Kuanzia leo Zantel Tsh. 1 kwenda mitandao yote! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuanzia leo Zantel Tsh. 1 kwenda mitandao yote!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Boniface Evarist, Jun 3, 2012.

 1. Boniface Evarist

  Boniface Evarist JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 1,100
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Wamezindua huduma mpya inaitwa Epic Moto ambayo mteja atatumia sh. 1 kwa sekunde kupiga kwenda mitando yote nchini. I hope sasa watazoa wateja kwa mtazamo wangu!

  Source: TBC1 & ITV Habari.

  Update:
  • BURE – Haina haja ya usajili wa kila siku
  • Piga simu mtandao WOWOTE kwa 1Tsh kwa sekunde masaa 24
  • Megabaiti 50 za mtandao bure na• Kiwango cha chini kabisa cha Tsh 25 tu kwa SMS
  • Piga simu bure ZANTEL kwenda ZANTEL kuanzia saa 11:00 usiku mpaka saa 6.00 ya asubuhi.
  • Punguzo la asilimia 100 kwenye maduka mbalimbali nchini kwa wananchama wa Epiq
  • Huduma hizi za Epiq Moto ni bure kabisa kutoka Zantel, hutakatwa kiasi chochote kwa kuzitumia.


  Dar es Salaam, 3/5/2012: Zantel, kampuni inayoongoza kwa ubunifu na inayoheshimika zaidi kwa huduma zake za mtandao nchini, imezindua ofa mpya ya kihistoria kuwawezesha wateja wake kufurahia huduma za kiwango cha chini kabisa kuwahi kutokea ambazo zitaibadilisha kabisa sekta ya mawasiliano nchini.


  Huduma hii ya Epic Moto!, imeundwa kiupekee kabisa ili kuwapa wateja sio tu thamani ya pesa zao wakati wa kupiga simu, kutuma meseji na kutumia huduma za mtandao, lakini pia kwa mara ya kwanza kabisa Zantel wanapunguza kabisa gharama za mawasiliano za kupiga kwenda mitandao mingine kuwa shilingi 1 tu kwa sekunde, ofa ambayo inaweka historia na kuibadilisha sekta ya mawasiliano nchini.


  "Epiq Moto inaenda sambamba na Epiq Bongo Star Search ambayo inawawezesha vijana kuwasiliana na ndugu na marafiki kwenda mitandao yote kwa shilingi moja tu kwa sekunde, kupigiana simu bure kabisa Zantel kwenda Zantel usiku kucha, kupata megabaiti 50 za mtandao bure lakini pia, kupata meseji 25 bure kabisa bila kukatwa meseji wala pesa yoyote' Anasema Bwana Ahmed Mokhles, Afsa Biashra Mkuu wa Zantel wakati akizindua huduma hiyo mbele ya waandishi wa habari.


  "Huduma hizi zote zitaipeleka sekta ya mawasiliano katika ngazi nyingine kabisa, hasa hasa ikiendana na imani yetu hapa Zantel kuwa mawasiliano ni msingi wa maendeleo kwa taifa lolote. Tanzania ni mojawapo ya mataifa ambayo kundi la vijana linakua kwa kasi kabisa barani Afrika. Na hii ni hatua ya kipekee kama kampuni kuchukua hatua madhubuti kuwapa fursa vijana kujiendeleza lakini pia kuwarahishia huduma za mawasiliano' anasisitiza Mokhles.


  Epiq Moto ni moja kati ya huduma za kipekee kutoka Zantel zinazoenda sambamba na Epiq Nation ambayo ilizinduliwa mwaka jana na kuiteka nchi yote kwa kuwafanya vijana wote nchini wajiunge Zantel kupata huduma za kipekee kabisa ambazo Zantel na washirika wake walikuwa wakizitoa kwa wanachama wote wa Epiq Nation kupitia maduka na huduma mbalimbali zaidi ya 100 nchi nzima sambamba na huduma za mtandao wa Ezynet.


  Ofa hii pia inaungana na uzinduzi wa Zantel Epiq Bongo Star Search, ambayo pia ni ofa nyingine kutoka Epiq Nation ambayo itawapa fursa vijana wenye vipaji katika sekta ya muziki na mitindo Tanzania kuonyesha vipaji vyao. Epiq Bongo Star Search itazinduliwa tarehe 15 mwezi huu wa sita katika mji wa Dodoma. Zantel inawaomba wateja wake kuzungumza kwa uhuru zaidi na wenzao juu ya Bongo Star Search kwani mawasiliano sasa yamefanywa rahisi na nafuu kwa watu wote.  #Namna ya kujiunga na huduma ya Epiq Moto:Wateja wa Zantel watajiunga kwa kupiga *149*09# kutoka katika laini zao za Zantel. Wateja wapya wa ZANTEL wataunganishwa moja kwa moja kwenye huduma hii ya kihistoria.
  #MWISHO#


  [​IMG]
  Like · · Share

  kama ukipenda huduma unajiunga na huduma hiyo kwa kupiga *149*09#.
   
 2. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,072
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  hii nmeipenda sana.
   
 3. Boniface Evarist

  Boniface Evarist JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 1,100
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Yaani huku ndo kukombolewa dhidi ya ukoloni! sababu Tz tunaibiwa sana katika mawasiliano
   
 4. mpenda pombe

  mpenda pombe JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,188
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Wow!! Kesho nahamia ZANTEL..
   
 5. R

  Rebel volcano JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yale yale tu
   
 6. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #6
  Jun 3, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Naanza usiku huu kwa majaribio ya siku tatu. Wakizingua naitupilia mbali laini yao.
   
 7. Boniface Evarist

  Boniface Evarist JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 1,100
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  karibu sana Zantel
   
 8. Mshuza2

  Mshuza2 JF-Expert Member

  #8
  Jun 3, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 4,119
  Likes Received: 1,746
  Trophy Points: 280
  Hakuna jipya!
   
 9. Captain22

  Captain22 JF-Expert Member

  #9
  Jun 3, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Dear customer,you have insufficient balance. Your balance needs to be 1000.
   
 10. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #10
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  ngoja niitafute ile line yangu ya zantel sijui kama itakuwa active.
   
 11. Mtu Mzima

  Mtu Mzima JF-Expert Member

  #11
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Habari hapo ni moja tu ya Tsh 1/sekunde ila mbwembwe na maneno meeeengi. Kuchosha wasomaji
   
 12. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #12
  Jun 3, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,377
  Likes Received: 22,242
  Trophy Points: 280
  Tigo bye bye
   
 13. F

  FJM JF-Expert Member

  #13
  Jun 3, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Zantel wana matatizo ya msingi. Mawasiliano ni mazuri ukiwa ukanda wa Pwani yaani Zanzibar, Dar, Bagamoyo kidogo na Tanga. Ukienda Inland kama Dodoma, Mara, Lindi, Arusha, signals ni mbovu kuliko maelezo. Lakini jingine, vouchers kwenye sehemu nyingi (mbali na ukanda wa Pwani) ni tabu. Sijui wanakula mtaji hawa watu au vipi lakini miaka yote hiyo kwa nini mawasiliano ni mabovu nje ya ukanda wa Pwani?

  Halafu haya mambo ya kupeana muda wa bure usiku wa manane wanataka watu wakeshe? Kwa nini wasitoe mchana au kama haiwezekani, punguzeni gharama za maongezi mchana badala ya kutaka watu waongee usiku wa manane?
   
 14. Boniface Evarist

  Boniface Evarist JF-Expert Member

  #14
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 1,100
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Uthititisho
   
 15. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #15
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  jamaa longo longo haziwafikishi kokote...bora wangeweka minimum iwe 500
   
 16. kivyako

  kivyako JF-Expert Member

  #16
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 2, 2012
  Messages: 8,857
  Likes Received: 4,241
  Trophy Points: 280
  Hata wafanye bure kwa mitandao yote, tatizo lao zantel wamekaa kama CUF.
   
 17. Boniface Evarist

  Boniface Evarist JF-Expert Member

  #17
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 1,100
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  wana political bana kila kitu lazima mlete politics!
   
 18. j

  junior05 Senior Member

  #18
  Jun 4, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wanajamii tuongee ukweli,ukiachana na mazoea ya mitandao mingine hakika zantel inajitahi,hii ni ofa nzuri,inavutia na kweli imeonesha kujali mtumiaji wa kawaida wa matumizi ya simu, dah kuna ile ya unlimited nayo ni mwiba mkali sana kuhusu mambo ya internet,
  Hongereni Zantel

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 19. Fekifeki

  Fekifeki JF-Expert Member

  #19
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 1,164
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  baadae ukiwauliza watakujibu ni sh 1/sec bila kodi! hapa hajasema kama kodi imejumlishwa au la! hata hivyo nitajaribu kuhamia ZANTEL!
   
 20. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #20
  Jun 4, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Wachaga bana
   
Loading...