Kuani msibani na sherehe Kunavyochangia Kuenea kwa ugonjwa wa malaria

Nov 20, 2018
45
30
Jamani sote tunajua malaria ni ugonjwa gani ?Moja ya jambo gumu na ambalo limeshindwa kufanyiwa utafiti na wasomi wetu ni hii kadhia ya kuhani msibani na sherehe mbali mbali Kama harusi ndo chanzo kikuu Cha kuenea huu ugonjwa wa malaria Barani Afrika kwa ujumla,samahani kwa mtakao ona kma nimewakera lakini ukweli ndo huo na siku zote ukweli unauma na huu ugonjwa uenezwa msibani kama ifuatavyo;

Kuhani msibani kwa muda mrefu bila ya kutumia chandurua.
utamaduni wa kwenda kufariji mfiwa kwa kulala msibani na hii ni karibu maeneo yote ya Mjini na vijijini na huu utamaduni umekuwepo na ni wa kurithi vizazi na vizazi na watu wanaenda kuhani msibani bila kuwa na tahadhari yoyote kama ya kuchukua chandarua kwa ajili ya kujikinga na mbu waambukizao malaria kwani huchukulia poa tu, hivyo kuambukizwa malaria kiurahisi.Na huu utamaduni umekuwa ukifanywa na majirani, ndugu wa karibu na ndugu wa mbali kwani ulazimika kufunga safari kwa ajili ya kwenda kuhani na husiombe huo msiba ukawa ni wenye uwezo (matajiri) acha bhana Kuna watu umaliza mpaka wiki tatu wakihani!
Kwani kufurahia chai,ubwabwa na nyama zinazopatikana msibani hapo! sio kwamba natania na ninataka kuzuia watu wasiende kuhani jamani msinielewe vibaya nisije nikaitwa mchochezi!na Kama Kama Kuna mtu mzima hajawahi kufanya hivyo anyooshe kidole juu .

Sherehe Kama harusi,hii sana sana imejikita vijijini watu huchukua muda mrefu wakila, kucheza disko na kunywa mpaka zaidi ya wiki huku wakilala bila Ya kuchukua tahadhari kama ya kutumia chandarua wakati wa kulala usiku hivyo kujikuta wakiambukizwa malaria makumi kwa maelfu na hivyo kuipa gharama serikali ya kuwatibu.


Nini kifanyike ili kuzuia hili janga
Kwa mtazamo wangu ningeiomba serikali kuchukua tahadhari na Kwa njia mathubuti Kama ifuatavyo;

Kutengeneza vyandarua vya uma vitakavyochukua watu watano watano kwa ajili ya misiba na sherehe ili kuwalinda Wazee, watoto wanawake na vijana kwa ujumla wanaoenda kuhani misibani na kwenye sherehe mbali mbali Kama harusi badala ya kujikita kutengeneza vyandarua vya watu wawili wawili ,sikatai ni jambo zuri lakini huku kwenye misiba na sherehe serikali imejisahau au haijuhi kabisa kwani nguvu kazi inateketea bure bila ya kuchukua tahadhari!

Serikali kutoa elimu kwa uma juu ya msisitizo wa kuambukizwa huu ugonjwa watu wanapoenda kwenye misiba au sherehe hivyo watu wachukue tahadhari mapema!hivyo jamii itakuwa imejikomboa kifikra na kuachana na kukariri kwamba huu ugonjwa uambukizwa bila ya kulala na chandarua eti ukiwa ndani wakati Kuna njia nyingine Kama nilizotaja hapo juu na zimejificha ni vigumu watu kulijua hilo.

Hivyo basi naomba kuwasilisha kwenu hii nadharia yangu kwenu kwa ajili ya kuichakata na nawaombeni kura zenu!ili tuweze kuisadia jamii yetu inayoangamia kidogo kidogo mithili ya mtu aliye na ugonjwa wa kansa kwa kukoswa maharifa yenye mawanda mapana ya kuelimisha.
By katotojunior5@gmail.com
0764100526/0715000590
 
Back
Top Bottom