Kuanzia leo Mkora bila cheti hanikamati | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuanzia leo Mkora bila cheti hanikamati

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bikra, Jun 21, 2012.

 1. Bikra

  Bikra Senior Member

  #1
  Jun 21, 2012
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 103
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  [FONT=&quot]LEO wanywa kahawa wamejilawa kweli kweli kutokana na kuwapotukio muhimu kwa kijiwe. Kusema ukweli leo ni siku muhimu na ya kukumbukwakwani ni siku ya kutunukiwa udaktari kwa wanakijiwe uliotolewa na chuo kimojanchini, jina kapuni.

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Samahani kwa kuficha jina la chuo kilichotunikia kijiwe kizimaPhD ni kutokana na kuogopa wapenda udaktari wasifurike kule kughushi. Ilamsomaji ujue kuwa chuo hiki ni genuine na tuliopewa hatujajikomba wala kuhongatupewa shahada hii inayopagawisha wabongoalalalanders na wadanganyika hasawenye nazo na madaraka.

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Kutokana na kupewa shahada za udaktari, madaktari wapya leowatajadili aibu ya Mkora na wasoja kughushi vyeti vya taaluma kama walemawaziri wa Njaa Kaya ambao ameamua kufa nao kutokana na huduma safi ya kuibiakaya wanayompa. Hayo tuyaache. Leo ni sisi na Mkora na Mkora nasi kutokana nawanavyotuhangaisha kwa kutukamata tukiwa tunarejea toka kijiweni ukiachia mbalikuingilia mada zetu kila mara hasa tunapogusa wezi wenye madaraka.

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Kama kawa Dk. Mgosi Machungi analianzisha. “Wagosi, mie sieewihii kaya inapeekwa wapi?”[/FONT]
  [FONT=&quot]Kabla ya kumaliza Dk Mchunguliaji anadandia, “Kwani hujui kuwainapelekwa jehanamu au nalo hili uliongoja kulijua ulipopewe shahada kuu?”[/FONT]
  [FONT=&quot]Dk. Mgosi Machungi hakupenda alivyojibiwa kwa kuonyeshwa kamahajaenda shule. anakula mic kwa hasira, “Daktai Mchunguliaji tiheshimianenisijepiga mtu zongo bure. Nauiza swai ya maana wewe unaanga nkungukwa!”

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Dk. Mchunguliaji anaomba radhi na kikao kinaendelea ambapo piaanakatua mic, “Madaktari watukufu wasomi wa kaya na kijiwe hiki, kwanzanawapongezeni kwa kupewa zana zetu za ulaji hasa huko nje ambako kila mtuanapagawishwa na udaktari. Hata hivyo udaktari tuliopewa si wa kutibu watu.Hivyo jihadharini msijeletewa wagonjwa mkaaibika.”

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Kabla ya kuendelea Dk. Mipawa anakula mic, “Mie nikiletewamgonjwa namtibu. Kwani kazi? Si unamuandikia karatasi kwenda kununua dawakwenye duka la madawa na anakulipa pesa ya kumuona daktari.”

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Kijiwe hakina mbavu kutokana na Dk Mipawa anavyoonyesha makaliyake.

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Tukiwa tunaangua kicheko si Dk. Mbwa Mwitu aliingia akiwa nagazeti la Tanzania Daima. Anasema bila hata kutuamkua, “Jamani waheshimiwa,”Kabla ya kuendelea, Dk Eng. Maneno anadakia na kusema, “Sisi si waheshimiwatena bali madaktari. Omba radhi uendelee kutupa ulilo nalo moyoni.”

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Dk Mbwa Mwitu anaomba radhi na kusema, “Wenzangu nisameheni.mwajua kuwa cheo hiki bado ni kipya hivyo nilisahau. Nisameheni.” Anaendelea,huku akiwa anabwaga gazeti mezani huku kila mtu akiligombea asome kwanza.“Mmeona huu upuuzi unaofanywa na lisirikali na makuwadi wake? Eti Mkora 4,000na masoja 2,000 wamepatikana na kashfa ya kughushi!”

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Dk. Kidevu hangoji hata aendelee, anakatua mic, “Unashangaa la Mkorakughushi wakati mawaziri wameghushi na hakuna anayewashughulikia. Usishangaesiku moja ukiambiwa hata Njaa Kaya alighushi kutokana na elimu na matendo yakekuwa mazabe matupu.”[/FONT]
  [FONT=&quot]Dk. Mpemba hajivungi, anakatua mic, “Siye Pemba tushazoea hayamambo. Mwankumbuka yule komandoo alokuwa akitutesa?” Anakatua kashata nakuendelea, “Yu aitwa daktari wakati hata hicho cheti cha fomu foo hana!”

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Hatuna mbavu tokana na Mpemba anavyokamua lafudhi ya Kipemba.Wakati tukiendelea kucheka, Dk. Eng. Maneno anakamua mic, “Yule jamaa laanatupu. nasikia siku hizi hasikii kabisa.”

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Dk Mpemba anaramba tena mic, “Kweli hasikii tena. hata walewalokuwa wakintumia weshankimbia yu ahangaika kama ndege alonaswa ntegoni. Hizolaana wallahi. Hata hawa waloghushi huku wakikamata wenzao watajalaaniwawallahi.”

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Nami Profesa Dk. Mpayukaji naingilia kati baada ya kukaa mudamrefu. Nakula mic, “Hapa laana siyo hawa wanaoghushi basi mfumo na walewanaowafuga. Kweli kaya imegeuka kaya ya matapeli. Usishangae siku moja kusikiaDk. Koplo Mwita. Dk. Sajenti Chacha. Dk. Afande Ulaji na Dk. Mgambo wa Jiji,Dk. Mpigadebe na Dk. Masaburi, Dk. Mamantilie na kadhalika.”

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Watu hatuna mbavu tena. Profesa Dk. Msomi Mkatatamaa anavaa jezina kuingia uwanjani. Maana kabla mimi na yeye hatujaongea kijiwe huwa kinahisikama hakujafanyika kitu.

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Anakula mic huku akijifuta mdomo baada ya kunywa kahawa yake,“Wapendwa madaktari na wana taaluma wa kweli, kwanza nawapongeza kwa kupatanondo hii muhimu inayowavua nguo watu wengi wenye majina yao.”

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Kabla ya kuendelea anajaribu kufukuza moshi wa sigara kaliunaovurumishwa na Dk. Kidevu ambaye ametoka kubomu kipisi kwa Dk. Mbwa Mwitu.

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Profesa Dk. Msomi anaendelea, “Hapa tusilaumu watu binfsi balijamii hasa kaya nzima. Kama alivyosema profesa Dk Mpayukaji mwenzangu kuwatatizo hapa ni mfumo, pia tatizo ni wana jamii wenyewe wanaokubali kuliwa nakuchakachuliwa kila uchao.”

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Kabla ya kuendelea, Dk. Mgosi Machungi anamkatisha, “ProfesaDaktai Msomi tiombe radhi kwa kusema eti tinaliwa na kuchakachuiwa. Sema waowanachakachuana isipokuwa sisi wazee wa kijiwe. Vinginevyo unatitukana wote.”

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Profesa Dk Msomi anaendelea, “Na iwe hivyo Dk. Mgosi. Sisihatuwezi kuchakachuliwa wala kuliwa. Hamuoni tulivyopata shahada hizi nzitobila umaarufu wowote wala kutembeza pesa. Sisi ndiyo hazina ya ubongo ya kayanzima hata rahisi anajua hili. Hivyo, ninachomaanisha ni kwamba kama wanakayawataendelea kuvumilia uchafu ambapo mtu mchafu anamkamata mtu msafi, watakujakufanyiwa kitu mbaya siku moja wasilalamike.”

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Anavuta kombe lake na kupiga tama mbili na kuendelea, “Kimsingikaya yetu imeingiliwa na mchezo mchafu ambapo wakubwa wamewageuza wanakaya pundawa kubeba upuuzi wao. Kuanzia leo sitaruhusu polisi anikamate au kunihoji bilakuonyesha vyeti vyake. Nina mpango wa kumwandikia rahisi na spika wa Bungebarua waitishe bunge na kutunga sheria inayomtaka kila askari kuwa na vyetivyake kila anapokuwa.”[/FONT]
  [FONT=&quot]Kabla ya kuendelea Dk Mipawa anaingilia kati, “Kaka hilohalitasaidia. utajuaje kama vyeti watakavyokuwa navyo havijakachuliwa? Watuwanachakachua kura washindwe vyeti? Wanachakachua hata noti zetu tena mle mlebanki, washindwe vyeti?”

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Profesa Dk. Msomi anaonekana kukubaliana na hoja ya Dk. Mipawa.Anauliza kwa mshangao, “Sasa tufanyeje?”

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Dk. Mipawa anajibu haraka, “Tufanye kama Uchina. Tukimshika mtuna cheti cha kughushi, au akifanya ufisadi tunanyongelea mbali.”

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Dk. Eng. Maneno anaingilia, “Sasa hapa kaka umegusa pabaya.Utanyongwa wewe. Kambale wote wana ndevu. Naona Mkora wanakuja na mikwara yao.Acha tuwazomee kwa kughushi vyeti.[/FONT]
   
Loading...