Kuanzia leo Zantel Tsh. 1 kwenda mitandao yote!

Mods peleka hii kitu jukwaa la matangazo,halafu hii promo inatakiwa ilipiwe hapa.
 
Wamezindua huduma mpya inaitwa Epic Moto ambayo mteja atatumia sh. 1 kwa sekunde kupiga kwenda mitando yote nchini. I hope sasa watazoa wateja kwa mtazamo wangu!

Source: TBC1 & ITV Habari.

Update:
• BURE – Haina haja ya usajili wa kila siku
• Piga simu mtandao WOWOTE kwa 1Tsh kwa sekunde masaa 24
• Megabaiti 50 za mtandao bure na• Kiwango cha chini kabisa cha Tsh 25 tu kwa SMS
• Piga simu bure ZANTEL kwenda ZANTEL kuanzia saa 11:00 usiku mpaka saa 6.00 ya asubuhi.
• Punguzo la asilimia 100 kwenye maduka mbalimbali nchini kwa wananchama wa Epiq
• Huduma hizi za Epiq Moto ni bure kabisa kutoka Zantel, hutakatwa kiasi chochote kwa kuzitumia.


Dar es Salaam, 3/5/2012: Zantel, kampuni inayoongoza kwa ubunifu na inayoheshimika zaidi kwa huduma zake za mtandao nchini, imezindua ofa mpya ya kihistoria kuwawezesha wateja wake kufurahia huduma za kiwango cha chini kabisa kuwahi kutokea ambazo zitaibadilisha kabisa sekta ya mawasiliano nchini.


Huduma hii ya Epic Moto!, imeundwa kiupekee kabisa ili kuwapa wateja sio tu thamani ya pesa zao wakati wa kupiga simu, kutuma meseji na kutumia huduma za mtandao, lakini pia kwa mara ya kwanza kabisa Zantel wanapunguza kabisa gharama za mawasiliano za kupiga kwenda mitandao mingine kuwa shilingi 1 tu kwa sekunde, ofa ambayo inaweka historia na kuibadilisha sekta ya mawasiliano nchini.


“Epiq Moto inaenda sambamba na Epiq Bongo Star Search ambayo inawawezesha vijana kuwasiliana na ndugu na marafiki kwenda mitandao yote kwa shilingi moja tu kwa sekunde, kupigiana simu bure kabisa Zantel kwenda Zantel usiku kucha, kupata megabaiti 50 za mtandao bure lakini pia, kupata meseji 25 bure kabisa bila kukatwa meseji wala pesa yoyote’ Anasema Bwana Ahmed Mokhles, Afsa Biashra Mkuu wa Zantel wakati akizindua huduma hiyo mbele ya waandishi wa habari.


“Huduma hizi zote zitaipeleka sekta ya mawasiliano katika ngazi nyingine kabisa, hasa hasa ikiendana na imani yetu hapa Zantel kuwa mawasiliano ni msingi wa maendeleo kwa taifa lolote. Tanzania ni mojawapo ya mataifa ambayo kundi la vijana linakua kwa kasi kabisa barani Afrika. Na hii ni hatua ya kipekee kama kampuni kuchukua hatua madhubuti kuwapa fursa vijana kujiendeleza lakini pia kuwarahishia huduma za mawasiliano’ anasisitiza Mokhles.


Epiq Moto ni moja kati ya huduma za kipekee kutoka Zantel zinazoenda sambamba na Epiq Nation ambayo ilizinduliwa mwaka jana na kuiteka nchi yote kwa kuwafanya vijana wote nchini wajiunge Zantel kupata huduma za kipekee kabisa ambazo Zantel na washirika wake walikuwa wakizitoa kwa wanachama wote wa Epiq Nation kupitia maduka na huduma mbalimbali zaidi ya 100 nchi nzima sambamba na huduma za mtandao wa Ezynet.


Ofa hii pia inaungana na uzinduzi wa Zantel Epiq Bongo Star Search, ambayo pia ni ofa nyingine kutoka Epiq Nation ambayo itawapa fursa vijana wenye vipaji katika sekta ya muziki na mitindo Tanzania kuonyesha vipaji vyao. Epiq Bongo Star Search itazinduliwa tarehe 15 mwezi huu wa sita katika mji wa Dodoma. Zantel inawaomba wateja wake kuzungumza kwa uhuru zaidi na wenzao juu ya Bongo Star Search kwani mawasiliano sasa yamefanywa rahisi na nafuu kwa watu wote.



#Namna ya kujiunga na huduma ya Epiq Moto:Wateja wa Zantel watajiunga kwa kupiga *149*09# kutoka katika laini zao za Zantel. Wateja wapya wa ZANTEL wataunganishwa moja kwa moja kwenye huduma hii ya kihistoria.




#MWISHO#


576556_326146284129052_140380962705586_760657_770965120_n.jpg

Like · · Share

kama ukipenda huduma unajiunga na huduma hiyo kwa kupiga *149*09#.

hv kumbe master j ni sharobaro na anagonga modo za akina diamond, duh mambo ya boy2man
 
...dah! hiyo ofa ya kutwaga bure kuanzia saa 5 usiku ili uifaidi lazima ujifunze tabia ya "popo",wenzio wanapoanza kulala wewe ndo unaamka ...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom