Kuanzia Februari 01, 2022 ukinunua bidhaa dai risiti vinginevyo Jela itakuhusu. TRA kuendesha msako mkali sana nchi nzima

Mamlaka ya Mapato TRA imesema itaendesha msako mkali kwa wote wanaouza na kununua bidhaa bila kuwa na risiti.

Msako utaanza rasmi tarehe 01/02/2022.

Mjulishe na mwenzako kama nilivyowajulisha hapa Jf.

Maendeleo hayana vyama!

Tutaendelea tu kukwepa kwa namna yoyote ile. Maana hata tukilipa hiyo kodi kwa moyo, bado mtaishia tu kuiweka mifukoni mwenu, kuichezea kwenye mambo ya hovyo.
 
Sheria ni fursa kwa walinda sheria ndio tatizo la nchi yetu.
Walinda sheria utumia sheria kama sehemu ya kujinufaisha na sio kama kutimiza wajibu.
"Chagua lete laki 7 au twende ofisini ukalipe milioni 3" .
Yaani mlinda sheria anakupa option ipi rahisi kwako.
Ukikamatwa na rushwa unatoa rushwa mambo yanaisha.
Ukipeleka kesi mahakamani ni furaha ya mahakimu umewapelea dili we si umeshindwa kula.
Yaani kila sehemu watz wanakimbiza urefu wa kamba.
 
Pesa zinatapanywa, halafu wanataka kuwasumbua watu.

Kuna mawakili wanakula pesa ya bure kuendesha kesi za kubambikia watu, halafu eti niwe na mori ya kulipa kodi!

Hakika, kila penye uwezekano wa kukwepa kodi, nitafanya hivyo. Hiyo pesa inaweza kutumika vizuri zaidi kwa kuhudumia familia yako au ndugu zako walioko katika shida kuliko kupeleka mahali ambapo inaenda kusaidia uonevu na kusimika mambo ya kishetani. Wale tu ya tozo na nyingine zisizokwepeka.

Siku nchi itakapoongozwa kwa misingi ya haki, huduma zikatolewa kwa haki, pesa ya umma ikatumika kulinda haki na kuhuisha maendeleo ya haki kwa haki na usawa, hapo ndipo kila mwananchi mwenye mapenzi mema na Taifa hili atahamasika kulipa kodi. Tena wananchi tutakuwa tayari kwa pesa za mifukoni mwetu kujenga hata nyumba za polisi. Lakini leo hii usaidie kujenga nyumba za polisi, si itakuwa unashiriki uuaji, utekaji na utesaji wa watu wasio na hatia?
 
Tungeshirikishwa juu ya mipangilio ya matumizi ya kodi zetu zingeenda kwenye vipaumbele vyetu mfano scheme za umwagaliaji,vyuo vya ujuzi kila kata,pembejeo za kilimo,nk.
Na sio vipaumbele vya wanasiasa mfano ikulu mpya, kuhamia dodoma, Chato, kununua ndege,kuwalipa wasiojulikana,kuwalipa wasanii wajaze watu mikutano ya ccm,kuwalipa mapolice wafurumishe mabomu wapinzani,kurudia chaguzi, kununua wapinzani hivi habilitation vipaumbele vya walipa kodi.
 
ufisadi sio kuiba pesa za umma tu. hata kutumia vibaya Kodi na rasilimali za umma ni ufisadi, kwa akili ndogo tu unaweza kujenga ikulu nyingine ya bilioni 500 na ushehe huku wanafunzi wanakosa vyoo na madarasa?
 
Mamlaka ya Mapato TRA imesema itaendesha msako mkali kwa wote wanaouza na kununua bidhaa bila kuwa na risiti.

Msako utaanza rasmi tarehe 01/02/2022.

Mjulishe na mwenzako kama nilivyowajulisha hapa JF.

Maendeleo hayana vyama!
Hao TRA kama walichemka kukamata watu wasio na risiti kipindi cha Magufuli sidhani kama kipindi cha huyu bibi wa kikojani wataweza.
Hivi kuna mmachinga anayetoa risiti?
 
wamrudishe sabaya sir baya mkali wa hizo kazi za task force usipolipa hadi tigo inaliwa bila ky jelly...ila sasa mbuzi wenye kamba fupi watakulaje?
 
Back
Top Bottom