Kuanzisha biashara ya diapers na sanitary pads

mojave

JF-Expert Member
Apr 30, 2016
5,587
2,000
Waungwana habari ya leo....?
Bila shaka wengi wetu tu wazima na Mungu katupatia neema ya kuiona siku ya leo na walio wagonjwa Mungu aendelee kuwapigania.

Nakuja kwenu kuomba msaada wa kujua ni wapi naweza kupata hizi bidhaa/ product (diapers and sanitary pads) kwa makampuni mbali mbali kama (huggies, softcare, pampers, slipp bebe, predo adult, HQ pads, Ran n.k)
(a) Kwa ajili ya kuanza biashara ya duka la jumla
(b) Kwa ajili ya kuanza biashara ya duka la reja reja

(a) 1. Naomba kujuzwa viwanda vinavyotengeneza au wakala wanaosambaza hizo bidhaa
2. Pia naomba kujuzwa bei za kiwandani au kwa wakala
(b) 1. Naomba kujua wapi naweza kupata maduka yanayouza hizi bidhaa kwa bei ya jumla
2. Na bei zao zikoje

(c) Naomba kujua bei wanazouza maduka ya reja reja hizo diapers na sanitary pads.
 
The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
17,248
2,000
Hongera na kila la kheri mkuu. Hizo taarifa zote unaweza kuzipata, mie sio mfanya biashara ila sehem unayotaka kufungua biashara au aina ya wateja unaowalenga itaamua aina gani (brand) ipi uende nayo, kuna watu wanajali sana ubora, kwao akina huggies, pampers watahusika. Ila kuna maeneo ukiweka hizo brand hauuzi, wao hawaangalii ubora wala brand. Zingatia hilo.

Watu siku hizi wanaagiza container imejaa huo mzigo tu. Nafikiri inakua nafuu.
 
Shukrani sana mkuu,

Nategemea hili duka la jumla kuliweka sehemu ya jiji, dula la retail nategemea kuliweka pemebeni ya mji hivyo nitazingatia ushauri wako kabla sijafungua nitazungukia maeneo hayo ili kujua wateja wangu wataweza kumudu bidhaa za gharama ipi.

Naomba unifahamishe hapo kwenye kuagiza container, ni kwamba hizi bidhaa hazizalishwi hapa nchini? (binafsi ufahamu wangu kwa hili ni sifuri ndo kimenifanya nije hapa kuomba msaada).

Nifahamishe kwa kina kama hutojali mkuu.
 
Kuna jamaa walikua wanashirikiana wawili su watatu wanaagiza container za pampers na karatasi. Walikua wanaagiza nje, kuhusu kutengenezwa hapa sijajua aina zinazotengenezwa hapa.
 
mojave

JF-Expert Member
Apr 30, 2016
5,587
2,000
Kuna jamaa walikua wanashirikiana wawili su watatu wanaagiza container za pampers na karatasi. Walikua wanaagiza nje, kuhusu kutengenezwa hapa sijajua aina zinazotengenezwa hapa.
Naomba uweze kuniunganisha nao nipate ufahamu wa karibu mkuu kama hutojali maana hata kuagiza mizigo sijawahi hivyo nitaweza kupata elimu nzuri kabla sijaanza ama kuungana nao pakitokea utayari
 
The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
17,248
2,000
Naomba uweze kuniunganisha nao nipate ufahamu wa karibu mkuu kama hutojali maana hata kuagiza mizigo sijawahi hivyo nitaweza kupata elimu nzuri kabla sijaanza ama kuungana nao pakitokea utayari

Ah! Kaka unataka nije kuanzishiwa uzi mkuu? Ntafanya hivyo ila usichukue hatua hadi utakapo jiridhisha kabisa na mchakato mzima unavyoenda. ID yangu naipenda naogopa kuitelekeza
 
Lakini ningekushauri jambo moja mkuu. Ukiweza, vuka maji tembelea Zanzibar. Wanabishaa za aina tofautitofauti kutoka uarabuni, China na ulaya. Na kule bandari hazina urasimu, kodi ndogo, unaweza kujikuta unatoa mzigo hapo Unguja unauleta hapa na unapiga faida ya wastani huku unausoma mchezo wa kuagiza wewe mwenyewe ukishaiva kwenye tasnia.
 
mojave

JF-Expert Member
Apr 30, 2016
5,587
2,000
Lakini ningekushauri jambo moja mkuu. Ukiweza, vuka maji tembelea Zanzibar. Wanabishaa za aina tofautitofauti kutoka uarabuni, China na ulaya. Na kule bandari hazina urasimu, kodi ndogo, unaweza kujikuta unatoa mzigo hapo Unguja unauleta hapa na unapiga faida ya wastani huku unausoma mchezo wa kuagiza wewe mwenyewe ukishaiva kwenye tasnia.
Shukrani mkuu!
 
mojave

JF-Expert Member
Apr 30, 2016
5,587
2,000
Ah! Kaka unataka nije kuanzishiwa uzi mkuu? Ntafanya hivyo ila usichukue hatua hadi utakapo jiridhisha kabisa na mchakato mzima unavyoenda. ID yangu naipenda naogopa kuitelekeza
Uanzishiwe uzi tena kuhusu nini mkuu...?

Nitashukuru kama utaniunganisha nao, suala la tahadhali hilo ondoa shaka niko makini.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom