Kuanzia Mei 2022, Mahakama kuanza kupokea maoni ya wafungwa, mahabusu

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Kuanzia mwezi Mei, 2022, Mahakama itaanza utaratibu maalum wa kupokea maoni kwa wafungwa na mahabusu kwa kutumia mfumo wa dodoso kuhusu mwenendo wa utoaji haki.

Akizungumza jana na waandishi wa habari kuhusu muendelezo wa huduma kwenye kituo cha kupokea maoni ya wateja wa mahakama, Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Prof. Elisante Ole Gabriel, alisema uamuzi huo wameufikia baada ya kuona umuhimu wa makundi hayo kuyapa fursa ya kupokea maoni yao kwa kuwa ni vigumu wao kupiga simu ama kutuma barua pepe.

Alisema kituo hicho sio mbadala wa rufani bali ni cha kiutawala ikiwa ni kumulika mnyororo wa utoaji haki nchini.

“Mara nyingi tunategemea kwamba wale ambao ni wafungwa pengine wasiwe na njia rahisi ya kupiga simu au kutembelea kituo hiki kwa hiyo sasa tumewasiliana na Katibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani na utaratibu unafanywa haraka iwezekanavyo ili kuanzia mwezi ujao tutakuwa na utaratibu maalum tumetengeneza dodoso zuri lenye maswali 10 ambalo litakuwa linapelekwa kule mahabusu na kwa wafungwa ili kupata nafasi ya kutoa mrejesho,” alisema.

Alisema kuwa kituo kinatoa huduma tano ikiwamo suala la mirathi na talaka.

Alisema kituo hicho kina watumishi wabobezi wa kuwapatia huduma sahihi na ushauri kadiri itakavyohitajika.

“Kituo kinatoa huduma kama kuuliza jambo lolote linalohusu upatikanaji wa huduma za kimahakama ikiwepo suala la mirathi na talaka, kupokea mrejesho wa jinsi huduma zetu zinavyokidhi matarajio ya mteja malalamiko kuhusu jambo mahsusi ambalo kiutawala mteja hajaridhika nalo na angependa kufahamu utaratibu wa kulishughulikia,” alisema.

"Kutoa taarifa ya vitendo vyovyote vinavyoashiria ukiukwaji wa kimaadili katika mnyororo wa utoaji huduma ndani ya mahakama."

Alisema mpango huo sio mbadala wa rufani wala njia ya kupingana na maamuzi halali ya kisheria bali ni kuhakikisha haki inatendeka kwa uwazi na mteja anaridhika.


Source: Nipashe
 
Ni njia nzuri ila bado ina ukakasi hili zoezi litasimamiwa na askari magereza sidhan kma watakua na huo muda naona manyapara wakijaza dodoso hlo.
 
Back
Top Bottom