana na kutokudhibiti mitandao hiyo. "Sidhani kama ukienda kwenye nchi kama China kama wana 'Google' na 'WhatsApp' kama hizi za kwetu"




Wiki iliyopita, Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alihojiwa na kituo cha Azam Tv kuhusu fedha kutoidhiniswa na Bunge na kutoonekana zimetumika wapi na kusema Bunge linapaswa kuhoji kuhusu fedha hizo


Faru john mwizi unafikiri mlipoambiwa amemchagua mpwa kuwa ppaymaster general hamkuelewa lengo la huyu jambazi mnyanganyi wa silaha<
 
Hiyo ni sawasawa na mtu anayetumia ARV hauwezi kuzuia ukimwi najua watajitahidi kuficha ukweli kwa style mbalimbali lakini mwisho wa siku wataumbuka tuuu!!!!
Ukweli huu hawawezi kuuficha kabsa kutokana na idadi kubwa ya watanzania kuzinduka hawana imani tena na CCM na serikali yake, wananchi wanaamini hizo pesa Trillion 1.5 zimetumika kununua ndege, kukomboa ndege Canada, kujenga Chato Airport, kuwanunua wabunge, madiwani na wanachama wa upinzani, kurudia chaguzi kwa gharama kubwa, kufanyia uchakachuaji, kuwabambikia kesi, kuwapiga Risasi, kuwafunga jela Wapinzani na unyama mwingi ikiwemo hii ya kuwalipa kafulila na Cyprian msiba watengeneze Uzushi na Propaganda za kishamba shamba.
 
IMG_20180421_082732.jpg
 
Jawabu ni pesa imepigwa na Mtukufu malaika toka chato kwa kushirikiana na Naibu Rais Maliyamungu Bashite ambaye ni master plan wa Dili zote za kula pesa za Umma kwa kisingizio cha kuzitumia kudidimiza chadema, kuua CUF na kudhoofisha upinzani kwa ujumla, mladi wa kurejesha mfumo wa chama kimoja ni mladi mkubwa sana unatafuna pesa za Umma kama mchwa.
 
Utawala wa sasa unatumia katiba ya marehemu idd Amin Dada wa Uganda, kipindi kile ambapo Maliyamungu na idd Amin walikuwa wakichota pesa Hazina ya uganda kienyeji na Gavana alipokataa aliuawa, lakini Tanzania gavana alipokataa wamemtoa wakaweka Gavana wao ambaye anawapa Pesa toka BOT mda wowote hata saa nane Usiku wakitaka, ni Aibu na fedheha kwa Taifa kuendelea kufucha upotevu wa Trillion 1.5 kipindi hiki ambacho watanzania wameamka wanajua kila maigizo ya CCM na serikali yake.
 
Mh Raisi nakwamumkia kwa jina la Baba Muumba mbingu na Dunia.

niseme ukweli Jana nilikuwa miongoni mwa watanzania walio fatilia hotuba yako ya pongezi kwa majaji kumi ulio wateua

nilikusikia kwa umakini ukikemea mitandao ya kijamii.

nilijiwa na pcha moja kuwa ulichukizwa na ile clip ya kiongozi wa ACT wazalendo ambayo inakemea watanzania wabadili mwelekeo dhidi ya utawala wako clip ambayo Zitto kabwe anasema wazi tusipo kuwa makini utawala wako utaifili Tanzania.

kuwa muwazi mimi naiona ile clip ila bira maelezo ya kina kutoka kwa Zitto sitoamini kwa asilimia 60%tu kuwa utawala wako hautalifilisi taifa

Asilimia 40%nitaamini endapo ntapatiwa majibu murwa kutoka utawa wako ukiipinga kauli ya Ziito kabwe.

sina lengo la kujadili mambo hayo ya mitandaoni.

nikakuomba unirihusu niohoji................. nmekumbuka mjadara wa kifo cha Akwilina umefungwa je tunaruhusiwa kuhoji DPP akishafunga mjadara k
shitaka?
 
IMG_5866.JPG


niliandika hapa kua CAG atakuja kukana kwamba hazijaibwa uzi ulifutwa sasa haya yametokea rudishen uz wangu
 
Mkuu huyu jamaa kakutana na nyumbu nyingi ingekuwa nchi kama South Africa tayali asinge kuwapo siyo ombi ni lazma.

Nchi gani huruhusiwi kuhoji ila ruhusa ni kusifia tuu?
 
Tumeona namna serikali inavyo pambana kujibu hoja za CAG zilizoweza kuchambuliwa kwa ufasaha na mbunge wa Kigoma kaskazini ZZK! Rais wetu JPM amejingengea heshima ndani na nje ya nchi kwa vita dhidi ya rushwa na ufisadi, kauli ya jana ya rais kujaribu kujibu juu ya tuhuma za rushwa za serikali yake zimeanza kuondoa na kutia mashaka juu ya heshima aliyoijenga juu ya vita ya ufisadi,tumeona kwa muda mrefu rais akihubir elimu ya uzalendo kwa watz, je kwa yanayo endelea anaweza kuwa na moral authority ya kuendelea kukemea rushwa? Hili ni doa kwa serikali iwe kuna wizi ama la, lkn bado serikali haijaweza kuja na kauli kamilifu inayoweza kujibu maswali na shauku ya watz juu ya 1.5trillion! Siyo rais, polepole, kafulila ama naibu wazir wa fedha au yeyote aliyeweza kuja majibu timilifu kujibu hoja za CAG...
Mamlaka zinazohusikia huenda zikaja na majawabu kuliko personal attacks
 
Tumeona namna serikali inavyo pambana kujibu hoja za CAG zilizoweza kuchambuliwa kwa ufasaha na mbunge wa Kigoma kaskazini ZZK! Rais wetu JPM amejingengea heshima ndani na nje ya nchi kwa vita dhidi ya rushwa na ufisadi, kauli ya jana ya rais kujaribu kujibu juu ya tuhuma za rushwa za serikali yake zimeanza kuondoa na kutia mashaka juu ya heshima aliyoijenga juu ya vita ya ufisadi,tumeona kwa muda mrefu rais akihubir elimu ya uzalendo kwa watz, je kwa yanayo endelea anaweza kuwa na moral authority ya kuendelea kukemea rushwa? Hili ni doa kwa serikali iwe kuna wizi ama la, lkn bado serikali haijaweza kuja na kauli kamilifu inayoweza kujibu maswali na shauku ya watz juu ya 1.5trillion! Siyo rais, polepole, kafulila ama naibu wazir wa fedha au yeyote aliyeweza kuja majibu timilifu kujibu hoja za CAG...
Mamlaka zinazohusikia huenda zikaja na majawabu kuliko personal attacks

Rais Mstaafu Kikwete nae alipojibu ' Hoja ' hivi hivi juu ya Sakata zima la ' Escrow ' pia ulipatwa na ' Hofu ' au ni kwa Rais a sasa tu Dr. Magufuli ndiyo unaipata hiyo ' taharuki ' Mkuu?
 
Hahahaha Magufuli ni kiboko yani ukirusha nchale yeye ana rusha bomu kabisa ....acheki na kima...Mmezoea mpotoshe watu.wanyamaze

Safi sana JPM..
 
Rais Mstaafu Kikwete nae alipojibu ' Hoja ' hivi hivi juu ya Sakata zima la ' Escrow ' pia ulipatwa na ' Hofu ' au ni kwa Rais a sasa tu Dr. Magufuli ndiyo unaipata hiyo ' taharuki ' Mkuu?

Mkuu soma vizur nilichosema, sifa moja wapo ya awamu ya tano ni vita ya rushwa na ufisadi na kuhubiri dhana ya kuwa na uzalendo,kwa hili JPM aliweza kupambana nalo tofauti na watangulizi wake, hofu yangu ni hili la 1.5 trillion limeanza kutia doa record nzuri ya rais wetu, yaani mpambanaji wa rushwa aanze kunyoshewa kidole ama kuhusishwa na taarifa za ufisadi mimi naona haijakaa vizuri inanipa hofu kubwa
 
Back
Top Bottom