Kuanzia leo anaitwaa Mheshimiwa Dr.AMANI ABEID KARUME..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuanzia leo anaitwaa Mheshimiwa Dr.AMANI ABEID KARUME.....

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Engineer Mohamed, May 19, 2008.

 1. E

  Engineer Mohamed JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2008
  Joined: Jul 27, 2007
  Messages: 461
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ktk press conference ilofanyika leo hii hapa IKULU ZANZIBAR,muheshimiwa rais wa zanzibar amesema mengi kuhusu usaniiwa cuf n.k lakini kubwa amesema kuwa ametunukiwa shahada ya heshima ya udaktari na chuo kimoja huko usa.

  JF members......naomba kuanzia leo mheshimiwa rais wa zanzibar tuwe tunamuita Mheshimiwa Dr AMANI ABEID KARUME.
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kuitwa Dr is not an issue hapa .Tueleze usanii wa CUF ni upi ambao yeye kausema .Hili ndili kubwa linatugusa sote na si yeye kuwa doctor ahata akiwa Mganga mkuu sawa .Issue ya CUF tueleze anasemaje .
   
 3. B

  Baba Lao Member

  #3
  May 19, 2008
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 40
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Sasa we engineer na wewe tutakuwa ma mashaka ya u enginner wako.unaleta issue bila facts bwana.Mkuu mwaga facts za huo anaouita usanii huyo daktari wa kununua shahada.kama kuna ukweli wowote tuujadili hapa jamvini
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  May 19, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  well Dr. Karume unaweza kutuambia kwanini Wapemba wako nje ya serikali yako, Mr. Doctor wa Kutununikwa heshima ya juu na Chuo Kikuu kimoja cha Marekani ambako ni Taifa lenye nguvu zaidi duniani na ambalo limetugawia karibu bilioni moja na vyandarua vya kuzua mbu wa Malaria ambao wanaua watoto wetu?
   
 5. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Kapewa na Columbia University,Hivi kuna mtu anyejua huyu jamaa kama alishwahi kusoma Elimu ya chuo,Kumbukumbu zangu ni kwamba alimaliza Form six tu.  Pia kazungumzia suala la kura za maoni,ambapo zitapigwa kura kama za uchaguzi na kusisistiza kasema zitapigwa na Wazanzibar tu.


  Hivi kuna nchi ngapi?Kuna watanganyika??
   
 6. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #6
  May 19, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mzee Mwanakijiji
  wamareakani wana jambo hapa siyo hivi hivi kumpa mtu wa ajabu PHD. na wamemhaidi kumjengea kiwanja cha Ndege pale Zanzibar.sasa sijui kitajengwa upande upi
   
 7. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #7
  May 19, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Huyo Dr. Karume si mwanafunzi wa bachelor of Arts in ..... pale Open University of Tanzania. Ni kitu gani kikubwa alichokifanya mpaka apewe hiyo heshima ya kutunikiwa cheti??????????????
  ama ni Usaniii wa Muafakaaaaa?
   
 8. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #8
  May 19, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135

  NA bado hajamaliza Shule??Duh..
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  May 19, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Jamani ndio maana ya udaktari wa heshima. Hahuusiani na elimu ya mtu. Binafsi sina tatizo kama Chuo Kikuu kinakupa huo wa heshima kuliko hawa wanaotuzuga na Udaktari wao wa hewani.
   
 10. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #10
  May 19, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  na hao wanaotuzuga majina yao haya hapa

  1.Dr. Emmanuel Nchimbi
  2.Dr. Mathayo David Mathayo
  3.Dr Getrude Rwakatare
  4.Dr. Mary Nagu
  5.Dr. Makongoro Mahanga
  6.___________________
  7.___________________
  8.
   
 11. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #11
  May 20, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,703
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Sawa Mkuu! Lakini Columbia University?

  Pili, wenyewe wanaelewa hili? Kuwa hii ni ya heshima na si academic? Na je, mtu anayetunukiwa ana haki ya kujiita Dr.?
   
 12. E

  Engineer Mohamed JF-Expert Member

  #12
  May 20, 2008
  Joined: Jul 27, 2007
  Messages: 461
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  •
  Ili kukaa meza moja...Karume ataka Seif amtambue kwanza

  *Asisitiza kura za maoni ya Muafaka ni lazima

  Na Ali Suleiman, Zanzibar


  RAIS Amani Abeid Karume, ametoa masharti ya kukutana na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, kuhusu Muafaka na kumtaka kwanza amtambue kuwa ni Rais halali aliyechaguliwa kwa kura nyingi kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2005.

  Akizungumza jana na waandishi wa habari Ikulu visiwani hapa baada ya kurudi safari ya Marekani, Rais Karume alisema kimsingi hana matatizo na Maalim Seif kukutana naye na kuzungumzia mustakabili wa kisiasa nchini, lakini amtambue kwanza kuwa ni Rais aliyechaguliwa kwa kura nyingi kuongoza visiwa vya Unguja na Pemba.

  "Milango iko wazi kwa mtu yeyote kukutana nami...hata ninyi waandishi wa habari si mnakuja hapa...lakini masharti ni lazima anitambue mimi kama Rais halali niliyechaguliwa kwa kura nyingi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005," alisema Rais Karume.

  Alisema hilo kutokana na swali aliloulizwa kuhusu moja ya masharti ambayo CUF inayatoa kwa sasa ili kuanza tena kwa mazungumo ya Muafaka wa kisiasa, kati ya vyama hivyo ambao kwa sasa unaonekana wazi kukwama.

  CUF wanataka ili kurudi katika meza ya mazungumzo ya Muafaka, Rais Jakaya Kikwete kwanza aingilie kati na kuwakutanisha Maalim Seif na Rais Karume, hatua ambayo itawezesha mazungumzo hayo kuanza tena baada ya kukwama.

  Mazungumzo ya Muafaka kati ya CUF na CCM kwa sasa yamekwama na juhudi zinafanywa ili viongozi wa pande mbili hizo, warudi kwenye mazungumzo katika hatua za mwisho ili Muafaka huo upate kufanya kazi.

  Rais Karume alisikitishwa na kauli ya CUF ya kupinga kura ya maoni katika suala zima la Muafaka ambapo ni moja ya uamuzi uliofikiwa na Halmashauri Kuu ya CCM kijijini Butiama, Musoma, Mara.

  Alisema kura ya maoni ndio utaratibu mzuri unaokubalika katika kutoa na kusikiliza matatizo ya wananchi kuhusu jambo fulani na kuongeza kwamba si vizuri watu wawili kuwaamuliwa wengi katika jambo kubwa lenye maslahi kwa Taifa.

  "Watu kuulizwa ndio utaratibu unaokubalika duniani kote katika nchi yenye kufuata demokrasia na utawala bora...nawashangaa sana hawa CUF ambao wanajidai kwamba wana nguvu ya umma," alisema Rais Karume na kuongeza kuwa uamuzi wa watu wawili katika jambo la maslahi ya Taifa ni dhima kubwa na ni sawa na udikteta," alisema Rais.

  Alisema kura ya maoni kwa wananchi kuhusu mwelekeo wa kisiasa nchini, itapigwa na si lazima iwe chini ya usimamizi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na kusisitiza kwamba utatafutwa utaratibu mwingine katika kupata maoni ya watu.

  "Hawa CUF wanaogopa nini kwa sasa katika suala la Muafaka...watu kuulizwa katika suala la Muafaka na mwelekeo wa Serikali ya visiwa vya Unguja na Pemba ni lazima, ambapo kisanduku kitatumika katika kupata maoni ya hatma za siasa za Zanzibar.

  CUF hadi sasa inapinga kuhusu mwelekeo wa kuwapo kwa kura ya maoni, kwa sababu mbalimbali ikiwamo kuhofia kuwapo kwa udanganyifu na kuibiwa kura katika suala hilo, wakichukulia uchaguzi mara tatu katika mfumo wa siasa za vyama vingi kura zao ziliibuliwa na CCM.

  Hata hivyo, Rais Karume alisema kura ya maoni kuhusu mustakabali wa siasa za visiwa vya Unguja na Pemba zitapigwa na Wazanzibari wenyewe na hakuna mtu kutoka sehemu nyingine ambaye atapiga kura hiyo.

  Akijibu shutuma za wapinzani kwamba amechagua waziri mmoja tu katika Baraza lake anayetoka Pemba, alisema yeye amechaguliwa na wafuasi wengi wa CCM ambao wanatoka Unguja.

  Rais Karume alisema si sera ya CCM kubagua Wapemba kama inavyodaiwa, lakini yeye amechaguliwa kwa kura nyingi na wafuasi wa CCM ambao wanatoka Unguja, hivyo kwa mujibu wa mfumo uliopo sasa, anatakiwa kuunda Baraza la Mawaziri kwa kutumia wajumbe waliomchagua.

  "Mimi nimepata kura 20,000 tu katika kisiwa cha Pemba...nimechaguliwa kwa kura nyingi ambazo nimepigiwa na watu wa Unguja sasa hawa CUF wanachokilalamikia ni kipi...hapa tunafuata mfumo wa Uingereza, anayepata kura nyingi anaunda Serikali," alisema Rais Karume.

  Aliitaka CUF kuacha chokochoko na maneno ambayo mwelekeo wake ni kuwabagua wananchi wa visiwa hivi sambamba na kupuuza kuwepo kwa vikaratasi vinavyosambazwa vikiwataka wananchi wa Pemba kuondoka Unguja na kusema ni upuuzi mtupu.

  Alisema chokochoko hizo zinazofanywa na baadhi ya watu wachache ambao hawawatakii mema wananchi wa Unguja na Pemba, zinahatarisha amani na utulivu uliopo sasa na kuvitaka vyombo vya habari kulifanyia kazi suala hilo.

  "Nyie waandishi wa habari acheni kuandika habari za uchochezi na kugombanisha wananchi...nyie hamna kinga mnaweza kufikishwa mahakamani....mimi nawachukia sana waandishi wa habari wa aina hiyo," alisema Rais Karume.

  Rais Karume alikutana na waandishi wa habari Ikulu kufuatilia kumalizika kwa ziara yake ya wiki mbili Marekani, ambapo alisema ilikuwa ya mafanikio makubwa katika maeneo mbali mbali ikiwamo elimu na afya.

  Serikali ya Marekani ilimwahidi kutoa misaada zaidi katika mapambano dhidi ya malaria ambapo Zanzibar imepiga hatua kubwa kupitia Mpango wa Malaria wa Rais George Bush wa Marekani.

  http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=6710
   
 13. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #13
  May 20, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Mbona umesahau kutanguliza Dk?
   
 14. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #14
  May 20, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  nilimwona dokta karlume ktk luninga leo, ule mustachi unamuondolea pozi la udokta....
  kuhusu zenji nadhani hata mie namuunga mkono kwa kusisitiza kura ya maoni ili wananchi waamue kama wanataka amani au la! na ninavyowajua wazanzibari watashabikia upuuzi huu na walah watakuwa wametenda dhambi ya kuwatenga wenzao wazenjibarii.

  Na serikali ya muungano inachekelea
   
 15. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #15
  May 20, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280

  Hapana Karume hana ubavu wa kupewa Honoris Causa na Columbia University; pale ni lazime awe amefanya jambo la uhakika kuthibitisha kuwa anastahiki heshima ya namna hiyo. Huyu bwana kapewa honoris causa na chuo kidogo sana cha South Carolina State University; hiki ni Historicaly Black University chenye kufanya vibaya sana katika karibu kila nyanja. Karume ndiye aliyekuwa mgeni wa heshima kwenye mahafali (Commencement) ya chuo hiki ya Spring 2008 (May 9th 2008). Kwa standard za Marekani chuo hiki ni kidogo sana chenye jumla ya wanafunzi wasiofikia hata elfu tano. Hakina uwezo wa kutoa digrii ya Ph.D.; digrii kubwa wanayotoa ni D.Ed (Doctor of Education) tu.

  Angalia Mheshimwa Karume katika pilika za mahafali na SCSU hapa:

  [​IMG]

  [​IMG]

  Kwa babari zaidi bonyeza kongoli hapa:
   
 16. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #16
  May 20, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  shuzi limepata mjambaji
  jiko limepata mpishi
   
 17. E

  Engineer Mohamed JF-Expert Member

  #17
  May 20, 2008
  Joined: Jul 27, 2007
  Messages: 461
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  hongera mheshimiwa Dr Amaan Abeid Karume kutunikiwa shahada ya udaktari Phd.akina mbowe,mwanakijiji na mnyika mpaka leo hata degree hawana.hii inadhihirisha kuwa zanzibar bado inaongozwa na marais wasomi.
   
 18. M

  Mama JF-Expert Member

  #18
  May 20, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  yamekuwa hayo tena, umri unawaruhusu hawa vijana kupata degree halisi na siyo kupata title. Maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua, inakuwa mushkeli kuwasema mwanakijiji na mnyika, je wakikuambia wamepanga hadi wakike 45 or 50 ndio watafute hizo degree na sio kusubiri za kupewa?
   
 19. E

  Engineer Mohamed JF-Expert Member

  #19
  May 20, 2008
  Joined: Jul 27, 2007
  Messages: 461
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  If you must drink and drive, drink milk.
   
 20. M

  Mama JF-Expert Member

  #20
  May 20, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  H20 for the other sake
   
Loading...