Kuanzishwa kwa " un- women" - kaeni mkao kwa kula! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuanzishwa kwa " un- women" - kaeni mkao kwa kula!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WomanOfSubstance, Jul 16, 2010.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Katika tukio la kihistoria tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa 1945, UNGASS ( Baraza kuu la Umoja wa Mataifa) kwa kauli moja tarehe 2/7/2010, walipitisha na kuanzisha chombo kipya au Taasis ya kuharakisha maendeleo ya wanawake na wasichana duniani. Taasis hii itakayojulikana kama “UN WOMEN” -Kiingereza – “WANAWAKE – UM” kwa kiswahili au UNO - FEMME -Kifaransa ni matokeo ya mchakato wa miaka mingi wa majadiliano baina ya nchi wanachama na pia ushawishi wa wanaharakati wa haki za wanawake.

  Vile vile ni sehemu ya mabadiliko katika Umoja wa Mataifa katika kuunganisha rasilimali na mandates za taasisi na mashirika mbalimbali ya UN ili kuleta mashiko au mafanikio zaidi.
  UN Women itaziunganisha taasis 4 za UN zenye kushughulikia maswala ya wanawake – DAW, INSTRAW, OSAGI, na UNIFEM ili kupata taasis moja madhubuti.


  Sasa hii ina maana gani kwa watanzania? Kutakuwa na fursa mbalimbali – ajira, na mipango ya maendeleo.Lakini hizi hazitakuja kwenye sahani ya dhahabu.Kutakuwa na ushindani. Serikali inaweza kufanya lobbying ili kufikiriwa kwa wanawake wa Kitanzania katika nafasi za juu hasa ile ya USG lakini mwisho wa siku hao wanawake watakaopendekezwa watatakiwa kushindana na wengine duniani.Kuna majina strong sana kutoka nchi za Latin AmerIca, wapo pia kutoka nchi nyingine za Africa na bila kusahau nchi za Scandinavia.Hivyo hakuna mteremko.


  Ukiacha ngazi za juu, kutakuwa na fursa katika ngazi za nchi - ina maana kwamba watanzania - wanawake na wanaume wataweza kutafuta fursa hizo kwenye nchi mbalimbali duniani, mradi wawe vigilant kutafuta fursa hizo kwa kuangalia matangazo kwenye websites mbalimbali za UN. Pia nchini mwetu ofisi ya UN Women itaimarishwa na kutoa fursa ........

  Kina GS, MJ1, Nyamayao na wengineo kaeni mkao wa kula....
  Pia kina kaka msijivunge.
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Jul 16, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  HOngereni sana kina mama; ila tatizo la Umoja wa Mataifa wa Sasa hivi ulivyo una matatizo gani yanapokuja masuala ya wanawake?
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Jul 16, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Girl power....

  I'm all for it
   
 4. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2010
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  hivi baada ya kutimiza hili suala la gender equality then nini kitatokea? kuna kila dalili za kuanzishwa 'UN-MEN' ....
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Jul 16, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Halafu baada ya hapo nini? UN-gay men and UN-lesbuns (note: lesbians)?
   
 6. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2010
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Then kina Semanya aka 2 in 1
   
 7. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2010
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,125
  Likes Received: 23,734
  Trophy Points: 280
  Wewe Mkaruka acha hizo!.
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  Jul 16, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Now, that will be madness...
   
 9. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  INTERESTING !
  AMF - Zipo harakati towards that end...sic
   
 10. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2010
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Na ukichukulia hao jamaa wa jinsia moja walivyo na nguvu za pesa na wameweza kupenya kwenye 'makanisa' yaliyoamua 'ku-amend' biblia kinyemera .....tutegemee kuona mengi. sipati picha!
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Jul 16, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Habari Leo

  MBUNGE wa Viti Maalumu, Janet Kahama (CCM), ameiomba serikali kufanya ushawishi kwa Umoja wa Mataifa ili Mtanzania ateuliwe kuongoza chombo kipya kitakachoshughulikia masuala ya wanawake na jinsia.

  Kahama alitoa ombi hilo jana wakati alipoulizwa swali la nyongeza kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, katika swali lake la msingi kuhusu hatua zilizofikiwa katika uundaji wa chombo hicho.

  Baada ya kufahamishwa kuhusu uundwaji wa chombo hicho kinachoitwa 'UN Women', Kahama aliomba serikali kufanya ushawishi huo ili Mtanzania ateuliwe kuongoza chombo hicho atakayesimamia atakuwa na wadhifa wa Katibu Mkuu Msaidizi wa UN.

  Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Seif Ali Iddi, alisema UN ina utaratibu wake wa uteuzi, na Tanzania ingependa kupata heshima hiyo, lakini inasubiri uamuzi wa UN.

  Alisema serikali imepokea ombi la mbunge huyo na italifanyia kazi, lakini kwa sasa ieleweke kuwa Katibu Mkuu wa UN ndiye mwenye kufanya uteuzi kwa kushirikiana na vyombo vya maamuzi vya umoja huo.

  Awali, akijibu swali la Kahama, Naibu Waziri alisema uteuzi wa msimamizi wa chombo hicho haujafanyika.

  "Hivyo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amemwomba Naibu wake, Mheshimiwa Dk. Asha-Rose Migiro asimamie chombo hiki kipya hadi uteuzi utakapofanyika," alisema Naibu Waziri Balozi Iddi.

  Kwa mujibu wa Azimio Namba A/63/311 la UN, Baraza Kuu la UN liliazimia kuunga mkono kwa dhati uunganishwaji wa taasisi za Ofisi ya Mshauri wa Masuala ya Jinsia na

  Maendeleo ya Wanawake (OSAGI), Divisheni ya Maendeleo ya Wanawake (UNDAW), Mfuko wa UN wa Maendeleo ya Wanawake (UNIFEM) na Chuo cha Kimataifa cha Tafiti na Mafunzo kwa Maendeleo ya Wanawake (INSTRAW), kuwa chombo kimoja cha kuunganisha majukumu ya sasa ya taasisi hizo.

  My Take:
  Asante WoS, maana ningesoma hii habari tu sidhani kama ningeelewa ni nini umetupa perspective nzuri.
   
 12. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #12
  Jul 16, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  [FONT=&quot]KIREFU CHA TAASIS NILIZOTAJA:[/FONT]
  [FONT=&quot]DAW = [FONT=&quot]Division for the Advancement of Women – ilianzishwa 1946 na ni sehemu ya ECOSOC[/FONT][/FONT]
  [FONT=&quot]INSTRAW =International Research and Training Institute for the Advancement of Women ilianzishwa 1976[/FONT]
  [FONT=&quot]OSAGI - Office of the Special Adviser on Gender Issues and Advancement of Women ilianzishwa 1997[/FONT]
  [FONT=&quot]UNIFEM -United Nations Development Fund for Women ilianzishwa 1976[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
   
 13. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #13
  Jul 16, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,938
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Sasa hii inaitwa UN WOMEN na hawa akina kaka wa nini tena hapa? Pia umetumia nene 'vigilant', je wajua maana yake halisi?
   
 14. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #14
  Jul 16, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Mhh!
  Umeniacha nashangaa! Ina maana hukuelewa kilichoandikwa au huna habari kabisa na trends katika development management! Pia umeniuliza kama najua maana ya neno ( umeita nene) "VIGILANT".Nitakujibu kwa kifupi kama ifuatavyo japo nasikia hata uvivu kukujibu.
  VIGILANT - ni neno la kiingereza likimaanisha - watchful, alert, on your guard etc.... au na haya nayo utataka nikufafanulie?Kwa maneno mengine, nilichotaka kusema ni kuwa watu wawe macho, wasilale, wasibweteke, vinginevyo watakuta fursa zote zimekwisha waanze kulalama kama kawaida ya watanzania wengi.
   
 15. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #15
  Jul 16, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Kula tena? WoS mbona unaniangusha? Mimi nilidhani nia ni kuhudumia na kuwatumikia wanawake wenzenu na sio kuwatumia kama ngazi! Badala ya kukimbilia vyeo kama wakina Janet wanavyotaka, muanze kwa kuangalia namna gani chombo hicho kitamsaidia mwanamke mtanzania wa kawaida. hadi hivi sasa wanawake wa kitanzania wako over representented Umoja wa mataifa. Asha Rose Migiro, Anna Tibaijuka na Amina Salum Ali wote wana nafasi za juu huko Umoja wa Mataifa ( Ms. Ali akiwa balozi wa A.U Umoja wa Mataifa) si rahisi kupewa nafasi nyingine. Jiulizeni hao waliopo wamewasaidia vipi kabla ya kukimbilia kunawa mikono!

  Amandla.........

   
 16. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #16
  Jul 16, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  MKUU FM...
  MIMI naamini katika kuwa mkweli and pragmatic. Kuna pande mbili za shilingi:
  1. Huwezi kuokoa bila kujiokoa mwenyewe kwanza. Ina maana mimi kama mwanamke siamini kuwa wanawake wanapaswa kuwa philanthropists wa dunia. Tutafanya kazi tukiwa well remunerated ili tuwe fully committed kutekeleza majukumu yetu. Huwezi kunitegemea mimi nitoe huduma bure ati kwa vile nashughulika na maswala ya wanawake ilhali wanaoshughulikia maswala ya wakimbizi, watoto, wazee, wasiojiweza, usalama na amani, mazingira, idadi ya watu nk. wote wanalipwa vizuri mno.
  2. Haya maswala ya wanawake ni specialized kama taaluma nyingine zozote.Tuheshimu taaluma hii na tusifikiri kuwa ni rahisi kivile.Tutofautishe siasa na professional jobs.Kwenye siasa wengi hujifanya wanataka kusaidia wananchi au kundi fulani maalum.

  Asante kwa kunielewa...
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Jul 16, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Aaah Fundi na wewe vipi bana...kwani hujui kuwa mkao wa kula ni tamathali ya usemi?
   
 18. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #18
  Jul 16, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mkuu WoS,

  Bahati mbaya kwangu mimi neno "kula" ndilo linalonitatiza. Unakuwaje well remunerated kama haujazilisha? Hili suala la kutanguliza remuneration nzuri kabla hatujaonyesha uwezo wetu naamini ndiko kwa kiasi kikubwa kilichotufikisha hapa. Wengine hata kunawa hatutaki! Ukweli ni kuwa kama committment yako inajali zaidi remuneration yako basi public servbice si mahala pake. Na U.N. ni Public Service, ingawa imekuwa abused.

  Mimi sidharau profession. Ninachotofautisha ni Public na Private service. Hata siku moja sitamsema mtu kama akitanguliza kula katika Private sector. Public sector ni tofauti.

  Wanawake hawawezi kuwa philanthropists wa dunia maana hawana cha kutoa. Sehemu kubwa ya wanawake duniani ni maskini ukilinganishwa na wanaume. Wanahitaji msaada wenu ( na wetu) na committment bila kwanza kuangalia Moi!

  Bado tumetofautiana, Mkuu.

  Amandla.......
   
 19. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #19
  Jul 16, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Nyani, si hivyo. Watu wanafanya kweli wanapokaa mkao wa KULA!

  Amandla......
   
 20. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #20
  Jul 16, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Mkuu, narudi tena... na si vibaya tukakubaliana kutokukubaliana...ni kitu cha kawaida katika michakato mbalimbali. Kama tukiwa tunakubaliana kila kitu kila wakati basi kuna uwezekano kuwa kuna mtu hafikiri.
  Neno "KULA" usilichukulie kivile kama unavyofanya... ni msemo tu nilioutumia loosely kunogesha mjadala.

  Nikirudi kwenye point yangu... bado nasisitiza tuweke kando misemo ya " kusaidia" linapokuja swala la gender/jinsia na wanawake. Sidhani tunatumia dhana hii tunapowazungumzia watendaji wenye kushughulika na maswala mengine ya maendeleo. Fikiria kuna mambo kama mazingira, UKIMWI, nk. Kote huku kunatakiwa interventions kwa kutumia wataalamu waliobobea. Sidhani tunawataka hawa wataalamu wajitolee! Ndio sikatai kuwa kuna kujitolea to some extent, but the danger of depending on volunteerism ni kushindwa kuwawajibisha wahusika. Hapa mimi nazungumzia utendaji wa kitaalam kwenye programming na operations. Unahitaji wataalamu kufanya upembuzi na kupanga mipango nk. Wataalamu hawa wanafanya kazi ili waweze kujikimu wao na familia zao. Watu wamesoma na kujinoa kwenye maeneo fulani ili wajiajiri au waajiwe na siyo kwenda kufanya kazi za kujitolea!Vinginevyo wataalamu katika kila fani wangefanya basi kazi za bure kitu ambacho hakiwezekani!

  UN ni public service na siyo private japo inategemea pia private sector for goods na pia services hasa za wataalamu ( consultants ) na hawa siyo bei rahisi nadhani unafahamu. Unahitaji top- notch experts to give u top of the range products.Hata serikali sasa hivi katika private- public partnership wanafanya hivi.
  Nadhani nimejitahidi kuweka point yangu ieleweke.EXPERTS SHOULD SELL THEIR EXPERTISE AND ITS THEIR RIGHT TO DO SO.

  NB: THERE IS NO FREE LUNCH.... THE ONLY FREE LUNCH IS THE PIECE OF CHEESE ON A MOUSE-TRAP - Na hii nayo ina gharama kubwa.
   
Loading...