GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,548
- 108,859
Ifike muda sasa tujifunze kuheshimu misiba na hasa wale ambao tunawaomboleza ili kuonyesha kwamba kweli tumeumia na kuondoka Kwao hapa duniani na tuache hizi tabia za ' Kipuuzi ' za kila mara kupenda kutumia misiba kama sehemu yetu ya Kujiimarisha na kupata Sifa Kisiasa.
Chama kipya cha ' MboKa ' Alliance hakiwezi kuwa na baraka kama kimeanzishiwa Msibani sana sana tu kinaweza kikajikuta kinapata ' laana ' ambayo itakiangamiza zaidi.
Kwahiyo mnataka kutuambia kwamba bila Msiba huo kutokea huu Muungano wa ' Kinafiki ' wa ' MboKa ' Alliance usingetokea? Je tukisema labda kwa tamaa zenu za Kisiasa labda nyie ndiyo ' Wachawi ' wenyewe ambao ' mmemroga ' Marehemu ili afe halafu kupitia Msiba wake mjijenge Kisiasa tutakuwa tunakosea?
Siasa bora, njema na zenye mantiki na tija huwa hazianzishwi Misibani bali kuna ' mazingira ' maalum ambayo yanaweza yakachochea Watu kufanya Siasa ila kamwe na hata katika Mila za Kiafrika Misibani ni sehemu ya Kuomboleza tu na kumuombea Marehemu makazi mema huko aendako.
Nawasubiri kwa hamu sana niwaone hao Wanachama wa awali wa Chama kipya nchini Tanzania cha ' MboKa ' Alliance ili nami niweze kujua idadi kamili ya Watu ambao wanaenda kupata ' laana ' ya Kutukuka ya Marehemu Mwalimu ili pengine liwe fundisho kwa ' Wanafiki ' wengine wote wa Kisiasa nchini Tanzania.
Nawasilisha.