Kuapisha viongozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuapisha viongozi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaFalsafa1, Sep 28, 2009.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Nimekaa na kufikiria kitu. Nchi yetu tunasema ni secular na dini na serikali havi fungamani. Tunasema serikali haina dini lakini watu ndani ya serikali wana dini. Swali langu linakuja kama ni hivyo kwa nini viongozi wetu wengi huapa kwa kutumia vitabu vya kidini? Kwa nini wanaapa mbele ya Mungu wao lakini bado serikali yetu tunasema hakuna dini? Sijui kwa upande wa Uislamu ila kwa upande wa Wakristo najua kuapa ni dhambi kwa hiyo kwa nini viongozi wa Kikristo wana apa? Na wakati wa kiapo hapo wanaapa kwa Mungu, wananchi au kwa wote? Kama viongozi bado wanaapa kwa Mungu wao wamuaminio na bado huvunja hizo ahadi ni kwa vipi sisi wananchi tuna tegemea wata timiza ahadi zao kwetu? Labda ni mimi tu lakini hapa naona kuna walakini fulani.
   
 2. O

  Omseza Mkulu Member

  #2
  Sep 28, 2009
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mkuu, tatizo kubwa hapa lipo ktk fikra zako..!
  Hakuna walakini wowote kama unavyo fikiria wewe.
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  nadhani Mkuu mwanaFA unachanganya mambo kidogo. KUna tofauti kati ya dini na Mungu. Serikali haina dini, lakini hata yenyewe inasema kuwa watu wake wana dini. Kutokuwa na dini hakumaanishi kuwa serikali au watu wake hwaamini kuwepo kwa Mungu. Nduio maana wakati wa kuapa wanaapa kwa Mungu na si kwa dini ingawa wanaapa kulingana na dini zao.
  Halafu suala la kuapa kuwani dhambo wa wakristo, umelitoa wapi hili Mkuu? Au kwenye ile amri inayosema usilitaje bure jina la bwana Mungu wako?
  kama ni hiyo, angalia vema kwa maana andiko nadhani linasena USIJIAPIZE, ikimaanisha kuwa usijichukulie uaminifu kwa kutaja jina la Mungu kwa kitu ambacho si cvha kweli, jambo ambalo ni tofauti na kuapa kwa namna inayotumika kwa viongozi wetu.
   
 4. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #4
  Sep 28, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Serikali haina dini haina maana kwamba serikali haitambui uwepo wa dini hizo. Inazitambua kwamba zipo, na ndiyo maana inazisajili dini hizo na kuziachie uhuru wa kuabudu na kujitangaza. Serikali haina dini (secular state) ina maana kwamba serikali au dola haikumbatii dini yoyote katika nchi. Mfano wa serikali kuwa na dini ni kama vile Irani ambako dini ya serikali (dola) ni Uislamu. Ndiyo rasmi. Serikali yetu haina dini rasmi. Kumbe inazitambua dini zote zilizopo lakini shughuli zake ziko nje ya shughuli za uendeshaji wa serikali.

  Kumbe Serikali ikitambua uwepo wa dini na uwepo wa watu wanaozifuata dini hizo, inatoa fursa ya washika madaraka wa dini hizo kuapa kwa kutumia misahafu ya dini zao: kuahidi kufanya kazi kwa uadilifu kama Mungu anavyotaka kwa faida ya Taifa. Anaposhindwa kuishi kadiri ya kiapo chake basi dhamiri yake inamsuta kwani anakuwa ameshindwa kutimiza kiapo chake kwa Mungu.
   
 5. G

  Gongagonga Member

  #5
  Sep 29, 2009
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 25
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Bora wawe wanaapa kwa kushika katiba tu
   
Loading...