Kuanzia 2015 Tanzania itatawaliwa "kidikteta"! Ukweli huu hapa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuanzia 2015 Tanzania itatawaliwa "kidikteta"! Ukweli huu hapa...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAGAMBA MATATU, May 18, 2012.

 1. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  [​IMG]


  ADOLF HITLER.

  Kwa nini nimeamua kusema hivi? Kuna mambo matano (5) makuu yananilazimisha kusema kuwa:
  "Tanzania itatawaliwa kidikteta"
  Ni vigumu sana kwa mtu asiyeona mbali kunielewa kirahisi na pia ni rahisi sana kwa anayependa demokrasia kunibeza na kuniona kama naota.

  1. Kwanza kuna uwezekano mkubwa Rais ajaye ataingia madarakani kwa utata nikimaanisha kutakuwa na mizengwe katika utoaji wa matokeo kwani hali halisi inajionesha wazi kuwa kuna mvutano mkubwa wa vyama viwili na hakuna kinachokubali kuwa kimeshindwa ki-haki.Endapo mgombea wa chama tawala akashinda basi chama kikuu cha upinzani kitatumia nguvu ya umma ili kupata sapoti wakati aliyejiona kashinda kwa haki atakimbilia ikulu na kushawishi dola kulinda ushindi wake kadri wawezavyo.Tukumbuke yaliyozikumba nchi za :LIBYA, IVORY COAST, LIBERIA, NIGERIA, ZIMBABWE, KENYA, VISIWA VYA COMORO, MISRI na TUNISIA.

  2. Pili ni ahadi atakazozitoa hususani zile za kushughulikia "MAFISADI". Ili kupambana na aliyekuzidi kifedha lazima uchukue fedha zake kwa nguvu hivyo atataifisha mali za waliosemekana ni wahujumu uchumi au mafisadi. Akiwa yupo kwenye hali hiyo lazima watamwinda hivyo itamgharimu kuwa dikteta katika kupambana na mafisadi ikiwa ni pamoja na kunyonga baadhi yao ili kuweka fundisho. Pia atajikuta analipa kisasi cha mateso yote yaliyompata katika harakati za kuingia ikulu.

  3.Suala zima la maendeleo haliendani na kuwapa watu uhuru wa kukaa mijini na kuendeleza masuala kama ya kupiga debe, kutembeza vitu mijini, kuuza na kula madawa ya kulevya, polisi wa barabarani kupokea rushwa, maafisa wa TRA kusamehe kodi na kutoa vibali kwa njia za panya, viongozi wa serikali kutumia ofisi zao kama kampuni zao! Yote haya yatasababisha rais ajaye awe dikteta na mkatili kwa wazembe wote wanaokwamisha matarajio yake, ikiwa ni pamoja na kuwafurutisha vijana wote mijini na kuwafukuza kazi wazembe wote.

  4. Suala zima la ushawishi wa dini, endapo ataegemea dini moja basi atajikuta yupo kwenye wakati mgumu kwani atajikuta amegeuka gafla na kuwa adui wa dini nyingine hivyo kujikuta akichukua maamuzi ya kibabe ili kukabiliana na upinzani kutoka dini fulani. Suala kujiunga na dini ya mashetani au "FREEMASONS" litakuwa jambo la kawaida na watu wengi wenye kupinga serikali watatoweka na wasijulikane wapo wapi.

  5.Ushawishi wa nchi za magharibi; hili nalo ni tatizo ambalo nitafanya nchi isitawalike endapo Rais ajae ataamua kufuata matwakwa ya raia wake kwenye masuala la uwekezaji, ajira, ugawaji wa ardhi, kodi, na utaifishaji wa mali za umma kama viwanda, mashamba makubwa, n.k.na endapo atawageuka wananchi na kusikiliza matakwa ya nchi za magharibi basi atajikuta amepitisha sera ya ndoa za jinsia moja, biashara haramu ya siaha, urutubishaji wa nyuklia. Hali hii itapelekea wanachi waanze kumchukia na atajikuta anatumia nguvu za dola kulazimisha wananchi wakubali sera zake.

  Pia kuna mambo mengine kama kuibuka vyama vya siasa vyenye nguvu vinavyotaka kumtoa madarakani kwa nguvu na atajikuta akiwasweka rumande wapinzani wengi ambapo itachafua hali ya hewa ya nchi. Pia utata wa mgawanyiko wa wabunge maana kuna kila dalili vyama viwili vyenye ushindani kugawana sehemu kubwa ya idadi ya wabunge na hivyo kumlazimisha Rais kuwa na wakati mgumu wa kuvunja bunge zaidi ya mara moja kwenye kipindi cha miaka mitano.

  Pia suala la ajira litaendelea kutesa nchi na ongezeko la wasomi itakuwa pia tatizo hivyo itamlazimu kutumia sheria kali na za kibabe ili kuendesha utawala wake.

  Vyombo mbalimbali vitanyimwa uhuru wa kutoa mawazo yao hii itapelekea vyombo vya habari vya magharibi kumuulika nchi na hivyo hali kuwa mbaya zaidi.

  Swali la kujiuliza, Rais ajaye atakuwa nani ?

  Ni vigumu kupata jibu la moja kwa moja ingawa watu wengi wanatazamia kuona sura mojawapo kati ya hizi:
  .Zito Kabwe,
  .Dr.Willbrod Slaa,

  .Dr.Asha Rose Migiro,
  .Edward Lowassa.
  .Samwel Sitta
  .Prof.Ibrahim Lipumba.
  .Bernad Membe, na
  .John Pombe Magufuli.

  Kwanini Watanzania wengi wanategemea kati ya watu hawa mmoja wapo atakuwa Rais wa Tanzania mwaka 2015?
  Jibu kubwa na la msingi ni suala zima la uwajibikaji na kujituma.

  Kwa nini nasema hivyo?
  Ukiangalia sura zote ni watu wachapa kazi, wanajituma na wenye maamuzi magumu kwa masuala nyeti ya nchi. Ingawa kila mmoja ana mapungufu yake lakini ukweli bado unabaki pale pale wanauwezo mkubwa wa kulifikisha taifa pale Watanzania wanapotaka ikiwa watatekeleza majukumu yao ipasavyo.

  Bado suala la wapinzani kuungana na kumsimamisha mgombea mmoja litakuwa ni ndoto. Kwanza utofauti wa sera na mawazo yao vinakinzana. Pia kuna suala zima la itikadi ya chama na mitazamo. Wapinzani wamejifunza mengi kutoka kwa jirani zao Kenya. Hivyo hawapo tayari kuungana na kuanza kung'ang'aniana madaraka ni bora kila mmoja ashiriki kwa nguvu zake na ashinde kwa nguvu zake.
   
 2. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  Uongozi ni kalama na usataarabu ila ukiona wateule wako wanaenda kinyume na unavyotaka sanasana pale unapohitaji uwajibikaji lazima uapply udiktator..
   
 3. w

  warea JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2012
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu akufumbue macho uone mwanga badala ya giza la udikteta!

  tunapigania utawala wa sheria na haki, na ndio tunawataka watanzania wote pamoja na wewe tuelewe!
  Tanzania ni ya watanzania wote, si ya hao unaowataja! Amka!
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,904
  Trophy Points: 280
  Haya ni mawazo yako , naweza kukuambia kuwa haya unayoyasema baadhi tao yapo sasa hivi , ubabe , kuvunjwa kwa baraza la mawaziri na mengine , free mason kuongelewa na wapuuzi bila sababu za msingi , so hakuna jipya
   
 5. Pendael laizer

  Pendael laizer JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 961
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Umesahau suala la mgombea binafsi.
   
 6. Bra-joe

  Bra-joe JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,559
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  Sikubaliani na wewe, baada ya 2015 kutakuwa na katiba mpaya ambayo haitampa raisi madaraka makubwa na kutakuwa na utawala wa sheria, pia kuwawajibisha wavivu siyo udikteta, swala la mashoga raisi hawezi kuwa na maamuzi nalo kwani litakuwa chini ya mahakama ya katiba kuamua, kumbuka wakati huo mahakama zitakuwa huru, tofauti na sasa.

  Kuhusu kupola mali za mafisadi huenda hasifanye hivyo, badala yake akawasamehe, akaunda tume ya uwazi na ukweli ambayo itawahoji watakaohisiwa walikuwa mafisadi ili wasaidie kuzuia ufisadi usitokee kirahisi.

  Rais ajae atakuwa na kazi ngumu sana, kwani kila idara ya nchi imeoza na hawezi kuwa na nguvu sana kisheria kama alivyo raisi wa sasa.
   
 7. k

  kaguru Member

  #7
  May 18, 2012
  Joined: May 11, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  kwa kweli katiba ipitishe sheria ya mgombea binafsi tuu,hapo ndipo mwanga utakapoonekana ,watanzania tupo kwenye giza neneeeeeee
   
 8. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mkuu MAGAMBA MATATU,

  Nashukuru kwa maoni yako, lakini naomba nikukumbushe kuwa, haya unayoyaandika kama maono yako, yalikuwa yatokee 2010. Katika uchaguzi wa 2010, ccm walitumia kila hila kushinda ule uchaguzi, ccm waiba kura kwa mbinu mbalimbali, kuanzia urais mpaka udiwani. Kwa karama za Mungu, viongozi wa CDM walivumilia huo uchafu wote, ili damu ya mtanzania isimwagike, hata Mh. Dr. Slaa alilizungumzia hili.

  Kwa hiyo, hayo maono yako sidhani kama yanaweza kutokea 2015 kwa sababu, hadi kufika huko ccm itakuwa imeshapoteza mvuto au itakuwa imeshajifia kabisa. Ila swala la CDM kuingia ikulu kwa umwagaji damu, hilo swala halipo...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  kati ya viongozi uliowataja hapo juu sioni hata mmoja anafaa kushika nchi 2015...embu pendekeza majina mengine lasivyo kura yangu itaharibika
   
 10. m

  mkizungo JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 247
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hujamuweka mbowe kwanini? Umemuweka Zitto wa kwanza kwanini? Una agenda....aliyekutuma uwange mwambie hatujalala,,,,,,,,, sikuwajua kuwa ndivyo walivyo utadhani malaika wanuru,,,, ukichunguza,,,,, gambaz at work
   
 11. M

  Mercyless JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 652
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kumuwajibisha kiongozi mzembe na mvivu sio udikteta ndugu zangu. Mbona wakati wa uongozi wa Mwl. Nyerere na Sokoine viongozi wote waliokuwa chini yao walijituma na kufanya kazi kwa bidii kwa kuogopa kujibishwa? Tatizo lililopo sasa hivi ni kupeana madaraka kwa kujuana au kulipa fadhila.
  Mimi sioni kama kumuwajibisha waziri au Mbunge ni udikteta!!
   
 12. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  Mkuu Mbowe ni kiungo kikuu cha chama,,,na hana muda wa kuwa rais kwan anawaamini wale wote watakaoteuliwa na chama,,,na hilo watz wanalifahamu,,,,mbowe atabaki kama mgombea ubunge na baadaye kuja kuteuliwa kuwa waziri mkuu kutokujali ni kiongozi gani atakayechaguliwa ,,haijalishi atatoka ccm cdm au cuf ila jua atakuwa waziri mkuu wa nchi hii najua hutaweza niamini kwa haraka lakini utajua baada ya katiba mpya ikitoka..
   
 13. masatujr1985

  masatujr1985 JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2012
  Joined: Oct 27, 2011
  Messages: 1,933
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 180
  Bora aje huyo dikteta kuliko kuwa na democrat ambaye ni mzururaji na mbabaishaji (unconcerned).
   
 14. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Hahahahahaha!!!
  Interesting!
   
 15. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #15
  May 18, 2012
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ...Kama ulikuwa unafuatilia yaliyoendelea katika kikao cha ccm dodoma, utagundua kuwa wameshtuka na kupendekeza masuala ya coalitions katika kutawala serikali yawekwe kwenye katiba mpya.

  ...Possibly.

  ...Ni kweli. Lakini si lazima tupate rais dikteta come 2015. Well, lets wait and see.
   
 16. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #16
  May 18, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Sidhani kama yote ulosema yatakua kweli,lakn jambo zuri tumuombe Mungu CDM ishinde bila mizengwe yoyote
   
 17. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #17
  May 18, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Nilianza kusoma kwa hamu lakini nilipofika namba 4 ndiyo nikaishia hapohapo. Hivi kwa watu msiyoelewa Freemasonry huwa mnakuwa wa kwanza kuitaja? Freemasonry imekuwepo Tanzania tangu enzi za mkoloni alipotia mguu hapa, mbona hatukuona watu waliowapinga wakoloni wakitoweka sababu ya Freemasonry?
  Mnakera sana, siku hizi kila kona ukipita, magazeti ya udaku, redioni, yaani kila mtu neno lililokaa mdomoni ni Freemasonry tu.
  Jifunze kitu ukielewe ndipo ukizungumzie, vinginevyo unaleta kichefuchefu tu.
   
 18. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #18
  May 18, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,959
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  freemason si dini ya kishetani. Jifunze
   
 19. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #19
  May 18, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  ni kweli kuwa watanzania wanategemea sura moja wapo kati ya hizo lakini hakuna sura ya udikteta hapo wote hao ni watu wa democracia kwa wingi.
  ila tukitaka tuendelee nakubaliana na wewe kuwa udikteta wafaa.ila uwe ule wakuleta maendeleo
   
 20. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #20
  May 18, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,157
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo hii katiba mpya tunayoipigania unataka kuniambia kuwa tunaitunga iruhusu haya uliyoyaandika yatokee au kichwa kimefeli hata kuwaza japo kidogo
   
Loading...